Mnyasikoma
Member
- Oct 17, 2014
- 30
- 13
Kwako Gerson Msigwa na Serikali kwa ujumla
UTANGULIZI
Foleni jijini Dar es Salaam imekuwa kikwazo kikubwa cha uchumi, muda wa uzalishaji, afya ya wananchi na taswira ya taifa. Kitovu cha msongamano mkubwa kinaanzia Morogoro Road na Mandela Road kupitia Tabata hadi Mbezi, na hii inahitaji mkakati wa haraka, wa kitaalamu na wa muda mrefu.
1. UJENZI WA FLYOVERS MAENEO MUHIMU
Pendekezo la kujenga flyover katika maeneo yafuatayo:
2. VITUO RASMI VYA DALADALA KILA BARABARA
3. UDHIBITI WA MALORI MJINI NA BANDARINI
6. UDHIBITI WA BIASHARA NA USAFIRI MDOGO
9. KUHAMISHA HUDUMA NJE YA MJI
UTANGULIZI
Foleni jijini Dar es Salaam imekuwa kikwazo kikubwa cha uchumi, muda wa uzalishaji, afya ya wananchi na taswira ya taifa. Kitovu cha msongamano mkubwa kinaanzia Morogoro Road na Mandela Road kupitia Tabata hadi Mbezi, na hii inahitaji mkakati wa haraka, wa kitaalamu na wa muda mrefu.
1. UJENZI WA FLYOVERS MAENEO MUHIMU
Pendekezo la kujenga flyover katika maeneo yafuatayo:
- Mwenge
- Kamata
- Morocco
- Njia panda ya Tabata
- Fire
- Aggrey – City Centre
- Karume
2. VITUO RASMI VYA DALADALA KILA BARABARA
- Kuwe na vituo rasmi hata kwenye barabara zenye mwendo kasi.
- Askari wa trafiki wawe wakali kuhakikisha daladala hazisimami njiani.
- Mfumo wa faini kali kwa ukiukaji.
3. UDHIBITI WA MALORI MJINI NA BANDARINI
- Malori yapangiwe ratiba maalum ya kuingia mjini.
- Yatumiwe zaidi usafiri wa reli kupitia Tanzania Railways Corporation.
- Yatengwe maeneo maalum ya kusubiri mizigo nje ya mji.
- Bandari pia iwe na uratibu mzuri ili foleni ya mizigo isisambae hadi mitaani.
- Roundabout zote ziongezwe ukubwa.
- Ziwe na lane maalum ya kuingia na kutoka kabla ya kuungana na barabara kuu.
- Misafara ya viongozi isiwe kikwazo kwa wananchi kwa kuziba barabara muda mrefu.
- Mataa yawe smart traffic lights yanayodhibitiwa kwenye control centre.
- Kamera za CCTV ziwe sehemu ya mfumo.
- Faini kali na za kielektroniki kwa wanaokiuka sheria.
6. UDHIBITI WA BIASHARA NA USAFIRI MDOGO
- Wafanyabiashara waondolewe kwenye hifadhi za barabara na watembea kwa miguu.
- Punguza boda boda, mikokoteni na vyombo visivyopaswa katikati ya mji.
- Toa maeneo rasmi ya biashara nje ya barabara.
- Punguza parking za kiholela za manispaa.
- Tengeneza maeneo machache makubwa (central parking yards).
- Sheria iwe: majengo mapya lazima yawe na parking kubwa ground floor.
- Badilisha 2-by-2 kuwa 3-by-3 lanes barabara kuu.
- Boresha barabara za mkato ili kutawanya magari:
- Kinyerezi – Maji Chumvi
- Mbezi – Chanika – Mloganzila
9. KUHAMISHA HUDUMA NJE YA MJI
- Punguza kurundika masoko, vyuo, hosteli, ofisi na maduka makubwa sehemu moja.
- Panua jiji kwa kupeleka huduma pembeni.
- Mfano: mrundikano wa shughuli maeneo ya Kariakoo na Posta ni chanzo kikubwa cha msongamano.
- Panua miundombinu ya Dar Rapid Transit (DART).
- Ikiwezekana kuwe na usafiri maalum ndani ya CBD.
- Bajeti iongezwe kwa sababu hii ni suluhisho la muda mrefu.
- Zuia malori mabovu kuingia mjini.
- Ukaguzi mkali wa ubora wa magari.
- Tanzania isiwe dampo la magari chakavu.
- Msongamano wa watu katikati ya mji
- Parking kiholela
- Mrundikano wa huduma sehemu moja
- Uharibifu wa magari barabarani
- Kukosekana kwa vituo rasmi
- Malori mengi mjini
- Uratibu mbovu wa bandari
- Roundabout hafifu
- Usimamizi dhaifu wa trafiki
- Misafara ya viongozi kuziba barabara
- Kuwe na yard maalum nje ya mji.
- Mtu binafsi apaki gari lake hapo, alipe parking fee, apande mwendo kasi au usafiri maalum kwenda katikati ya mji.