Mdude_Nyagali
Member
- Dec 11, 2022
- 79
- 1,444
Kutokana na mahakama ya Africa kutengua wakurugenzi kusimamia uchaguzi Tanzania na kuagiza serikali kufanya marekebisho ya sheria ya uchaguzi ndani ya miezi 12 nilikuwa na mapendekezo yafuatayo.
Napendekeza tume ya uchaguzi iundwe katika mfumo ufuatao.
1. Tume iwe na wajumbe 10 ambao watapendekezwa kwa mgawanyo sawa kuanzia ofisi ya Rais, Vyama vya siasa, Asasi za kiraia na za kidini.
2. Kwamba wajumbe hao 10 watakaopatikana kupitia Utaratibu huo wataapishwa na baada ya kiapo wataanza mchakato wa kupendekeza majina ya Mwenyekiti na Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi miongoni mwao.
3. Kwamba baada ya hatua ya hiyo, hatua inayofuata iwe ni tume hiyo kuteuwa wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kwa kutangaza Sifa za waombaji kwa kuzingatia matakwa ya kisheria.
4. Kwamba tume ya uchaguzi iwe ni taasisi huru inayojitegemea kuanzia utendaji wake pamoja na watumishi.
4. Tume hiyo inapaswa kulindwa na sheria ili isiwajibike kwa mamlaka zozote isipokuwa mahakama.

Upvote
1