PreGE2025 Mapendekezo ya Mgawanyo na Mabadiliko ya Majimbo kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

PreGE2025 Mapendekezo ya Mgawanyo na Mabadiliko ya Majimbo kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Mgawanyo wa majimbo ya uchaguzi ni hatua muhimu katika mchakato wa Demokrasia nchini Tanzania.

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) inawajibika kuhakikisha kuwa majimbo yanagawanywa kwa kuzingatia vigezo kama idadi ya watu, jiografia, na mahitaji ya uwakilishi wa wananchi.

Katika Uchaguzi Mkuu wa 2025, mgawanyo wa majimbo umefanyiwa marekebisho ili kuhakikisha uwiano mzuri wa idadi ya wapiga kura na maendeleo ya kisiasa.


Baadhi ya Majimbo ambayo yamependekezwa Kugawanywa na kubadilishwa majina ni pamoja na

Yanayogawanywa


Yanayobadilishwa majina
Njombe
- Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Njombe Yajiridhia Kubadili Jina la Jimbo la Njombe Mjini kuwa Njombe Kusini

Yaliyopingwa
Arusha - Baraza la Madiwani wagoma kuligawa jimbo la Arusha mjini mara mbili
Kilimanjaro - Pre GE2025 - Mbunge wa Moshi Vijijini Prof.Ndakidemi Apinga mpango wa kuligawa Jimbo hilo kwa kuwa hauzingatii maslahi ya wananchi

Maoni ya Wadau
 
Watanzania ndo watazidi kuwa masikini kwa kuongezeka mzigo mwingine wa pesa nyingi kutumika huko daaah!
Maana hayo maposho,mishahara n.k ni mikubwa sana kawa hayo majimbo na wabunge .
 
Wanasiasa wengi wamelaaniwa.Kufanya siasa kama ajira ni laana.Idadi kubwa ya vijana wasio na ajira wala uthubutu wa kujiajiri inaendelea kuongezeka. Wapo vijana wanaokwama elimu ya kati na ya juu sababu ya ada LAKINI huku wengine wanagawana keki kimtindo.
Wabunge au madiwani wamesaidia nini katika maendeleo ambacho wataalamu hawawezi? Africa should change otherwise poverty will stay and nourish on their land forever
 
Ninachokiona majimbo yote 230 yatagawanywa na hii tume fake ya kijiga yawe 460 na hakuna la maana wanachoenda kufanya, kama majimbo ni makubwa si watuachie sisi tupo tayari kuzunguka Wilaya nzima, Zanzibar nao watayagawa yawe 100 jumla tutakuwa na majimbo ya uchaguzi 560
 
Ninachokiona majimbo yote 230 yatagawanywa na hii tume fake ya kijiga yawe 460 na hakuna la maana wanachoenda kufanya, kama majimbo ni makubwa si watuachie sisi tupo tayari kuzunguka Wilaya nzima, Zanzibar nao watayagawa yawe 100 jumla tutakuwa na majimbo ya uchaguzi 560
Mbona 560 ni machache? Tunataka Mabalozi wa Nyumba Kumi ndio wawe Wabunge! Daaadeki!!
 
Back
Top Bottom