Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Ili kupunguza matumizi ya fedha taslimu katika mwaka 2026/27 inapendekezwa kufanya maboresho yafuatayo:
Kuweka sharti la baadhi ya malipo ya huduma na biashara kufanyika kwa njia za kidijitali kama ilivyoainishwa katika Aya Na. 61;
Kusitisha usambazaji na matumizi ya vocha za kukwangua za muda wa maongezi (scratch cards) katika maeneo yote ya mijini yenye miundombinu wezeshi ya malipo ya kidijitali;
Kuweka sharti la matumizi ya vifaa vya malipo ya kidijitali (Lipa Namba na TANQR) kama moja ya kigezo wakati wa utoaji na uhuishaji wa leseni ya biashara;
Kuweka sharti la kufungua akaunti ya benki kama moja ya vigezo vya utoaji wa leseni kwa wafanyabiashara wanaoshiriki katika shughuli za madini, mifugo, mazao, mbao na uvuvi na kuhakikisha miamala inafanyika kupitia akaunti husika; na
Kuweka sharti la uthibitisho wa malipo ya kidijitali kuwa rejea ya lazima itakayotumika kuidhinisha maombi ya uhamishaji wa mali kama vile ardhi, majengo na magari kama ilivyoainishwa katika Aya Na. 64.