SoC02 Mapendekezo yatakayoleta mabadikiko chanya katika elimu ya kitanzania, Hasa kuifanya elimu iwe ya kufurahia na isiyo chosha kwa wanafunzi

SoC02 Mapendekezo yatakayoleta mabadikiko chanya katika elimu ya kitanzania, Hasa kuifanya elimu iwe ya kufurahia na isiyo chosha kwa wanafunzi

Stories of Change - 2022 Competition

Change for tomorrow

New Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
2
Reaction score
1
Elimu ni mfumo wa mafunzo yanayopatikana shuleni , vyuoni , na maishani .(nukuu kutoka kamusi ya kiswahili sanifu). Elimu huwasilishwa kwa njia mbili; nazo ni elimu rami na elimu isiyo rasmi . Elimu rasmi kutolea na walimu wenye sifa na juzi wa kufundisha wakati elimu isiyo rasmi ipo nje ya taasisi rasmi za elimu ya jamii na haina mpangilio( ).

historia fupi ya elimu Tanzania;
kabla ya ukoloni
, watu walijifunza kupitia hadithi , nyimbo za asili , unyago , pia na kazi zilitengwa na kufundishwa kadri ya umri wao mfano mzuri ni " wamaasai"

kipindi cha ukoloni, (karne ya kumi na nane). Elimu iliwasilishwa kwa Lengo la kuwanufaisha wazungu /wakoloni.

baada ya ukoloni , mnamo mwaka 1962 , hayati Julius kambarage Nyerere aliona ni vyema idadi ya wasomi iongezeke. Hivyo basi shule zilianzishwa kwa dhumuni la kukomboa uchumi wa Tanganyika na mpaka sasa hivi tuna taasisi ya wizara ya elimu , sayansi na teknolojia inayoshugulika na mambo ya elimu tanzania .

mapendekezo yangu ni kumshirikisha kila mtu kwenye kuiboresha elimu ya kitanzania . Mpaka hivi sasa serikali pamoja na raia wake tunalalamika mfumo wa elimu ni mbovu ya kwamba unatumia ujuzi wa vitabu kwa sana bila kufanya vitendo . Kwa kingereza tunasema "education system is more theoretical rather than practical
" hivyo basi ni jukumu letu kuanza kuiboresha elimu yetu wenyewe . Mfano wa kuigwa ni tajiri mmoja duniani "Elon Musk" ambaye ameanzisha shule yake "Ad Astra" yenye elimu ya kipekee aliona kuna umuhimu wa kubadilisha mfumo wa elimu . hivyo basi alianzisha mtindo mbadala wa kujifunza ambao unafanya wanafunzi kujifunza kwa vitendo , hii husaidia wanafunzi kutokukariri na kuwa na uelewa mpana , pia kugundua maslahi, nguvu na vipaji vya watoto.
yafuatayo ni vichocheo vitakavyo leta mabadiliko chanya katika jamii kwenye nyanja ya elimu :
  1. kuweka msisitizo juu ya ubunifu wa kufundisha ; elimu inapaswa kuwa ya kufurahisha na sio ya kuchosha. Walimu na wanafunzi wabunifu wanapaswa kuwasaidia wanafunzi wengine katika kurahisiha mchakato wa kujifunza na kuelewa kwa wanafunzi kwa mfano
  • utumiaji wa michoro mfano jedwali mdwara
  • utumiaji wa katuni kwenye vitabu
  • utumiaji wa nyimbo katika kuwasilisha elimu
  • kutoa muhtasari unaoeleweka
  • ziara za kimasomo
2. Ukuzaji wa talanta za watoto ; elimu ya Tanzania yapaswa kukuza talanta mbalimbali za wanafunzi kama vile uimbaji, uchoraji pamoja na upambaji . Elimu hii iimeshindwa kukuzwa kutokana saikolojia ya wazazi wengi kuwa, elimu juu ya uimbaji, upambaji na uchoraji hazina maana ilhali kazi zote zina umaana katika jamii . Mfano mzuri ni watoto wengi endapo huwaambia wazazi wao wanataka kuwa wanamuziki , utakuta wazazi wao huwakataza na kuwaambia wasome sana baadae wapate kazi zenye heshima kama udaktari , hivyo basi mtoto hatoweza kuendeleza kipaji chake . elimu juu ya uimbaji, upambaji , na uchoraji zote zikiwekwa na usawa mmoja hivyo basi maendeleo katika nchi yetu yatakuwa makubwa mno . Na pia itasaidia kutatua tatizo la Ajira kwa kuwawezesha vijana kutumia vipaji/ talanta zao.

3. Kupiga marufuku uuzaji wa vitabu ambayo havijathibitishwa na wizara ya elimu; idadi kubwa ya waandishi wadogo wadogo wa vitabu ambayo havijathibitishwa na wizara ya elimu huwapotosha wanafunzi . Vitabu hivi vidogo vinavyojulikana sana kama "vitini" vya masomo mbalimbali . Vitini vingine kufundisha kinyume na silabasi hivyo kuwapotosha wanafunzi wengi katika masomo yao .

4.kukazia sana juu ya elimu ya vitendo ; elimu ya Tanzania iwe na msingi wa nadharia na vitendo ili kurahisisha uelewa wa mwanafunzi. Elimu ya vitendo husaidia wanafunzi kukumbuka zaidi kuliko kukamia, pia itawasaidia kujua wapi wanatakiwa kuitumia kwenye maisha .kwa mfano ukosefu wa maabara na vifaa vyake kwenye shule za serikali imepunguza uelewa mzuri wa wanafunzi .

5.kubadilisha mtazamo kwa jamii; jamii yapaswa kuwa na mtazamo hasi , kwamba masomo ya sayansi pamoja na ya Sanaa, yote yana vipaumbele sawa. Jamii huichukulia kuwa masomo ya sayansi ndo yanastahili kipaumbele kuliko ya sanaa , mtazamo huu umepelekea upungufu wa nguvu kazi kwa wanafunzi wa sanaa na biashara na kupelekea matokeo yasiyoridhisha.

6.walimu hawapaswi kuwakatisha tamaa wanafunzi, kwa kuwatisha kuwa elimu ya juu ni ngumu sana . hivyo kutengeneza hofu kwa mwanafunzi . Walimu pamoja na wazazi yawapasa kuwapa moyo wanafunzi. Na ni jukumu la mwalimu kumsaidia mwanafunzi ambaye uelewa wake ni mdogo kwa kujua ni namna gani ya kumsaidia mwanafunzi .hii itamuongezea mwanafunzi mtumaini na jitihada za kufanya vizuri kwenye masomo yake .

Hitimisho
Andiko hili linasisitiza / kutoa mapendekezo juu ya mfumo wa elimu utakavyoboreshwa kwa vichocheo vilivyotajwa halo juu, ili kuleta mabadiliko chants katika jamii. Mabadiliko haya unahitaji muda , uelewa, na utayari wa kila mtu ili kuiboresha elimu yetu.

Mfano wa kuigwa ni kutoka kwa tajiri mmoja wapo wa duniani "Elon Musk" ambaye amechukua hili jambo na kuanzisha shule yake inayoitwa "Ad Astra" shule hii inatoa elimu ya kipekee na ni mradi wa maendeleo, wanafunzi kujifunza kivitendo badala ya kutegemea ujuzi wa kitabu tuu . Hivyo basi Elon Musk ametambua umuhimu wa kubadilisha mfumo kwenye shule zetu .

Kwa kuongezea; faida tutakazozipata tukiboresha elimu ya vitendo ni:
  • Huwezi wa kuchambua tatizo na kupata ufumbuzi sahihi
  • Uelewa wa kina wa shaba mbalimbali
  • Hukuwa maarifa na juzi wa mwanafunzi
  • Msingi wa ukuaji na maendeleo.
Asanteni sana.
 
Upvote 6
Back
Top Bottom