Mapenzi bila mawasiliano

marandu2010

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2010
Posts
1,201
Reaction score
446
Nina msichana ambaye kwa mwaka mmoja hatujawasiliana,,,baada ya mwaka mmoja akanibip na kuniambia mawazo yake yako palepale..

Kumbuka hatujawasiliana kwa mwaka mzima,,kutokana na yeye kuwa hana simu,,na mimi siku zote ili nibidi anibip ili nimpigie tuwasiliane,,,lakini mwaka mzima ulipita hajanibip...baada ya mwaka mmoja akaniambia mawazo YAKE yako palepale,,hajabadili mawazo...

Baada ya kuzuNGUmza naye hapo,,sasa imepita miezi saba hajanibip tena,,sasa najiuliza kuna mapenzi kweli kwa ufinyu huu wa mawasiliano.????? Na nifanyeje???
 
It seems you don't love her....! Nawe ungechukuwa hiyo namba na uwe unamtrace kupitia namba hiyohiyo...! Au ungefunga safari ukakutane naye, au ungemwezesha aje ulipo...! Hata hivyo wewe unaonekana kama vile uko tayari kwa lolote, lakini tamaa zinakuandama...! Yaani unataka kummega lakini umekuwa occupied already...! Otherwise, Let the nature take place...!
 

I couldn't have put it better..............................................
 
Arrgh! Mambo mengine bana ; Kweli weye mchaga....unaona ubahili kumnunulia dem hata simu ya kitochi................mie nakwambia ukifanya masihara wenzio watachukua huyo dem jumla na hutakaa umuone tena.next tyme mnakutana naye anapakata katoto........yaaani huoni hata aibu kujisema weye ni bahili namana hii?
 
Siku hizi kuna simu za kichina za mpaka 15000 acha ubahili wewe mnunulie uwe unamtumia voucher na akiishiwa akubeep kiurahisi just very simple we usubiri mpaka aombe simu abeep? acha hizo bwana
 
Siku hizi kuna simu za kichina za mpaka 15000 acha ubahili wewe mnunulie uwe unamtumia voucher na akiishiwa akubeep kiurahisi just very simple we usubiri mpaka aombe simu abeep? acha hizo bwana

Dena laway??
 

1.Onesha mapenzi ya kweli kwa kumtafuta kwa njia yeyote ile.
2. Mnunulie simu na uwe unamtumia vocha ili kuboresha mawasiliano.
3. Acha kumpotezea muda ikiwa huko seriasi naye.
 
Okey,,yeye yuko shule,na huko shule simu haziruhusiwi kabisa wala harusiwi mtu kumtembelea labda baba yake tu tena kwa masharti makubwa,,akaniambia atakuwa ananishtua yeye na sio mimi kipindi cha likizo,,lakini hajatekeleza ahadi hiyo,,ninajaribu kumtafuta kwa namba aliyokuwa anatumia lakini hapatikani,na anaishi mkoa mwingine,na siwezi kuonana naye hata nikienda kwao kwa sababu ni geti kali sana,sasa imepita miezi minane.hiyo ndiyo hali halisi..

Mimi ninampenda huyu binti,,na ninajitahidi kwa njia mbalimbali kumtafuta,,njia pekee ninayoitegemea ni hiyo simu itakapopatikana,,na labda likizo ya mwezi wa kumi na moja ikiwa atanitafuta...lakini kukaa muda mrefu bila kunitafuta,,nina mashaka sana...japo mimi ninaendelea kutulia kumsubiri,,lakini mawasiliano finyu kiasi hiki yananitia mashaka..

Asante wote kwa michango yenu mizuri.
 
aaaagh, acha wanafunzi wapate elimu bana badala ya kuwapotezea mwelekeo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…