lakini ni asilimia ngapi wanaoanzisha mapenzi chuoni wanakuja kuoana na hao wapenzi wao? Kama sio pass time
Asilimia ni ndogo sana. Nakumbuka wakati naingia chuo ulikuwa wakati serikali ilipoanzisha zile juhudi za kuwa na wasichana wengi vyuo vikuu. Watu tulifurahia hiyo, lakini tulikuwa tunapigwa vibuti ile mbaya. Yaani ilikuwa vingumu kumtongoza mtoto wa chuo akakubalia. Walikuwa wanajiconsider kama high class. Labda hali imebadilika kwa sasa.
Kwa experience yangu ya chuo wakati huo,nwasichana wengi walikuwa wakitembea na wanaume wa mtaani. Na hawa wanaume walikuwa sio uchwara. Walikuwa ni wanaume wenye pesa zao za kutanua. Ilikuwa ikifika ijumaa jioni unaona tuu magari binafsi yantinga cumpus kupick up girls. Wasichana wa chuo walikuwa na hulka ya kutowadate wanaume wa chuo kwa sababu tulikuwa tunapata income sawa. income yenyewe tulikuwa tunaiita ngororo (jina la aliyekuwa katibu mkuu wa wizara ya sayansi, teknologia na elimu ya juu wakati huo).
Kuona hivyo wanaume wa chuo nao wakaamua kwenda kudate mtaani. Pia ilikuwa kipindi hicho ambacho wamaume walikuwa wakiwaajiri mahousegirls kwa nia ya kuwapikia, kupiga soap soap room, na wengine walikuwa wanajishindia hapo hapo. Tulikuwa na pesa kipindi hicho.
Interesting thing ni kuwa tulipokuwa mwaka wa mwisho wasichana wengi walijikuta wako single. Ilionekama kama vile wale wanaume wa mtaani walikuwa hana long plans na hawa wasichana. By the way, walishakuwa wakubwa na hawakuwa tena na ule mvuto wa first year. Hapo sasa walijaribu kujiaatch tena na wanaume wa chuo lakini haikuwezekana b'se these guys have already moved on. In addition, walikuwa tayari walishajua CV za hawa wasichana, so they were no longer interested in them. Pia wakati huo kulikuwa na wanaume chuoni na mitaani waliokuwa na zile fikra za kutooa wanawake waliopiga shule.
Wasichana ambao walikuja kuolewa na watu waliokuwa nao chuo ni wachache. Tena wengi wao walikuwa tayari na mahusiano hata kabla ya kuja chuoni. Wanaume wengi walienda kuoa mitaani. Pia baadhi ya wasichana waliolewa na watu wa mitaani lakini bado kuna ambao wapo single though walikuwa na life kiaina chuoni.