Mr Kachila
Member
- Jul 31, 2022
- 5
- 1
Mapenzi; unaposikia neno mapenzi moja kwa moja unapata tafsiri yake binafsi katika ufahamu wako. Wengi huelezea maana yake kutokana na mtazamo aliopo nao, mfano; matazamo wa kidini, kimazingira yanayomzunguka na hata kimahusiano. Binafsi neno mapenzi, kwa kawaida hubeba hisia za ndani zisizoelezeka, za kudumu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine. Bila shaka msomaji wa makala hii huenda ukapigwa na butwa ni kwa namna gani mapenzi yanaiendesha dunia.
Kutokana na visaga, visa na wivu wa wenza(wapenzi) pale wanapohitilafiana husababisha athari kubwa kutokea katika jamii kama vile; mauaji na ukatili wa kijinsia na mengine mengi. Ni dhahili siku zote mapenzi yamekuwa yakiongeleka kila kona ya dunia, iwe kwa taarifa ya habari na mitandao ya kijamii. Yafuatayo ni madhara na athari za mapenzi katika dunia tuliyonayo kwa jamii;
Kuvunjika kwa ndoa, siku hizi ndoa nyingi hazidumu hii ni kutokana na usaliti wa mapenzi unaozidi kuiangamiza dunia kila kukikucha. Mapenzi yamekuwa hayatulii kwa mtu moja, hivo kupelekea uvunjifu wa ndoa nyingi ambapo kwa upande wa jamii hujaza watalakiwa na hata watoto wa mitaani ambapo wazazi wanapotengana huenda mzazi atakaye kaa na watoto kushidwa kumudu gharama za kuwahudumia watoto, pia hupelekea ongezeko la tabia baya kwa vijanaa ambao hupata malenzi ya upande mmoja wa wazazi.
Mauaji; wivu, visaga na visa vya mapenzi yasiyo na uadilifu kila siku yamekuwa chanzo cha mauaji kwa watu wa rika zote haswa kwa vijana. Mitandao ya jamii imekuwa ikiripoti kila siku juu ya mauaji yanayotokana na mapenzi, hii hali inapelekea kuwa poteza ndugu, jamaa na marafiki ambao hutuachia majonzi na pengine watoto yatima. Vile vile mauaji yanayotokana na mapenzi yamekuwa pingo kwa taifa kwa ujumla ambapo tunapoteza nguvu kazi ya taifa.
Kushuka kwa ufaulu mashuleni; katika upande wa taaluma haswa mashuleni ufaulu wake unaporomoka kwa kasi, hii yote ni sababu ya mapenzi kuwashika vijana ambao huishia kujisahau nini wanatakiwa kufanya wakiwa mashuleni. Pia katika mashuleni mapenzi yamechangia kwa kiwango kikubwa katika maambukizi ya ukimwi sambamba na watoto wa mitaani ambao ni janga kwa sio jamii tu hata taifa kwa ujumla.
Ukatili wa kijinsia; visa na wivu wa mapenzi yamekuwa chachu ya ukatili wa kijinsia katika jamii zetu ambapo si jinsia ya kike wala ya kiume imekuwa wahagha wa ukatili wa kijinsia. Huu ukatili wa kijinsia unakuja kwa mauaji hata kwa utelekezwaji wa watoto kwa upande wa mzazi wa kike, mara zote huja pale mzazi wa kiume kutekwa kimapenzi na mpenzi wa nje(mchepuko).
Chanzo cha watoto wa mitaani, janga la hawa watoto linatokana na usaliti na utelekezwaji wa watoto wa wanandoa ambapo wanapopatwa na migogoro ya kimapenzi hujikuta wanawasusa hata watoto wao wasio na hatia. Watoto wa mitaani katika jamii zetu wamekuwepo wakitesa na ungumu wa maisha ambapo wengi wao huishia kujihusisha na uovu kama vile; wizi, ukabaji, ujambazi na hata ukahaba kwa upande wa watoto wa kike. Adhari na madhara ya mapenzi katika dunia hayana budi kuzibitiwa kwani ni hatari na yanagharimu maisha ya vijana na hata wazee. Zifuatazo ni mbinu na njia ambazo kwa namna moja zinaweza saidia na hata kuondoa haya madhara na athari za mapenzi yanayo tikisa dunia kwa nguvu. Moja ya hizo njia ni kama vile;
Uwepo wa sheria na adhabu kali, ili kukomesha majanga yanayo sababishwa na mapenzi ni utungaji na utolewaji wa sheria na adhabu kali kw wahusika wa uovu huo zidi ya wenza wao. Adhabu kali kama kunyogwa kwa mhusika wa mauaji yatokanayo na wivu wa mapenzi huenda ikawa fundisho kwa wengine kutodhubutu kufanya uovu huo.
Utoaji elimu kuhusu madhara na athari za mapenzi, elimu juu ya uovu kama mauaji, ukatili wa kijinsia na mengine mengi kuhusu mapenzi inatakiwa kutolewa kwa vijana ambao mara nyingi ndo wahusika wa machafu kuhusu mapenzi yasio adilifu.
Uwepo wa dawati la kusikiliza migogoro ya wapenzi, dawati mahususi kwa ajili ya kusikiliza kesi na migogoro ya wenza wa mapenzi linapaswa kufunguliwa ili lishughulike na migogoro ya mapenzi kwa wenza ambapo bila shaka litasaidia kwa upande wake katika kupunguza na hata kuondoa machafuko ya matukio mabaya wa visa vya mapenzi.
Kwa kuhitimisha, suala la mapenzi kuishika na kuiendesha dunia linapaswa kuchukuliwa kama janga litakalo iangamiza dunia kiuchumi, kisiasa na hata kijamii kwa siku za usoni, kutokana na machafuko haswa ya mauaji ya wivu wa kimapenzi kushamili kona ya dunia.

Upvote
0