Jamani tusikimbilie kuhukumu kwamba mke kamuua mwenza, tu kwa sababu kaamua kuishi na serengeti boys.
Kupata mwenza mara kabla ya kutimiza kukaa eda integemea na mtu.
Mimi binafsi naamini kuwa:
1. mfiwa anaweza kuamua kuoa/kuolewa haraka kutokana na maumivu ya upweke. Ukizingatia ni mama amefiwa na mume, inatisha kulala peke yako. Hebu niambie baada ya kufiwa na kuzika palikuwa na ndugu waliokaa na mama huyo kumpa company? kama hana ndugu au rafiki wa kuwa naye karibu huenda ni hali hiyo imemfanya apate mwenza haraka ili kuondoa upweke. Ingawa kiutamaduni wa mwafrika ndo tunapeana uchawi tena.
2. Mfiwa naaweza asiowe/asiolewe kwa kuwa haoni kama atapata wa kuziba pengo, wapo wengi waliooshi bila kuoa au kuolewa baada ya kufiwa.
Ukiacha taratibu za kimila n.k. kuoa au kuolewa muda mfupi baada ya kufiwa inabidi tumwachie mhusika mwenyewe, hatujui nini kitamsaidia kupata usingizi na aendelee kuishi.
Naomba msimtenge huyo mama, maana majirani nao ndo kama hivyo washaanza, ooh, kaua ili aolewe. TUSIHUKUMU mwachieni Mungu ahukumu kila moja kwa dhambi aloitenda.