Mapenzi Mapenzi Mapenzi aah jamani aua sababu ya penzi zito kwa...


issue hapa ni mme alikufa na mke akaolewa ndani ya mwezi ..na kwa sababu ilikuwa very short time ndo maana watu waliwaza wanayojua wao Kwa binadamu mwenye akili timamu hawezi fanya hivi ,,,,hata wewe mdada siamini kama unaweza fanya hivi-no labda unaweza nisiusemee moyo
 

1.Kuhusu kama naweza kufanya hivyo au la..nadhani post yangu imeanza na disclaimer...kuwa sifagilii wala kuunga mkono hicho kitendo cha kukimbilia kuolewa...

2. HUTUJUI UNDANI WA KILICHOKUA KINAENDELEA BAINA YA HAWA WATU...
kuna ndoa nyingi siku hizi ni keeping up appearances na hakuna ndoa kama ndoa....
Pia sitaki kuamini kuwa huyo mama "alifunga ndoa" kama tunavyoelewa kufunga ndoa.... maana kuna mengi yanayohitajika kabla hujafunga ndoa..in short umeiweka hii mada katika namna simple mno kiasi kwamba inakuwa na maswali mengi zaidi ya majibu na ndio maana kama wachangiaji tunatoa michango simple hivyo hivyo.Umesema huyo mdada ni mkristo.... kweli anaruhusiwa kuolewa kama mume amefariki..lakini usisahau kisheria kuna wiki tatu za kutangaza na mambo mengine...sasa hiyo ndoa ya mwezi mhhhh sijui....labda utufafanulie zaidi.
 

Vera mpendwa ndoa ya Kwanza ilifungwa kanisani RC hii ya pili Mdada alifunga ndoa kwa mkuu wa Wilaya bila Tatizo lolote na mpaka sasa ninapoongea yuko na mme wake huyu mpya
Ngoja niiache kama ilivyo kwangu ilinishangaza na baada ya kusikia majirani na pia ofisini kwa mdada wanajiuliza maswali bila majibu ndo maana na mie nikaimuvuzisha hapa
 

Wewe ulitaka akae muda gani? Kwahiyo angekaa miaka 2 basi usingemdhania kuwa ameuwa?
 


hii kitu ipo tegeta au boko jamani, mie napaita boko pale....niliendaga muda kidogo , bado pazuri kama awali?
 
ningebahatika kumuona huyo kijana aliyerithi ningemhonga anipe siri ya ufundi wake hata mama aue na kummilikisha mzigo jumla.ila wewe first lady ni mwanamke tena jirani yako fanya umafia akupe dodosa kiduchu alipagawa na nini au huenda yule wa kwanza alikuwa analala totorooo!angalia usiingie ndani zaidi usije nawe ukapractice,huyo chrispine humwezi mwache hukumbuki kisa chake cha waliogombea baa medi?Hahahahahaaaaaaa!
 
kwani hujui baamedi naye ni mwanamke na anahitaji huduma na moja ya marupurupu yake yanatoka kwa hao akina chrispine? msiwanyanyapae kwanza wanasaidia sana kutoa first aid kabla ya kwenda kupata huduma nyumbani,na shida kwa wanywaji ukifika nyumbani mara unyimwe huduma ati wamelala wamechoka,sasa usingejiwahi kule bar si utaanzisha valangati na mama?Mweeeh!
 
ni bora asingemuua ili naye aishi kuliko kumuua kwa ajili ya penzi la serengeti boy
 

una uhakika gani aliuwa?
 
sawa kabisa hatuhukumu ngoja tusubiri mungu ahukumu mwenyewe
lakini Boss 1 month ni muda mfupi sana kuamua jambo kubwa kama hilo

Firstlady1, Ninavyojua mimi (nakubali kurekebishwa) kwa kawaida huwa wanakaa eda siku 40. Sasa hesabu inaonyesha huyo dada ana less 10 days.

Lazima kuna mazingira yaliyopelekea mama achukue/aolewe mapema.

Mambo yamebadirika sana siku hizi, zamani wifi au shangazi alibaki na mfiwa kwa siku 40. Siku hizi watu hata matanga hawakai, tukizika tu palepale makaburini tunaambiwa shughuli ya msiba imekwisha. Kila mtu anaondokea makaburini kuelekea kwake. Mazingira haya yataleta mabadiriko mengi ktk jamii ya kileo.

Ni bora huyo aliyeonyesha wazi, wapo wengi wanafanya hivyo lakini haiwi issue kwa sababu wanajificha.
Mimi binafsi nampongeza dada kwa kuweka mambo hadharani kwamba hawezi ishi ndani bila kuwa na kichwa. Anahitaji ulinzi.
 

CMM,
YOU ROCK!
I like your bold spirit.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…