Wazee wa zamani walisema kua uyaone. Hiyo ni pamoja na tabia research nyingi zilizofanywa zinaonyesha kwamba akina mama kati ya miaka 40 -50 huwa hawataki kuishi tena na waume zao hasa kama wanaweza kujitegemea kimaisha. Vile vile usisahau kuna kuoana kwa kupendana kiukweli na kiuongo. Wengine huoa kwa sababu hawana namna na wengine huwa wanategemea vitu fulani fulani wakivikosa basi tafrani. Life is too short enjoy.
Kwenye bold....una point ndugu yangu.
Ndoa ni taasis ngumu na isiyotabirika.Mahusiano ya kwenye ndoa huenda yakibadilika kadiri miaka inavyozidi kwenda.Mwanzoni wana ndoa huweza kuanza kwa style yoyote - chini na pole pole kupanda kimaisha...hapo kuna wanaume wengine hujikuta wakibadilika kitabia kwa kulewa mafanikio... hapo wanawake hupata mateso makubwa sana lakini kwa vile mtu anataka kupigania ndoa na labda wanae basi hukomaa na kuvumilia tu.
Pia wapo wenye kuendelea kuleana na kufurahia maisha pamoja kadri maisha yanavyoendelea kuwa mazuri.
Kuna wanaoanza maisha katika hali iliyo bora kifedha - hapa inategemea pia.Mafanikio haya ya mwanzo huweza kujenga tension na migogoro isiyoisha kutegemeana na sababu zilizowafanya wanandoa hao kuoana.Kama ndoa ilianza kwa kufuata mali/vitu pasipo na mapenzi ya kweli basi wanandoa huweza kujikuta wakijutia ndoa zao na hivyo kuanza harakati nyingine za kuishi hata kama wapo pamoja kwa kujionyesha tu.
Tukirudi katika ishu aliyoleta MTM - NAWEZA kusema kuwa inategemea mafanikio hayo unayapima vipi maana cheti tu na huku hakijaleta chochote si waranti wa kuondokea.Tuangalie mafanikio na hali halisi ya ndoa ya mwanamke husika.Nitaomba kutoa maelezo yafuatayo:
1.Mwanamke mwenye amani hawezi kuchukulia mafanikio yake kama sababu ya kuvuruga amani na uhusiano katika ndoa.Mwanamke anayefanikiwa mara nyingine hujikuta akiingia katika matatizo mengine ndani ya ndoa yake kutokana na hali halisi ya fikra na mitizamo ya kijamii akiwemo mumewe.
2.Kuna wanaume hawajiamini kuwa na mwanamke wa namna hiyo na kila mara hujikuta wakitaka kuonyesha bado wao ni wanaume na kupelekea ukatili wa ajabu - maneno ya kejeli, vipigo wakati mwingine n.k na mifano ni mingi sana. -Hii hupelekea mwanamke kuona hakuna sababu kuishi maisha ya masimango ha hasa kama anataka kuendeleza career yake.
3.Kipindi cha maisha nacho kinachangia.Wanawake wengi hutaka security ya aina fulani. Ni wachache sana wa umri mdogo utawakuta wakiwa na mafanikio ya kutisha na ya kuwapa jeuri ya kujiondosha. Mpaka mtu apate kwa mfano PHD au awe kwenye hali nzuri ya kuridhisha kikaziau biashara atakuwa angalau amevuka miaka 30. wanawake katika umri huo na hasa 40-50 wengi hujikuta wameshapitia mengi katika ndoa zao.Wameonja nini kuwa kwenye ndoa - raha na karaha zake, wamelea watoto wao.Wenye kufanya kazi au biashara, ni umri ambao wameshakomaa na wako katika hali nzuri sana ( cheo, fedha, kujiamini).Umri huu pia couples wengi wanakuwa katika maisha wanayoyajua wenyewe - kama ni maamuzi basi mtu anakuwa anajipanga kwa muda mrefu na hadi afikie umri huu tayari anakuwa yuko tayari kwa matokeo yoyote.Hivyo si ajabu kuona mama wa umnri huu akiamua kuachana na ndoa isiyompa faraja/furaha na amani kwa kutumia style mbalimbali - wengi hawatapoteza muda kudai talaka ambazo ni gharama( muda na fedha), watatafuta njia ya kistaarabu kuondokea kama kutafuta kazi nje ya nchi/mkoa, kuhama nyumba n.k.Ukichunguza sana utakuta wanatoka katika ndoa zenye migogoro ya muda mrefu sana.Hakuna mwanamke wa umri huo atakayeamka siku moja tu na kuishia.
Haya ni maoni yangu kufuatana na niliyoyaona.