Mapenzi Na Mafanikio Ya Mwanamke

Mapenzi Na Mafanikio Ya Mwanamke

Kaka zangu mlio humu ndani kumsomesha mke ni jambo zuri sana, ila mimi kwa maisha ya sasa hivi siwezi hata kumshauri kaka yangu kufanya hivyo. Kwa sababu kuna kaka yangu alimsomesha mke wake akaacha kumsomesha mdogo wake, baada ya wifi kumaliza chuo, tulishangaa kaka akiacha kila kitu, gari na kila kitu na kuondoka personal things tu na ndoa ikaishia hapo. Ukimsomesha msomeshe kwa faida ya wanao kwa sababu ht mkiachana watoto wataendelea kupata msaada kwa mama yao.

No coment .
 
No coment .
Huo ndo ukweli, kwa wengi wao hakuna aliyejaribu kumsomesha mkewe akasalimika, kama sio kukimbiwa physically-basi hata psychologically, anabaki anateseka maishani kwa ku-tolerate vituko vya mpenzi wake wa dhati.
Ushauri, muanzishe level moja kwanza halafu -monitor tabia yake, Akiweza kuishi kama zamani-goodluck, unaweza kuendelea next level, lakini kwa ujumla hawatabiriki. Ila, hili suala linanikumbusha rafiki yangu yeye aliwahi kuoa kabla yangu, na akawa ananihamasisha nami nione, maana nilikuwa mbishi na siko tayari kwa ugomvi wa hizi nadharia -alisema " Hiyo ndio starehe ya ndoa"
 
mimi nahisi wanakuwa hawana mapenzi ya dhati kwa waume zao jamani!!! mwanamke ankuwa na ajenda zake za siri hapo anajua jamaa atanisapoti nipate elimu na nikigradueti tu nachapa mwendo!!!!!

otherwise naungana pia na aliyesema ni hulka y amtu binafsi....

MTM hongera hupo peke yako; Mke wangu ni ex starnd seven; amaeanza form one juzi baada ya kumaliza tution ya mwaka mzima ya kiingereza!

mimi nasoma Open university degree yangu ya kwanza!

Ananiombea nami nmwombea mafanikio ndio maan ya ndoa! Ni pamoja na kumwomba mungu amlinde!

Huko kugeukana ni kweli naungana na wacahngiaji hapa kuwa kutokuwapo mapenzi ya dhati; kutojitambua nafasi yako katika ndoa yenu na uchoyo amabazo ni hulka za binadamu; sio katika suala la elimu tu inaweza kuja kutokea katika hali yoyote nyingine si ajabu hata katika suala la afya zenu!

Mungu awape moyo na tuendelee kuwa support wake na waume wetu!😎😎
 
Kusomesha wake zetu ni wajibu
 
Mkuu uendelee na moyo huo wala usikate tamaa,

Nashauri kama mtu unania ya kumsaidia mke wako asome ufanye hivyo bila kuogopa kwamba atabadili after all ni mke wako note siongelei mpenzi/fiance etc..mke wako wa ndoa msomeshe mpaka mwisho wa juhudi yako

Mambo ya kubadilika si vitu muhimu, tuwe positive thinkers whem it comes to wenzetu, after tenda wema kila wema utaukuta mwisho wa safari yako

Ikitokea kageuka usikate tamaa tafuta mwingine Muumba atakupa raha tele kwakuwa umesaidia

Anayesaidia watu hajuti hata kidogo, nothing gives you happiness than giving, just try you will see
 
De Novo,

Kuna wanaume huwa wanawatesa, kuwaletea nyodo, kuwasimanga na kuwanyanyasa wake zao wakati wao (wanaume) ndo wanaoingiza kipato kikubwa ndani ya nyumba.

Hiyo hupelekea wanawake hao kuwa na hasira na kuandaa kisasi na wao wanaanza juhudi za kutafuta kwa bidii (juhuzi zaidi shuleni, kwenye biashara etc)

So, akishapata chake, kwa nini asikutose?

Chunguza vizuri kamanda, nyingine huwa ni 'sweet revenge'

Kama na wewe umekuwa uikimtesa wife wako na ghafla kaomba umpeleke shule, be warned!
 
Kaka zangu mlio humu ndani kumsomesha mke ni jambo zuri sana, ila mimi kwa maisha ya sasa hivi siwezi hata kumshauri kaka yangu kufanya hivyo. Kwa sababu kuna kaka yangu alimsomesha mke wake akaacha kumsomesha mdogo wake, baada ya wifi kumaliza chuo, tulishangaa kaka akiacha kila kitu, gari na kila kitu na kuondoka personal things tu na ndoa ikaishia hapo. Ukimsomesha msomeshe kwa faida ya wanao kwa sababu ht mkiachana watoto wataendelea kupata msaada kwa mama yao.

Sashay,

Maisha yao yalikuwaje kabla wifi yako hajaanza shule?

Kuna vita flani inawezekana ilikuwa inaendelea chumbani bila nyie kujua

We jiulize - WHY from nowhere mke wa kaka yako atafute shule?? alishaona hapo hakuna ndoa (probably kutokana na manyanyaso ya broda wenu...) na alikuwa anaanda mazingira ya kutokea tu.

Tutawalaumu wanawake tu hapa - tujitazamae na sisi
 
..kiukweli kuna baadhi ya wanawake ambao wakifanikiwa kielimu na kimaisha wakiwa ndani ya ndoa huanzisha kiburi na wakati mwingine hata kutishia kuondoka pindi ataona mambo si mambo. Kwa mujibu ya ufahamu wangu, wao hudai kuwa once akipata elimu nzuri e.g Master, PhD etc na mungu akamsaidia na kazi nzuri ikaja anaamini anakuwa amejikomboa sana katika suala kubwa la kipato ambacho wao hudai ndio jambo linalowatia wanawake wengi utumwani...

Aa! jamani hiyo ni tabia ambayo ipo kwa wale wanaoitwa kwa kiswahili cha asili "limbukeni" yaani wanavamia vitu tu bila ya kufikiria. Na hiyo inatokea kwa wanaume na wanawake ila kwa vile sasa wanawake wengi wamekuwa wanasoma ndio munaona ni issue.

Jee wanaume wangapi wamesoma na kuwacha wake zao kwa kuwaona washamba? Na wanaume wangapi baada ya kupata uongozi fulani wamekwenda kuoa mke wa pili au kutafuta nyumba ndogo kwa kumuona yule wa kwanza sio size yake?

MKUKI KWA NGURUWE, KWA BINAADAMU MCHUNGU - yaani mambo wafanye wanaume tu wakifanya wanawake imekuwa issue!
 
Kuna zaidi ya hayo maendeleo ya mwanamke yanayozungumziwa. Endapo mliooana mnapendana na mna mipango ya pamoja, hilo huwa si rahisi kutokea. Ila kama mmekuwa na mahusiano yanayosuasua japo mpo ndani ya ndoa, then tegemea lo lote iwepo shule au isiwepo. Kiwepo kipato au kisiwepo.
Ni kweli wanawake saa zingine wanabaki kwenye mahusiano kwa vile hawajiwezi kiuchumi, lakini je ni sahihi wanaume kuwanyanyasa wake zao kwa vile hawana vipato? Mbona mchango wa mke hauhesabiki wakati mwanaume anawekewa mazingira mazuri au ya kufanya kazi, biashara na pengine hata kwenda shule na kuiacha familia. Huo pia ni mchango na bado wapo wanawake walioachwa baada ya wanaume kumake it.
Ni vigumu kwa wanaume kuona hili kwani kwa muda mrefu mfumo dume umekuwa ukitawala.
Bravo kwa wanaume wanaosomesha wake zao. Nanyi wanawake mnaosomeshwa mjue hiyo ni investiment ya familia.
 
Akitoka shuleni ataanza kudai yuko busy, na kwa kuwa anaingiza kipato chake, basi ataringa nacho na kumleta msichana wa nyumbani mwenyewe. Huyu msichana atamwachia kufanya kazi hadi kukuandalia meza, kukunawisha, kukufulia hadi nguo za ndani, kufanya usafi chumbani hadi kutandika kitanda, kukuandalia maji ya kuoga n.k. Kuanzia hapo wewe utashawishika kumtomasatomasa binti, halafu mama atahisi. Je, nini kitatokea? Malizia ..............
 
Nakozi halafu twalaka
 
Nakozi halafu twalaka

YES. Sasa kuna umuhimu gani kumsomesha mkeo? Lakini nadhani haya yanawakuta wale wanasema siowi hadi niandae maisha yangu; yaani kujenga, kununua usafiri, kufungua biashara cha kuongeza kipato, kupata kazi nzuri n.k. Matokeo yake ni kwamba uko hatarini kumpata aliyependa vitu hivyo badala ya kukupenda wewe! Sasa, je twapaswa kuoa angali masikini? Je, wewe umpendea nini mwenzio? if any; Usidanganye.
 
wacha1 uneongea kitu cha msingi saana, kikubwa ni upendo na hata vitabu vya dini vimesisitiza upendo, kama mumeoana sababu kuna vitu fulanifulani unavitaka ndio matatizo yanakuwepo, lakini mkipendana kwa dhati vitu hivyo hakuna wewe huwezi kumuacha mumeo na kumuondolea watoto wote nyumbani kama kweli unampenda kwa dhati lazima jamaa alikuwa hana kitu alitaka mali tu kwa mwanamke naye mwanamke alitaka mwanaume wa mbegu tu na alipopata watoto hana ishu tena na jamaa ameamua kulea watoto na yeye kwenda zake kula shule

nakushauri kaka endelea tu kumsomesha mkeo maana ninaamini mnapendana kwa dhati na mafanikio yake ndio mafanikio yako na pia ya watoto wenu ila umuombe mungu pia ndio la msingi

mimi nina bachelor na mke wangu ana masters ila hakuna problem yeyote
 
De Novo,

Kuna wanaume huwa wanawatesa, kuwaletea nyodo, kuwasimanga na kuwanyanyasa wake zao wakati wao (wanaume) ndo wanaoingiza kipato kikubwa ndani ya nyumba.

Hiyo hupelekea wanawake hao kuwa na hasira na kuandaa kisasi na wao wanaanza juhudi za kutafuta kwa bidii (juhuzi zaidi shuleni, kwenye biashara etc)

So, akishapata chake, kwa nini asikutose?

Chunguza vizuri kamanda, nyingine huwa ni 'sweet revenge'

Kama na wewe umekuwa uikimtesa wife wako na ghafla kaomba umpeleke shule, be warned!

Yeah, thats where we make mistakes... we forget that women dont forgive and forget!!! we are just like fleas
 
I know of a couple ambao wameoana kitambo tu na mama anafanyakazi kwenye taasis nyeti tu na kwa mwezi anapata zaidi ya mara 5 ya mume wake ambaye ni wa kawaida tulakini anavyomuheshimu, kumthamini, na kumpenda inaondoa dhana nzima kuwa wanawake wa siku hizi wakifanikiwa huwa matatizo.
Huyu mama anachekwa na rafiki , ndugu na watu wengine lakini hajabadilisha msimamo wake. Kila wanachofanya hupanga pamoja na mume ndiye anayekabidhiwa jukumu la kusimamia.
Nadhani tatizo ni hulka, pressure za wanaokuzunguka,kutokuwa na mapenzi ya dhati na namna mlivyoanza .
 
Yeah, thats where we make mistakes... we forget that women dont forgive and forget!!! we are just like fleas

Mh... do we forget and forgive?? au ndio same same
 
I know of a couple ambao wameoana kitambo tu na mama anafanyakazi kwenye taasis nyeti tu na kwa mwezi anapata zaidi ya mara 5 ya mume wake ambaye ni wa kawaida tulakini anavyomuheshimu, kumthamini, na kumpenda inaondoa dhana nzima kuwa wanawake wa siku hizi wakifanikiwa huwa matatizo.
Huyu mama anachekwa na rafiki , ndugu na watu wengine lakini hajabadilisha msimamo wake. Kila wanachofanya hupanga pamoja na mume ndiye anayekabidhiwa jukumu la kusimamia.
Nadhani tatizo ni hulka, pressure za wanaokuzunguka,kutokuwa na mapenzi ya dhati na namna mlivyoanza .

Abarikiwe MAMA huyu; afaa kuigwa na kina mama wote wa kisasa🙂
 
Haya mambo huwa yanatokea kwa sababu mbalimbali
1: kawaida ya wanawake tunazoea kuwa wanaume kazi yao kututafutia hela ili sisi tutumie, ndo maana utakuta hata kama mwanamke ana kapato kizuri bado atahitaji kupata additional income toka kwa mume. sasa ikitokea kuwa mwanamke inabidi umtafutie jamaa atumie, inakuwa shida kidogo

2: Elimu haichangii sana katika kuvunja nyumba, ila pesa. mtakubaliana nami kwamba hata kama mwanamke ana elimu ya juu lakini mume akiwa na pesa nyingi zaidi yake (e.g. mfanya biashara) huwa haina shida sana, shida inatokea mke akiwa na hela zaidi ya mume.

3: wanaume pia huwa hawapo-secure wanapoona mke ana kipato/elimu zaidi yao. huwa hata kama mke amefanya kosa la kawaida tu ambalo mtu yeyote angeweza kulifanya, huwa wanafikiria amefanya hivyo sababu ya elimu/kipato chake, na ndo ugomvi unaanzia hapo.

wapo wanawake wachache sana wanaowavumilia waume zao wakiwa hawana kipato, lakini pia wapo wanaume wachache sana wanaokuwa secured wake zao wakiwa na elimu/kipato kikubwa
 
Back
Top Bottom