Mapenzi na mahusiano..tutakwisha - napendekeza

Mapenzi na mahusiano..tutakwisha - napendekeza

platozoom

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Posts
9,424
Reaction score
11,320
Nasoma mara nyingi kwenye hill jukwaa la MMU namna watu wanavyolizwa na mapenzi.Karibia kila siku kuna kuna misiba ya mapenzi:

'Ameniacha wakati nampenda'....
‘Kaniahidi kunioa lakini amenitosa’...............

‘Inaniuma sana' ……………N.K


Kwa kadri muda unavyokwenda ndivyo hali inavyozidi kuwa mbaya,majeruhi wa mapenzi wanaongezeka na hata pengine vifo.Ni kweli hapa MMU wanapata ushauri na wakati mwingine lawama,lakini hiyo bado haitoshi kutibu tatizo.


Napendekeza liundwe jukwaa dogo maalum kwa ajili ya majeruhi wa mapenzi na mahusiano (inaweza kuwa rehabilitation clinic),halafu huko watapata counseling na kuwa chini ya uangalizi wa wana-jukwaa (Kwa maana kwamba watawajibika kutoa feedback juu ya maendeleo yao kwenye mahusiano baada ya ushauri).


Hili muhimu: Wakati tunaendelea kulalamika juu ya matatizo ya uchumi,umasikini na maradhi unaweza kukuta hata mapenzi yana athari pia inayotutafuna taratiiibu bila kujua. Tutakwisha.


Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom