Mapenzi na ushabiki wa mpira kipi kinaumiza?

Vpn01

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2024
Posts
245
Reaction score
801
Nimekuwa katika mapenzi kwa miaka mingi ila ikafika hatua nikaamua kuachana nayo baada ya kujikuta naumia zaidi ya kufurahia.

Nikajikita kwenye utafutaji wa pesa tu lakini kutokana na hali ya upweke nikaona nijifunze kufuatilia mpira na taratibu ukaniingia akilini ila sasa nahisi kama nimejiingiza kwenye maumivu mapya maana kila timu yangu inapofungwa ama kutoa sare napata maumivu makali nadhani zaidi ya yale ya mapenzi

Je, kati ya mapenzi na mpira kipi kinaumiza zaidi ndugu zangu
 
Mpira mnafungwa leo, week ijayo mnaweza kushinda.

Ila uyo ujinga mwingine ikiisha imeisha. Atleast inachukua mwezi kurecover.
 
Mpira ni kifaa cha kufanyia mapenzi
 
Binafsi sijawahi ku experience maumivu makali yanayozidi yale ya kuliwa mkeka,

Kuna nyakati hadi nilipata kipanda uso wiki 6

Kubet kunauma jamani asikuhadithie mtu kama hujaingia huku usije kabisa
 
Maumivu yakujitakia lazima uumie Sana maana unakuwa umejitakia mwenyewe.

Unaweza kuumia kisa mpira? Au mapenzi? Ukiona unaumia ujue something is wrong
 
Binafsi sijawahi ku experience maumivu makali yanayozidi yale ya kuliwa mkeka,

Kuna nyakati hadi nilipata kipanda uso wiki 6

Kubet kunauma jamani asikuhadithie mtu kama hujaingia huku usije kabisa
Nakuelewa vizuri sana mkuu
 
Usifananishe mpira na mambo ya kijinga
 
Binafsi sijawahi ku experience maumivu makali yanayozidi yale ya kuliwa mkeka,

Kuna nyakati hadi nilipata kipanda uso wiki 6

Kubet kunauma jamani asikuhadithie mtu kama hujaingia huku usije kabisa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sasa kwenye maisha unalombaje? Unalomba mpira? Au umejiunga chama pendwa?

Hakuna kama mapenzi. Huu ujinga unauma kinyama. Yani kuna muda huelewi maumivu yanatoka wapi.

Pia yana faraja yakikolea.

Zamani nilikua napenda sana mpira mpaka ikiwa mechi day nasimamisha hata kazi. Kuna siku nikatafakari sana hivi wale si wapo kazini? Sasa kwa nini niumie au niharibu kazi yangu kuangalia mtu anafanya kazi yake? Na wale siku hizi hata wakifungwa hawaumii kama wachezaji wa zamani. Nikaachana na kuangalia mpira kimhemko. Siku hizi najiangalizia tu kawaida.
 
Mapenzi yanauma sana mara ya kwanza tu baadae hata uumizwe vipi inakuwa kawaida tu lakini hawa wajinga manchester united wakina onana ni kila weekend maumivu hayazoeleki

Nashauri kwa mwezi kuwe na mechi moja tu ya ligi hii kila wiki tutauana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…