Mapenzi na Utafutaji havikai pamoja!

Mapenzi na Utafutaji havikai pamoja!

Chibule

Senior Member
Joined
Sep 25, 2024
Posts
171
Reaction score
230
MKURUGENZI hapo Kitaa ambaye unapambana sana kuhakikisha huyo Mwanamke anakupenda, fikiria muda unaopoteza wenzako wanafanya nini kwa ajili ya kesho yao!

Amua sasa wakati unahangaika kumjazia texts na kumpigia wapo wanao wanakimbizana na michongo, hisia za mapenzi wamezizika na nyota ya ushindi ipo juu angani.

MSELA umeamua tu kumlilia Mwanamke ambaye sasa hivi yupo zake Lodge anaililia, Mwanangu umechagua kuzitupa hisia zako kwa Binadamu hawa wa sasa ambao wanajithamini wao kuliko wengine, hukusukia simulizi ya aliyemtolea Figo akaachwa? Umesahau Mwana alisomesha kisha Mwanamke akamsotesha?

MCHIZI nikwambie kitu? Pitia nyimbo za Diamond wakati mwanzo anaanza mziki, alikuwa analia sana kisa mapenzi lakini Mwanamke hapendi Mtu kisa huruma, aliamba Nataka Kulewa, aliimba Mawazo na sasa kajipata anasema bora niienjoy, yes maisha mafupi ni simple tu! DM ya Diamond huenda kwasasa anachagua nyama anayotaka yeye ndio life.

MWANACHUO, Mwanangu wewe nakuamini sana usipoteze kesho yako kisa sketi! Mwanamke ana ajira yake ya kudumu inaitwa Ndoa, ana tunda lake la kudumu lilofanya Adam afukuzwe heaven na leo akimpa Mtu anajihisi yupo Eden, wewe una nini kwa ajili ya Dunia Mwanangu? Weka njaa fanya kazi kwa bidii kesho haipo kwa ajili ya Mtu dhaifu.

MTALAAM, acha kulalama hajibu texts zako Mwanangu, acha kulalama hapokei simu zako Mwanangu! Kwani mioyo yao inapenda sehemu moja tu ila wengine wote mpo kwake kwasababu maalum, wewe upo kwa ajili ya Luku, yule yupo kwa ajili ya Dawasa, mwingine wa Vocha na mwingine wa Out halafu kuna mmoja atamchakarikia hata mic atashika.

MASELA sketi zimeuwa ndoto nyingi sana, Baba yetu Adam alimuasi Mungu pale Eden! Kama anaweza kukukaribisha kwenye kitanda anacholala na Mume wake atashindwa kukuuwa? Kama ana jeuri yake ya kuishi na Mwanaume umri sawa na Baba ako unategemea akupe heshima? Usisaliti ndoto zako ambazo ni kazi na sala.

WANANGU kesho sitaki kuona mnalia kisa Mapenzi, Wanangu kesho sitaki kusikia Mtu kajinyonga kisa Mapenzi, Wanangu kesho nataka kusikia mnazililia future zenu na mnafunga ndoa na Mafanikio, usiwekeze kwenye mapenzi, ni biashara kichaa ya hasara ndio maana TRA hawataki kodi.

DAKTARI.
20241022_151811.jpg
 
Umepiga kwnye mshono...

Wana Ajira yao ya kudumu inaitwa "NDOA"

hizi line ni wosia wa maana kabisa kila mwenye akili hakosi cha kubeba hapa..

Asante kwa SOMO.
 
Back
Top Bottom