Kuwatawala inakuja kutokana na mazingira mnayotengeza na wanaume.
Wewe umekuja kwenye maisha yangu umenikuta na mali zangu nimetafuta mwenyewe baada ya kuzinguliwa na akina Jack kwa maika nenda rudi hadi nikakata tamaa ya mapenzi ya kweli.
Kisha nimekutana na wewe nikakuweka ndani, halafu unataka nikuchukulie kama mtu kweli, wewe kwangu ni kitu, ni kama TV, Home theater, Gari na vinginevyo so utaishi kwa amri na maelekezo yangu vile nataka.... Sasa ubishane na maelekezo yangu kwa kuwa wewe ni nani?!
Mwanamke ambaye nitashauriana nae na nitaongea nae kama mwanadamu mwenzangu ni bi mkubwa wangu, dada yangu, na mwanamke ambaye alinikuta at my lowest akawa na mimi all the way up huyo kwangu ni malkia lazima apewe heshima yake, na akija mwanamke akamkosea adabu huyo ntamrarua, hata mama na dada zangu watapigwa biti matata wasimletee mizengwe huyo malkia