HorsePower
JF-Expert Member
- Aug 22, 2008
- 3,612
- 2,567
Mimi kwa kweli ni mara nyingi huwa nafurahishwa ila pia ni mara nyingi huwa nachukizwa. Nafikiri ndo maana halisi ya maisha ya mahusiano, uvumilivu na kusomana na kusameheana lazima kuchukue nafasi
Inasikitisha kwamba kuna watu wamekuwa wakianzisha uhusiano kwa raha, lakini inafikia wakati watu hao hao wanaanza kutiana shida, kutukanana, kupigana na kunyanyasana.
yani inakosesha maana halisi ya mapenzi! sasa huwa najaribu kufikiri hata kama mwenzio kakukosea kwani umtukane! kwanini kumpiga! kama kweli mlipendana mpaka kuamua kuishi wote bado mnaweza kusuluhisha mambo bila chaos na hali ikawa shwari..