Kuna uhusiano wowote kati ya mapenzi na elimu?
Hakuna uhusiano. Kitu mapenzi kinakuja naturaly. Unampenda mtu kutokana na tabia, sura, umbile. Labda elimu ni nyongeza tu, lakini haijengi penzi. Elimu SIO MSINGI WA PENZI.
Ni muhimu kwa wapenzi kuwa na elimu sawa?
Sio muhimu. Cha muhimu hapa ni maelewano, kuheshimiana, kuvumiliana na kusaidiana katika kutafuta ridhiki.
Inakuwa vipi kwa mwanaume anapomzidi mwanamke kielimu?
Ukimzidi mwenzako elimu, haibadili kitu katika upendo, haizidishi wala haipunguzi upendo halisi. Labda yawe mapenzi ya pochi.