bahati93
JF-Expert Member
- Aug 6, 2015
- 1,334
- 2,463
Miaka zaidi ya kumi Watanzania bado hawajategua kitendawili, Diamondi atashuka lini kwenye huu music wa Bongo Fleva. Wengi wamebakia kubashiri nini kipo nyuma ya mafanikio makubwa aliyopata, na anayoendelea kuyapata bwana Nasib.
Wapo wanaosema ni Freemason, ni mganga wa Morogoro, ni Majini. Haya majibu yote yana dosari ukweli ni kwamba Mapenzi ya dhati kutoka kwa mama yake Ndio chanzo kikuu cha mafanikio yake.
Unaweza kustaajabu jinsi mama Dangote alivyokuwa akimpa suport mtoto wake Nasibu Kwenye mambo ya muziki angali bado ni kijana mdogo, umri wa kuwa darasani. Kwa kweli Huyu Mama sijaona wa kumfikia hapa Bongo kwa ujazo wa mapenzi ya kweli aliyompatia mtotowe.
Nasema haya kwa sababu Wamama wengi wanachanganya mambo kati ya Mapenzi ya Kweli na Mapenzi ya Uwongo. Mapenzi ya Uwongo ni kuwapa watoto wao vitu ambavyo wanaviona ni vizuri bila hata ya kumuliza mtoto anataka nini. Wamama wengine wanajiona ni Mungu wa pili hawataki kabisa majadiliano na mtoto, mtoto akisema kidogo tu wanatishia kutoa Radhi.
Hata hivyo sio kila mwanamke anaweza kuwa mlezi mzuri kwa watoto wake. Kipaji cha ulezi ni zawadi kutoka kwa mola enyi wanawake muombe sana dua awajalie hekima. Pia kuna wamama na mabinti wamepitia mazingira mabaya katika ulezi wao hivyo kutokujua aina tofauti na bora zaidi ya vile walivyolelewa, tazameni jinsi mama Nasibu alivyomlea mwanae.
Diamondi na Mama yake wana mahusiano yenye afya sana kwa sababu mahusiano yao yameyajenga juu ya Heshima na Mipaka. Mama dangote anamuheshimu Nasib kwa kusikiliza alichotaka na ameweka mipaka kutokumlazimisha mambo anayotaka yeye. Diamond anamuheshimu mama yake kwa kumpa vyote anavyotaka na ana mipaka kwa kutokuingilia kwenye mahusiano ya mama yake.
Mwenye utajiri wa moyo.