Yes, Mapenzi ya dhati does exist, lakini wengi wetu hatujui hilo kwani tumeweka vigezo vingine. Kikubwa ni kuwa lazima tuzikubali zile tofauti za kawaida baina yetu. Kwani hatutegemei kumpata mtu ambaye ni malaika au yuko 100% perfect. Kama wote wawili tutajua hili basi ni rahisi kila mmoja wetu kuonyesha mapungufu yake kwani anajua ipo nia ya kweli katika kukubaliana au kuoanisha hayo mapungufu katika maisha. Kama wote mtajifungua, basi hapo hakutokuwa na artificial life..itakuwa ni real life iwe mbaya, ya kawaida au nzuri..

Kwa sababu hawajijui au wanataka kufanya mazoezi na mapenzi au maisha kutokana na jinsi wanavyoona kwenye TV, magazeti au Movie. Mimi binafsi naamini ..Formula ya Maisha au mapenzi unatengeneza wewe mwenyewe..ila kwa bahati mbaya haina majaribio..Unatakiwa uamini kile unachofanya ni sahihi kama unavyotaka wewe na siyo Movie, TV au gazeti la uwazi.

Ukisoma hapo juu utaona mapenzi ya dhati hayaji kama mvua, unayatengeneza, tena sio peke yako bali vyote wawili.. mtoke kwenye artificial life na nyote muwe real bila kuogopa. Kama hutampata au kumkubali mtu ambaye ni yeye kama alivyo..basi hutompata 100% perfect partner hadi kiama..kwani wote watakuwa wana pretend life kwa manufaa fulani..

Much Appreciation mkubwa! Umetulia, umechambua mambo vizuri tena kwa lugha nyepesi, fasaha yenye kueleweka kirahis kwa wote!
Nakubaliana nawe ktk mengi
1. Mapenzi ya dhati ni nadra kuyapata tena huwa ni kwa wachache sana.
2. Baadhi yetu (wengi) tuliopo ktk mapenzi hatujitambui then tuna expectation nyingi sana juu ya mapenz na wapenz wetu.
3. Maana ya penzi la dhati bado ni utata kwa wengi wetu. Wengi wanadhan udhati wa mapenzi ni kuigiza yale ya kwenye tamthilia za kigeni za mapenzi eg. Daniella, Second chance, The promise etc, tunachanganya udhati wa mapenzi na artificial life style ya wageni toka ulaya.
4. Uvumilivu,kukosoana na kuelekezana kati ya wapenzi bado n tatizo kubwa, mahusiano mengi huvunjika kwa kutokuelewana, kutokusilikizanana kudharauliana. Inabidi tukomeshe hii hali.
5. Umri na rika la watu waingiao ktk mahusiano ni tatizo kwa wengi, coz mapenz yamevamiwa na watoto wadogo wenye umri mdogo, hawa hawajapevuka kisawasawa, wengi wao huishia kutendwa na kuumizwa hvyo kupoteza udhati wa mapenz ya kweli.
Nb. Yapo mambo mengi, hayo ni baadhi.