Mapenzi ya facebook!

Bollo Yang

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2009
Posts
440
Reaction score
51
Mara nyingi baadhi ya wanaume wa kitanzania (mimi mmojawapo) tunaamini kuwa mwanamke utayeanzisha mahusiano nae kupitia facebook ama mtandaoni kwa ujumla ni kicheche!!! Ingawa yeye (Mwanamke) anaweza kuwa very serious kwenye hiyo relationship...
Mnabishaaaaaaaa??
 
Duh...maswli mengine bana......
 
Hayo ndo mawazo ya wanaume wengi ila mimi nina mtazamo tofauti kidogo.
Naamini sio wote na nina mfano hai wa rafiki yangu aliyepata mke kupitia mtandao na ni mke mwenye heshima na mcha Mungu.
 
Inategemea wewe unatafsiri vipi.
Kuna namna na sehemu mbalimbali za watu kukutana.Facebook na mitandao mingine ni njia mojawapo.Wewe unayetongoza huyu mwanamke basi ndio kicheche zaidi kama tafsiri ya kicheche kwako ndio hiyo!
 
Mara nyingi baadhi ya wanaume wa kitanzania (mimi mmojawapo) tunaamini kuwa mwanamke utayeanzisha mahusiano nae kupitia facebook ama mtandaoni kwa ujumla ni kicheche!!! Ingawa yeye (Mwanamke) anaweza kuwa very serious kwenye hiyo relationship...
mimi sikubishii kwakuwa huo ndio upeo wako wa kufikiri na ni mtazamo wako!
 
Nikuulize swali wewe mpenzi wako umemtoa wapi??? Tusijekubishana hapa
 
Nikuulize swali wewe mpenzi wako umemtoa wapi??? Tusijekubishana hapa

HAJUI KUWA SASA NI DUNIA YA ICT LOL...
Anadhani bado watu wanakutana kisimani, kwenye kukata majani, kwenye ngoma, kwenye mchiriku.....endeleza
Labda tumsaidie ku frame vizuri ishu:
Wana JF, MKITAKA KUPATA MWANAMKE/MWANAUME AMBAYE ANAFAA , NI WAPI MAHALI PAZURI?........
 

Nilihisi tu watakaojibu saaana ni wasichana!!! hahahaha..lol
 
kwa ku rephrase suala lako ungeuliza hivi " jee social networks mtandaoni kama facebook ni sehemu nzuri ya kutafutia wake?"
lakini sio unakuja hapa unataka "tubishane" na upeo wako wa kufikiri.

wako tele walopata wake facebook na wametulia nao kuliko hata wale waliowaona kwenye nyumba za ibada.
 

Very good idea, naomba sasa thread yangu isomeke hivo unavotaka wewe..nakubali upeo wangu ni mdogo.
 
WOS nakubaliana na wewe 100% hii dunia ni ya ICT....

nimeshaona mahusiano mengi yaliyotokana na mtandao na yakazaa ndoa tena ndoa za heshima wala hakuna tatizo.

ulimwengu huu watu hatuna hata muda wa kwenda kushiriki michiriku na midundiko basi tutakuwa hatupati wenza...........

hiyo issue umei-frame vizuri thanks
 
Hivi kuna njemba zinatafutaga mademu kwenye facebook?? lolz.
 
Ujanja wa kugombana na keyboard wengi wamefuzu.. Self taught experts 😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…