ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,030
- 61,298
Mapenzi ya siku hizi yanafurahisha kama hujawahi kuwa muhanga wa michezo. Uko zako Insta au Facebook ama TikTok unavinjari zako tu, ghafla unaona demu ka like comment au post yako na kaku follow kabisa.
Unasema, Ngoja nitest zali nijioenee nisikae kinyonge unakaaje mwezi mzima hutongozi na wewe sio anko T Basi unatuma DM/inbox huku ukiwa tayari kisaikolojia huna uhakika atajibu au VP. Cha kushangaza anajibu.
Basi story zinaanza, Leo Instagram, kesho WhatsApp. Kesho kutwa video call. Ndani ya siku tatu mnazoeana kama watu waliofahamiana tangu enzi za JK.
Tatizo linaanzia hapo.
Mwanaume anajisahau kabisa. Kila siku mnaongea masaa manne, matano, sita. Unajikuta umeshamueleza mshahara wako, michongo yako ya maisha, madeni yako,ma pillow talk unaweza ukaanza hata kuwasema washikaji zako.
Na yeye atakupa siri zake kidogo kidogo.Atakutumia picha za mama yake mama mkwe wako ili ujisikie salama ufunguke zaidi. Wewe unaona kama mnaaminiana, kumbe michezo inaendelea. Baada ya wiki unaanza kuona yes huyu ndo wife material aliyetoka kwa bwana. Video call sana mixture view once.
Hapo ndipo akili inatakiwa ichaji Kwa sababu ukishafika hatua ya kuitwa baby,future husband na majina mengine matamu, ujue kuna siku inakuja.
Siku yenyewe ndiyo ile ya;
Baby nina shida kidogo...Na shida yenyewe haiwi ya buku ya vocha.
Baby simu yangu imeharibika...
Baby kodi imefika...
Wiki inayofuata Baby mama anaumwa.
Ukifika hapo tayari uko deep. Huwezi kurudi nyuma kirahisi maana kila ukitaka kukataa unajiona mkatili.
Lakini cha kuchekesha zaidi ni haya mahusiano ya mbali. Mdada yuko Mwanza wewe uko Pwani. Hamjawahi kukutana hata mara moja. Lakini tayari mnapeana ahadi za milele.Anakwambia yuko single kabisa.Na wewe unaamini asilimia mia moja.
Sijui ni nini kinatokea kwenye akili za wanaume wanapoingia kwenye penzi jipya. Mtu ambaye kwa kawaida anahoji kila kitu duniani, ghafla anakuwa mwepesi kuamini kuliko mtoto wa darasa la pili.
Anakwambia Siku nzima nilikuwa nyumbani unaamini yaani mapenzi yana uwezo wa kuzima mfumo mzima wa uchambuzi ambao mtu ameutumia maisha yake yote. Mwanzoni nilikuwa nafikiri mambo haya ni ya watoto wa shule tu. Kumbe hata watu wazima wenye biashara zao na elimu na uzoefu wa maisha wakishaingia kwenye penzi jipya wanajizima data wenyewe