Inawezekana tena sana tu. Kwani kukutana na mwenza wako ni sehemu yoyote, kwenye arusi, misiba, birthday, sendof, mikutanoni, workshop, kisimani, kukata kuni,kanisani , sokoni na mpaka MJENGONI DODOMA. Sasa usishangae kuona copuples wa kwenye internet ni sawa kabisa, tena kwa kutumia uandishi au USANII WA VIDOLE UTAMSOMA MWENZIO IQ yake vizuri saana. mie ninamifano hai ya watu ambao wamekutana kwa kuchat tena enzi hizo hotmail au yahoo na wanaishi poa kabisa na familia zao. Ila uangalifu ni kitu cha kwanza. Kama ni mzuri kuweka maswali yako kimaandishi na mchambuzi wa mambo, ukisoma maandiko ya mwenzako word by word utamtambua yupi mkweli na yupi anazuga tu. Lazima uwe critical sana ndio utafanikiwa. Ukitaka mbinu nitafute takusaidia.