Mapenzi ya kufungwa mnyoror yananitatiza, msaada jamani.

Ngekewa

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2008
Posts
7,705
Reaction score
1,288
Wanajamii unapotaka kumlisha mbwa mkali usiemzoea si unaweka chakula pale unapohisi mnyororo unamzuia yule mbwa? Halafu unasogeza chakula kwa jiti. Nahisi na mimi napewa mapenzi namna hiyo.

Mimi niko kwenye kituo fulani cha kazi mkoa mmoja ulio mbali na Dar. Aliwasili kituoni hapo msichana mmoja mrembo ili kufanya mafunzo ya vitendo. Mimi si m chi nvi lakini msichana alinitowa roho yangu na moja kwa moja nikaanza kujenga maelewano nae na sikuchukuwa muda nikajieleza. Lilikuwa kosa kwani msichana alinigeuka hadi akaomba uhamisho na akapewa. Alipelekwa upande mwengine wa nchi mkoa fulani lakini alipofika huko alianza kuwasiliana nami na panapo shida ninazoweza kumsaidia nilifanya hivyo si mnajuwa mitandao imerahisisha kila kitu siku hizi.

Mapenzi ya ndani ya cm yakanoga na kuendelea siku hadi siku. Kwa upande wangu nilikwisha kata tamaa na hivyo nilitafuta mpenzi na yule msichana ameshasikia hilo na amenialumu sana na anajaribu kunifanya nimfuate huko mbali aliko.Meseji za mapenzi na simu za nyakati za usiku hazishi eti anasema yeye ndie mwenye haki na mie kuliko huyu nilienae sasa.

Nabaki kujiuliza nini kilimkimbiza na nini anataka sasa nashindwa kupata jibu. Naomba jawabu au ushauri ili nilitatue tatizo hili
 
alright...pole sana my advise is achana nae maana kwanza long distance relationship full usanii
 
Wewe kumuomba penzi ndio aombe uhamisho? Yawezekana ulikuwa boss wake ukawa unamghasi
 
hivi si ni wewe ulileta mada unataka kuoa mke wa pili?wewe endeleza uko chink kama hawajakuzika wenzio...
 
Wanajamii unapotaka kumlisha mbwa mkali usiemzoea si unaweka chakula pale unapohisi mnyororo unamzuia yule mbwa? Halafu unasogeza chakula kwa jiti.
Nahisi na mimi napewa mapenzi namna hiyo.
Mimi niko kwenye kituo fulani cha kazi mkoa mmoja ulio mbali na Dar. Aliwasili kituoni hapo msichana mmoja mrembo ili kufanya mafunzo ya vitendo. Mimi si m chi nvi lakini msichana alinitowa roho yangu na moja kwa moja nikaanza kujenga maelewano nae na sikuchukuwa muda nikajieleza. Lilikuwa kosa kwani msichana alinigeuka hadi akaomba uhamisho na akapewa. Alipelekwa upande mwengine wa nchi mkoa fulani lakini alipofika huko alianza kuwasiliana nami na panapo shida ninazoweza kumsaidia nilifanya hivyo si mnajuwa mitandao imerahisisha kila kitu siku hizi.
Mapenzi ya ndani ya cm yakanoga na kuendelea siku hadi siku. Kwa upande wangu nilikwisha kata tamaa na hivyo nilitafuta mpenzi na yule msichana ameshasikia hilo na amenialumu sana na anajaribu kunifanya nimfuate huko mbali aliko.Meseji za mapenzi na simu za nyakati za usiku hazishi eti anasema yeye ndie mwenye haki na mie kuliko huyu nilienae sasa.
Nabaki kujiuliza nini kilimkimbiza na nini anataka sasa nashindwa kupata jibu. Naomba jawabu au ushauri ili nilitatue tatizo hili
kata hayo mawasiliano na uwe unamjibu kwa meseji fupi kama ni mhimu kumjibu,mkiwa pamoja hakutambua feelings zako za nini sasa akusumbue wakati una wako,achana naye
 
Ushauri mzuri lakini siuji kama nishakata tamaa? Akirudi jee?
 
Naamini una msimamo wewe kama mwanaume wa kuamua uwe na nani mwenye mapenzi kwako na wewe unaempenda. Chagua mmoja wa kuwa nae, acha kutangatanga.
 
Asikushughulishe naende uko, si alisha kutapika sasa imekuwaje tena?
 
....Alikuwa mafunzo kwa vitendo, halafu akaomba uhamisho.....??????
 
Wanajamii unapotaka kumlisha mbwa mkali usiemzoea si unaweka chakula pale unapohisi mnyororo unamzuia yule mbwa? Halafu unasogeza chakula kwa jiti.
Nahisi na mimi napewa mapenzi namna hiyo.
Mimi niko kwenye kituo fulani cha kazi mkoa mmoja ulio mbali na Dar. Aliwasili kituoni hapo msichana mmoja mrembo ili kufanya mafunzo ya vitendo. Mimi si m chi nvi lakini msichana alinitowa roho yangu na moja kwa moja nikaanza kujenga maelewano nae na sikuchukuwa muda nikajieleza. Lilikuwa kosa kwani msichana alinigeuka hadi akaomba uhamisho na akapewa. Alipelekwa upande mwengine wa nchi mkoa fulani lakini alipofika huko alianza kuwasiliana nami na panapo shida ninazoweza kumsaidia nilifanya hivyo si mnajuwa mitandao imerahisisha kila kitu siku hizi.
Mapenzi ya ndani ya cm yakanoga na kuendelea siku hadi siku.
Kwa upande wangu nilikwisha kata tamaa na hivyo nilitafuta mpenzi na yule msichana ameshasikia hilo na amenialumu sana na anajaribu kunifanya nimfuate huko mbali aliko.Meseji za mapenzi na simu za nyakati za usiku hazishi eti anasema yeye ndie mwenye haki na mie kuliko huyu nilienae sasa.
Nabaki kujiuliza nini kilimkimbiza na nini anataka sasa nashindwa kupata jibu. Naomba jawabu au ushauri ili nilitatue tatizo hili

Binafsi sioni tatizo ikiwa unampenda yeye zaidi ya huyu aliyenaye hapo karibu. Kukukataa mwanzoni haimaanishi kama alikuwa hakupendi. Nahisi alikuwa na mtu wake ila amegundua hakuna future akaamua kugeukia kwako. Kuwa na mtu zaidi ya mmoja ktk harakati za kutafuta mwenzi wako wa maisha ni kitu cha kawaida kwa wote (mwanaume au mwanamke). So endelea naye tu mkuu as long as unampenda kumoyo.

Shida ya mwanaume akishajua hivyo, atataka amgonge halafu amwache kwenye mataa! it's very wrong!
 
kwani sasa hivi huna mpenzi?na huyo uliye naye unampotezea mda wake au?

Hivyo unafikiri kama nilimpenda ndio mapenzi yamefutika? La bado nampenda ila uhusiano gani niwe nae ndio ninaotaka msaada.
 
Binafsi sioni tatizo ikiwa unampenda yeye zaidi ya huyu aliyenaye hapo karibu. Kukukataa mwanzoni haimaanishi kama alikuwa hakupendi. Nahisi alikuwa na mtu wake ila amegundua hakuna future akaamua kugeukia kwako. Kuwa na mtu zaidi ya mmoja ktk harakati za kutafuta mwenzi wako wa maisha ni kitu cha kawaida kwa wote (mwanaume au mwanamke). So endelea naye tu mkuu as long as unampenda kumoyo.

Shida ya mwanaume akishajua hivyo, atataka amgonge halafu amwache kwenye mataa! it's very wrong!

mito, nakukubalia ushauri wako lakini kuna hatuwa nyengine hapo mbele, yaani ndowa, sasa hilo ndio nataka niwe makini kati ya wawili hawa.
 
Wanajamii unapotaka kumlisha mbwa mkali usiemzoea si unaweka chakula pale unapohisi mnyororo unamzuia yule mbwa? Halafu unasogeza chakula kwa jiti. Nahisi na mimi napewa mapenzi namna hiyo.

:biggrin1: nimependa huu msemo
 
Back
Top Bottom