Wanajamii unapotaka kumlisha mbwa mkali usiemzoea si unaweka chakula pale unapohisi mnyororo unamzuia yule mbwa? Halafu unasogeza chakula kwa jiti. Nahisi na mimi napewa mapenzi namna hiyo.
Mimi niko kwenye kituo fulani cha kazi mkoa mmoja ulio mbali na Dar. Aliwasili kituoni hapo msichana mmoja mrembo ili kufanya mafunzo ya vitendo. Mimi si m chi nvi lakini msichana alinitowa roho yangu na moja kwa moja nikaanza kujenga maelewano nae na sikuchukuwa muda nikajieleza. Lilikuwa kosa kwani msichana alinigeuka hadi akaomba uhamisho na akapewa. Alipelekwa upande mwengine wa nchi mkoa fulani lakini alipofika huko alianza kuwasiliana nami na panapo shida ninazoweza kumsaidia nilifanya hivyo si mnajuwa mitandao imerahisisha kila kitu siku hizi.
Mapenzi ya ndani ya cm yakanoga na kuendelea siku hadi siku. Kwa upande wangu nilikwisha kata tamaa na hivyo nilitafuta mpenzi na yule msichana ameshasikia hilo na amenialumu sana na anajaribu kunifanya nimfuate huko mbali aliko.Meseji za mapenzi na simu za nyakati za usiku hazishi eti anasema yeye ndie mwenye haki na mie kuliko huyu nilienae sasa.
Nabaki kujiuliza nini kilimkimbiza na nini anataka sasa nashindwa kupata jibu. Naomba jawabu au ushauri ili nilitatue tatizo hili