Mapenzi ya kweli bado yapo?

Rajabmbisha

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2024
Posts
316
Reaction score
530
Wadau, swali la iwapo mapenzi ya kweli bado yapo limekuwa likizungumziwa sana. Ni suala la muda tu kumpata mtu anayekufaa. Kwa mfano, kuna binti mmoja ambaye amenionyesha upendo wa dhati kiasi cha kunifanya nianze kuamini tena mapenzi ya kweli.

Awali, sikumzingatia sana, lakini kadri muda ulivyopita, nimeanza kumuelewa na kuhisi upendo wake. Niliwahi kuandika kuhusu yeye hapa jukwaani, na kiukweli nilikuwa mpita njia tu mwanzoni. Hata hivyo, jinsi anavyojitahidi kunionesha upendo, imenifanya kufikiria hatua kubwa zaidi, na hivi karibuni natarajia kupeleka posa.

Najua kuna wasiwasi kuwa huenda akabadilika, hasa kwa sababu kuelewa wanawake si rahisi, lakini kwa sasa kile anachoonesha kwangu kinaonekana kama upendo wa kweli. Mimi si tajiri, hivyo si suala la pesa.

Tuendelee kuamini kuwa mapenzi ya kweli bado yapo. Muwe na siku njema!
 
Tuone picha yake
 
Watu wanavyoyasimulia mapenzi utayaona mazurii, ingia sasa wewe ukaonyeshwe acrobatic ama ukurumbembe!!..

by the way hongera kwa kupata mpenzi wa kweli.
 
Wewe lazima umepewa stail mpya.

Haya hongera mkuu ikawe heri kwenu.
 
Mapenzi ya kweli Yapo mkuu
wewe oa
 
Watu wanavyoyasimulia mapenzi utayaona mazurii, ingia sasa wewe ukaonyeshwe acrobatic ama ukurumbembe!!..

by the way hongera kwa kupata mpenzi wa kweli.
Maisha yetu kwa ujumla yanakabiliwa changamoto, hivo ukitazama changamoto pekee hutouona uzuri wa kitu chochote.
 
Niseme kuwa, wewe una bahati sana kupendwa na anayekuvutia.

Mimi imenitokea mara nyingi kupendwa, lakini wanaonipenda wote nakuwa sivutiwi nao!

Nadhani hii ni karama, kupendwa na unayempenda, ni nadra sana jambo hilo kutokea.

Nakupongeza kwa hatua ya heshima unayotaka kuichukua.
 
mapenzi ya kweli yapo, na pia hayapo,,,pata mpenzi ukiwa na pesa halafu baada ya miaka kadhaa upepo uende vibaya na uishiwe, na wakati huo mkeo au/mumeo ndio awe na pata kubwa.... Hapo ndio utagundua kuwa mwenza wako ana mapenzi ya kweli au ni tapeli
 
Nina miaka 47 kwasasa mapenzi ya kweli hayapo kabisa...labda mtoa mada anayapigania yaludi kama zamani lakini haitowezekana kwani Dunia nayo inaenda kasi sana..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…