Iyo mapenzi ya masafa marefu ni adhabu tu, yanaweza kudumu kwa muda mfupi, sio zaidi ya mwaka baada ya hapo tena kwa kweli yanafifia na vishawishi vya kudanganya vinachukua nafasi, hata hivyo kuna mambo mawili matatu yanayoweza angalau kuyapa uhai hayo mapenzi:
1. Keep yourself busy itapunguza distraction.
2. Mawasiliano muhimu, mpatie mpenzio Bongo laptop na broadband connection ili muwe mna video link kila siku kwa Skype nk, ni nafuu kuliko kutumia cheap calling cards na munapoonana uso kwa uso mtandaoni inasaidia sababu asiekuwepo usoni na machoni hayupo.
3. Jaribu ku-socialize kusukuma siku na kupunguza stress ila chunga sana na social scenes za kibongo, zitakuchochea kumtosa mwenzio kule bongo.