Mapenzi ya siku hizi uzushi mtupu!!

Bra-joe

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,628
Reaction score
1,124
Ukitaka kuumiza moyo wako jifanye unajua kupenda, siku hizi ukiwa maarufu au mambo safi kidogo tu kila mtu atajifanya anakutaka kimapenzi, hata kama huvutii. Wengine huenda mbali hata wakafunga ndoa, matokeo yake wanaishi kichinachina ndani ya nyumba. Ndio maana mimi nimeamua SODA YA KOPO nakunywa nikimaliza natupa. Haina stress wala kusukumwa.
 
hah! Unaongea kiyemen?

Ukitendwa ndo inakuwa hivyo, ukipona utapenda tena tu.

Pole!
 
Hamna hamna hamna kabisa mapenzi na hii ni kukosa mafundisho ya mahusiano na hasa maisha ya ndoa, bora kuwa nguvu ya soda tu.
 
msemo mpya kwangu SODA YA KOPO' Nilijua ni soda hii ya kawaida kumbe ina mambo ndani yake haya bwana
 
Mapenzi yako safi sana siku hizi maana hata ukitaka kuoa hauchukui muda mrefu kama zamani, miaka mitatu, mitano, ila siku hizi tatizo ni roho za watu zimekuwa mbaya zimejaa uasi.
 
Kazi kweli me hapa wa kwangu ananiambia kwani mwanaume kitu gani! Na huku yy ni home wf nahangaika usiku mchana kutafuta lakin dharau nnayoipata ni mateke ya punda. Si unaweza kumsukumia ukutani kweli?
 
Kazi kweli me hapa wa kwangu ananiambia kwani mwanaume kitu gani! Na huku yy ni home wf nahangaika usiku mchana kutafuta lakin dharau nnayoipata ni mateke ya punda. Si unaweza kumsukumia ukutani kweli?

hapana usimpige hata kidogo, kumpiga mpenzi wako ni mambo ya kizamani sana, vumilia, akikushinda move on, umwache akiwa hana kovu lolote kama ulivyomkuta mwanzo.
 
ha ha eti mapenz ya siku hizi? Na we si wa siku hizi kwani zamani ulikuwepo?.
 
This material world!!!!!!!!!!!!???????????????:smash:
Kama huna ki2 huna m2.

Usikate tamaa, wachache bado wapo ambao wanataka maisha na sio kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…