Mapenzi ya ushirikina yana gharama kubwa

Mapenzi ya ushirikina yana gharama kubwa

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Ni huyu jirani yangu mama Sikujua hapa Kwamtogole. Alikwenda kwa mganga ili kumuweka sawa baba Sikujua asifurukute. Maganga alimpa mama Sikujua dawa ya kuweka kwenye maji ya kuoga.

Siku ya tukio mama sikujua aliamka alfajiri na kupasha maji moto. Aliyapeleka bafuni akitangulia na sabuni ya Imperial Leather, baba Sikujua akijiona mwenye bahati kati ya wachache waliooa wanawake waliofundwa. Alijivika taulo na kwenda bafuni.

Baada ya kuoga alisikia baridi na mwili ulianza kutetemeka. Ilibidi siku ile apige simu kazini kuomba ushuru kwani afya yake haikua sawa. Wakati huo mama Sikujua akijisemea yes mambo yanaiva.

Baada ya siku tatu za homa ya ghafla, uume wa baba Sikujua haukuwika tena. Subiri na subiri mwisho mama Sikujua alirudi kwa mganga wake. Kufika kule majirani I alimwambia mganga amesafiri. Hakuwahi kuonana tena na mganga.


Mama Sikujua uvumilivu ulimshinda kukaa na mume wanaangaliana tu. Alimuacha Baba Sikujua na watoto tena mkubwa akiwa na miaka saba.
 
Mke alikimbia tatizo alilolisababisha yeye mwenyewe!. Sijui akija sikia kuwa mumewe kashapona atarudi?

Wanawake wanatakiwa kujua kuwa Ndoa ni zaidi ya migegedo. Mwenye sifa za kuitwa Mke ni yule anayeweza kuvumilia matatizo.
 
wanawake wanatangatanga sana kwa hawa mawakala wa shetani
 
Back
Top Bottom