Mapenzi yalivyonibadilisha na kuwa mkatili na roho ya ajabu

Dooh pole ila uliwahi sana form 1 miaka 12 or 13 au 14, you was a kid.
 
sema wewe katili kiasili, hakuna kisa cha kukufanya uwe katili hapo, ila ulianza umalaya mdogo sanaaaaaa,
kwa namna ulivyo malaya unapaswa kuwa fair kwa wanawake maana na wewe malaya na mungu anakupa malaya wenzako
 
MAHUSIANO YA TATU

Baada ya kuachana na KAUTHARI nilipitia mahusiano kadhaa ila sikua siriazi sana na hayo mahusiano hadi pale nikaja kukutana na binti anaitwa RUKIA huyu namtaja kwa jina halisi kwasababu mpaka sasa ndo mtu pekee alikuja kuniomba radhi na tuko sawa hadi sasa japo ana maisha yake na mimi nina endelea na mitikasi yangu.

Rukia huyi ni bint wa kiislama mzaliwa wa rufiji ,akiwa hana elimi zaidi ya darasa la 7 nilikutana nae alipokua anafanya kazi ya ushonaji siku ambayo nilipeleka nguo zangu kwa ajili ya kushona. Huyu ni moja ya mabint wa kibantu ambaye mng'avu ,mrefu ,mpole shepu ya wastani ila sura nzuri balaa pi akiwa mtu wa dini sana. Siku ya kwanza tu kumuona alinivutia hasa kwa namna alivyonipokea na kunihudumia hapo nilikua kidato cha Nne.

Baada ya kuona kuna bint pale spidi ya kwenda kwa yule fundi ikawa kubwa sana ,haipiti siku 3 sijaenda muda mwingine hata kama sina nguo naenda. Mazoe yakaanza mdogo mdogo ndipo nikajua alikua pale kujifunza tu ushonaji na alikua anaishi mtaa wa pili kutoka pale. Kutokana na huyu bint kua mtu wa dini ilikua ngumu sana kumtongoza ghafla hivyo kwanza nikatengeneza mazoea mpaka nilipopewa mbinu na mwanangu Jose. Sikia Feyzal wewe tafuta hela kisha twende tukanunue chupi tuweke kwenye bahasha halafu mpelekee mtoto lazima aelewe.

Basi bwana nikafanya kama nilivyoshauriwa,kesho yake nikaenda kununua chupi 5 zenye rangi tofauti nikaandika na barua kisha nikaweka na Choklate vyote kwa pamoja nikaweka kwenye bahasha moja. Ishu ikawa namna ya kumpa siwezi kumpa pale kazini kwake ikabidi nivizie mpaka muda atakaokua anaondoka maana siku na namba yake aligoma kunipa japo tulizoeana,basi nilikaa mpaka saa 12 jioni alipokua anatoka(ratiba yake niliijua). Alipotoka nikamfuata nikamsalimia akaniambia unaelekea wapi nikamwambia nakusindikiza akagoma akaniambia mzee wake akimuona itakua ishu sana,basi nikamwambia nataka nikupe huu mzigo ndo lengo nikamkabidhi kisha nikaondoka. Sikujua alifungua wakati gani lakini sikumuona kwa wiki nzima kila nilipoenda pale sikumkuta na nilishindwa kuuliza,mawazo yangu yalinituma labda ameamua kuacha kazi au amekasirika ujumbe ule basi nikawa nipo dilema.

Siku hiyo narudi zangu shule nasikia mtu ananiita kwa nyuma kugeuka ni yeye ,aisee nilifurahi sana yaani mno akaniambia bwana alikua amepatwa na msiba wa kaka yake siku ile ameondoka na aliporudi kazini alisikia nimeenda pale mara kadhaa hivyo alijua nimefuata jibu langu. Nilitabasam akaniambia nimuandikie namba yangu halafu ataniambia siku gani tuonane tuongee ebwana nilifurahi kinoma nikampa namba nikaondoka,njia nzima kwangu ilikua shangwe sana nikafika home fasta nikamcheki Jose nikamueleza akasema mtoto kashakubali huyo.

Kwasababu nilikua kwenye mitihani sikuweza kwenda kule tangu hiyo siku na yeye hakunitafuta mpaka zinatimia siku 5 nikiwa nimelala usiku nikaona namba ngeni inaingia haraka sana nikapokea kumbe yeye,dah nilifurahi sana alikua ananipa jibu langu kua amekubali lakini kwa masharti yafuatayo. 1.Tusizini kabisa 2.Nikimaliza kusoma nikatoe posa kwao 3.Niwe nafanya ibada 4.Nisifanye uhuni.

Masharti yote niliyakubali basi safari mpya ikaanza hapo mwanzo nilona naweza ila kadri ilivyokua inaenda nikaanza kuona masharti magumu hasa 1 na 3 ikawa kikwazo migogoro ikaanza kati yangu na yake. Huyu binti nilimgharamia sana kwa vitu vidogo vidogo na nilimpa zawaida nyingi kiasi ikaja kuteteresha imani yake Mungu anisamehe mwishowe nikamuingiza kwenye dhambi ya zinaaa na yeye nilimkuta bikra. Baada ya kutoa usichana wake nilimuahidi kumuoa kabisa na yeye akafurahi ,maisha ya mapenzi yaliendelea huu ni moja ya uhusiano niliofurahia sana kwasababu kila mmoja alijitoa kwa mwenzake kwa asilimia 100.

Siku moja nikamfuata pale kazini nikamwambia akitoka kazini apitie maskani pale nitakua na kaka yangu ili amuone binti akakubali na jioni kweli alikuja maskani nikamtambulisha kwa washkaji na kaka yangu furaha ikaongezeka.


Siku moja nilipigiwa simu na Rukia hapo nikiwa najiandaa kufanya Mock aliniambia nihakikishe tunaonana siku ile kwa vyovyote vile bila kukosa. Basi nikakutana nae akaniambia yeye ni mjamzito amenunua kipimo baada ya kua haoni siku zake na ameona mistari miwili dah sikuamini furaha na kuchanganyikiwa vilikuja kwa pamoja. Rukia alikua akilia na uoga maana mzee wake alikua mzee wa msikiti na mkorofi sana tukapata shauri kwenda hospital kuhakikisha na majibu yalikua yale yale na ikaonekana ina mwezi na nusu. Nilimsihi aende nyumbani asimwambie mtu wakati natafuta ufumbuzi niliporudi nyumbani nikamshirikisha bro dah alinilaumu sana kutokua makini wakati najua bado mwanafunzi(huyu si bro wangu wa damu moja ila naye ana historia yake adhimu sana nitaeleza siku nyingine).

Akaniambia fanya tukutane na bint tuone namna ya kutafuta vidonge atoe basi nikasema sawa,kesho yake nilipotoka shule nikaenda pale ofisini bint hayupo na siwezi kumpigia mpaka yeye anipigie. Nilikaa wiki sijamuona wala hajanitafuta nilipita sana kwao bila mafanikio yoyote sikumuona, nikiwa nimekaa kwa wiki mbili nikapigiwa simu na namba ngeni kupokea ni mwanamke sauti ya mtu mzima bwana alinicharura sana na kunikomesha nisijaribu kumsogelea mdogo wake. Nilikata simu kwa hofu japo hakusema anamlenga nani ila nilikua nishajua hivyo nikamueleza bro akaniambia tusubiri matokeo ,safari za ofisini kwake hazikuisha zaidi ya mwezi ndo nikaambiwa ameacha kazi.
Nilijua tena ndo basi mahusiano yameshaisha ,baada ya form 4 mi nikaondoka kwenda kuishi kwa Mzee kwenye nyumba yake nyingine sio kule kwa mwanzo maisha yaliendelea lakini bado nilikua nikimkumbuka mpaka baada ya muda nikaja kusikia HABIBU(jina lake halisi linafanana na hili) huyu ni muongoni mwa washkaji tuliokua tuna shinda pale maskani na baba yake ndo alikua mpiga adhana wa msikiti wa mtaani kwetu kua anaoa. HABIBU alikua amemaliza kidato cha Nne maiaka 3 iliyopita ila hakufanya vizuri akasoma kozi fupi halafu akaingizwa bandari kwa mgongo wa baba yake mdogo. Nilipata na mfadhaiko baada ya kusikia ana muoa RUKIA yule yule wa kwangu hapo ilikua imepita miezi 9 bila mawasiliano yoyote na jitihada zote ziligonga mwamba. Kwakweli nilijsikia vibaya sana maana Rukia nakiri alikua bint mstaarabu sana ,nilihakikisha kwa wana wakasema kweli na ilikua rahisi kutokana na ukaribu wa wazee wao dah hapo sikua na jinsi nikapiga chini japo kwa maumivu na kama ningeona mapema basi RUKIA ndiye angelikua mke wangu leo hii.

Wivu ulinikaba sana siku ya harusi ilipofika japo sikwenda na washikaji walipost kabisa kwenye status zao ,niliona wivu kwasababu jamaa alikua amepata mke wa maana sana na mpaka sasa jamaa yuko na maisha ya mafanikio sana kwasababu ya yule mke kampa utulivu mkubwa na huwa anasema sana kwa wana.

Baada ya miaka 3 nilikutana na Rukia kwenye daladala akiwa na mtoto wa mwaka mmoja dah wivu na uchungu ulinikaba ila bint yule mstaarabu sana alinisalimia kwa heshima na tuliongea mpaka nilipotaka kushuka na yeye alishuka aliniomba radhi na kueleza ile ishu alishtukiwa na dada yake hivyo kuepusha matatizo kwa baba yao waliitoa kabla ya mzee wake kujua nimsamehe kwa kutoa kiumbe changu na yeye ameshatubu kwa Mungu.

Sikua na jinsi na alinisihi nimsahau ameshakua mke wa mtu na ananiombea nipate mke ila niwe na subira. Nilipomuomba namba alininyima huku akitabasam aliniambia namba yako ninayo au umebadilisha nikamwambia hapana akasema basi nitakutafuta mimi mwenyewe ..alikuja kujintafuta baada ya mwaka baada ya msiba wa baba yake na hapo ndo tukawa tunawasiliana ila kwa heshima sana. Naheshimu sana ndo yake ila nakiri wazee huyu ndo bint ambaye mpaka leo tupo sawa japo si kimapenzi na tunawasiliana ikiwa kuna sababu ya msingi sana na mara chache.
 
Duuuh
 
Mara nyingi mabadiliko au hali za kimaisha huwa hazibadilishi mtu, bali mtu huyo huingia kwenye tabia yake halisi.

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ