py thon
JF-Expert Member
- Sep 11, 2016
- 2,476
- 4,448
Mapenzi yana nguvu kiasi gani ?
Pasi na shaka mapenzi yamebeba maisha ya mwanaadamu na huwezi kutengenesha maisha ya mwanaadamu na mapenzi hata mtu awe kauzu kiasi gani au busy kiasi gani lazima atatafuta mwenza wa kutulia nae na watu waliojikita kwenye utafiti wametoa nadharia mbalimbali kuhusiana na umuhimu wa tendo la ndoa na mahusiano miongoni mwa watu.
Licha ya mapenzi kuwa matamu pia ni machungu kwa upande wa pili wa shillingi ,mapenzi yanaweza kumfanya mtu awe na furaha iliyo na kifani na awe na ufanisi kwenye shughuli ama kazi zake lakini pia mapenzi yanaweza kuwa mwiba mchungu na kumfanya mtu ashindwe kufanya shughuli zake ,moods zimtoke na awe na stress na kushindwa kutekeleza kazi zake au kufanya chini ya kiwango.
1.Binafsi mapenzi sikuchukulia kama yanaweza Kumuumiza mtu sana mpaka nilipokutana na mzee wa makamo ya miaka 70 hivi akilia kisa mapenzi...Miaka kama 3 nyuma mtaani kwetu nilikuwa natembea karibu na msikiti mmoja ndipo babu mmoja aliniita na kuniomba nimwandikie ujumbe wa maneno kwakuwa kwa utu uzima wake anavaa miwani hivyo kumuwia vigumu ,niliitikia wito wake na hali niliyoiona mke wake alimkimbia na kwenda kuishi kwa mwanaume mwengine wakati mzee yule ananisomea maneno ili niyaandike kwakweli ni maneno machungu yanayoumiza licha ya umri wake wa miaka kama 70 na ameshaishi kwenye mapenzi kwa miongo mingi lakini mzee yule maneno yake yalikuwa yanaliza mpaka ilifikia hatua alisema mimi kwa siku hizi 2 ukiniona nimekufa usihudhurie mazishi yangu usije kwenye msiba wangu mzee alikuwa anatishia kujiua na message niliandika kama essay vile maneno yalikuwa mengi lakini machungu.
2.Kuna jamaa yangu alikuwa genius sana alisoma shule za vipaji na ana rekodi iliyotukuka kwenye makaratasi kuanzia la saba mpaka kidato cha 6 ila mapenzi ,mwanamke alikatisha ndoto zake na kuwa anakunywa pombe sana na stress kumfanya asitishe chuo.
Watu hudiriki kujiua kisa mapenzi ,watu hudiriki kuua kisa mapenzi,ufanisi wa kazi au shughuli hupungua kisa mapenzi ..hivi mapenzi yana nguvu kiasi gani mtu haumii nchi yake ikiibiwa trillion 2 lkn mpenzi wake akizingua huumia sana na kumfanya awe mpweke na hata kufanya maamuzi magumu au yakijinga
Hivi mapenzi yana nguvu kiasi gani