Kuna mambo mengine magumu kuyasema by word, and the expectation is that, mhusika anatakiwa asome alama za nyakati. ningekuwa mi ndo huyo dada ningeshasepa, unawezakuta huyo jamaa ana mke na watoto kabisa. na kwa ufupi jamaa ni msanii period!
mimi kitu cha kwanza ningefanya ni kuwa nae karibu....distance is something else
Mdada it takes more than kufua na kupika to win a man's heart. Kma unaweza sogea dar ukabe rofu otherwise utaishia tu kudhani anakupenda we na mwanao.
Just curious, tangu mwanao akiwa class one na sasa yuko form three!!!! hakuna ndoa hapo, move on. let the truth be told!
Omwana: Omwana wewe ni wa nyumbani?Aksante kwa ushauri preta, hila kaz i ndo zinatubana.
Kuna mambo mengine magumu kuyasema by word, and the expectation is that, mhusika anatakiwa asome alama za nyakati. ningekuwa mi ndo huyo dada ningeshasepa, unawezakuta huyo jamaa ana mke na watoto kabisa. na kwa ufupi jamaa ni msanii period!
My dia kiukweli inaumiza sana maana kupenda duh!tabu sana alafu for ur situation najua huwezi kupata mtu yyte now maana akili yako yoooote umeweka kwake yy unamfanya kama Mungu wako wa dunia,my dia cc wenye imani zetu tunamsubiri Yesu alisema atarudi(hatujui cku wala saa)sasa nyie mwasubiri nn?mpz endelea na maisha yako tu kama ipo ipo tu!tangu mtoto class 1?hiyo ni 10yrs bana! we utaishia kufua kupika na kuosha vyombo si ndo kazi za ma hous gal?(am real soory to say zis but nimeumia)naumia maana najua unapoteza mda sasa ww mwambie umepata jamaaanataka kukuoa alafu umwone kama ana nia kweli.
unaona sasa tofauti yetu hapo.....
hata mie naona hapo kila kitukiko wazi kabisa, huyu dada sioni kama ategemee ndoa. impliedly huyu jamaa anaonesha hana mpango na inawezekana huyu ana mke tayari kweli....
labda bibie atueleze wnakutana kila baada ya muda gani??
i will b back....noja nikadigest hili mpendwa wangu...Hana mke wala watoto kwa hilo nalijua vizuri na huwa nikienda dar nafikia kwake. Na sioni kitu chochote tofauti, yaani kama ni cm anapokea vizuri huwa hatuna kipindi maalumu naweza kwenda ghafla tu na yeye anaweza kuja hapa mwanza tunaonana mara kwa mara kwa kweli.
Mdogo wangu OMWANA, mambo uliyosimulia kama ni ya kweli yamenisikitisha. Cha kwanza muweke Mwenyezi Mungu katika maombi yako umuombe akuangazie, akufunulie na akupe mme mwema!!! Tukirudi kwenye msingi wa ombi lako, umbali kati yako na mtarajiwa (Dar vs Mwanza), na muda uliopita tangu muanzishe uhusiano bila kufikia hatima ya kuoana ni mrefu mno. Huyo jamaa asikudanganyie penzi analoonyesha kwa mwanao, hiyo naona ni janja yake tu ili akiwa jijini Mwanza uendelee kuwa nyumba ndogo yake. Nakushauri huyo jamaa umpe yaliyoko moyoni mwako kuwa wahitaji kuolewa ili uwe na maisha yaliyotulia. Nahisi huyu mwanamme anaweza kuwa ana mke na watoto tayari huko Dar na akiwa Mwanza anakutumia tu kama nyumba ndogo. Be careful, mjaribu kumueleza akupeleke kwake Dar hata kwa wiki moja tu, siyo akufikishie hotelini, akupeleke kwake. In summary, huyo jamaa ni msanii, anakupotezea muda, anza na tafuta mwingine!!! Niko bado hapa Mwanza, ukipenda ni PM tukutane kesho asubuhi nikupe ushauri nasaha, naondoka kesho jioni.
Hana mke wala watoto kwa hilo nalijua vizuri na huwa nikienda dar nafikia kwake. Na sioni kitu chochote tofauti, yaani kama ni cm anapokea vizuri huwa hatuna kipindi maalumu naweza kwenda ghafla tu na yeye anaweza kuja hapa mwanza tunaonana mara kwa mara kwa kweli.
Aksante sana ma mdogo, kwa kunishauri vizuri yaani uwezi amini nilivyosoma ushauri wako nimejisikia kulia, hana mke wala mtoto huwa nikienda dar nafikia kwake hanionyeshi chochote kibaya, wala sioni simu za wasi wasi wala nini kwa sasa siko mwanza niko huku manyara kikazi, mimi ni mgeni kabisa hapa jamii hata jinsi ya kutuma pm sijui dadangu, hila kwa ukweli nimefarijika na ushauri wako. Nami pia nimeliona hilo kama vile ananichezea tu na ndio maana nikaona niweke hapa na ndicho hasa kilichonifanya nijisajiri hapa jamii hili niweze kupata mawazo yenu. Masikini mwanangu anampenda kama babake, hila nitaanza jitihada za kumtoa akilini kidogo kidogo kwani ndoa ni mpango wa Mwenyezi Mungu na si kwamba labda mimi namng'ang'ania saana sema tu mapenzi ni upofu
Endela kuvumili tu huenda kuna vitu bado havijakaa sawa.
Nawasalimu wana jamii, pia nawapa pole na mihangaiko ya hapa na pale
Pamoja na salaam pia naombeni ushauri. Naomba kwa yeyote aliyetayali kunishauri anishauri kwa dhati ya moyo wake, si kukejiei wala nini sababu hii siyo hadithi bali ni kitu cha ukweli na ndo maana nimeamua kuleta hapa mbele yenu muweze kunishauri kwani niko njia panda.
Niko katika mahusiano ambayo kwa kweli yananiacha njia panda, nina jamaa yangu wa muda mrefu tu, binafsi yangu nampenda sana huyu bwana, japo na yeye anaonyesha kunipenda lakini simuelewi sana. Mimi nina mtoto ambaye sikuzaa nae, huwa anaonyesha mapenzi makubwa sana kwa mtoto wangu ikiwa ni pamoja na kunisaidia kumlipia ada, kuongea nae kwenye cm kama vile baba afanyavyo kwa mtoto wake, akiwa nae anamtambulisha kwa marafiki zake kwamba ni mtoto wake wa kumzaa mimi pia ananiita mkewe, tunaishi mbali mbali (yaani mikoa tofauti) yeye yuko Dar mimi niko Mwanza. Tatizo liko kwenye kufunga ndoa, nimekuwa nikiwambia mara kwa mara kufunga ndoa lakini amekuwa akinipa moyo kila kukicha kwamba usiwe na haraka tutafunga tu ndoa, hili si jambo la kufanyia haraka na maneno mengine kibao, tumependana tangu mtoto wangu akiwa darasa la kwanza na hivi sasa mtoto yuko kidato cha tatu.
Nikiwa karibu nae kwa kweli namuonyesha mapenzi yangu ya dhati kwa kumpikia, kumfulia na kufanya vile ambavyo mke mwema anatakiwa kufanya. Ndugu zake kama dada, kaka na wadogo zake wananifahamu, wao pia wanipenda pamoja na mtoto wangu na wanasema sisi hatumtambui mtu mwingine zaidi yako.
Moyo wangu huko kwake, sijisikii kuwa na mtu mwingine kabisa ni kwamba nampenda sana, na yeye pia anaonyesha kunipenda, hila siwezi jua moyoni mwake. Sasa wapendwa wanajamii naombeni msaada wenu wa ushauri, kama wewe ni mwanamke nisaidie kama ingekuwa wewe ungefanyaje na kama ni mwanaume angalia hii hali na unishauri kwa kuwa wewe ni mwanamume na hii hali ya mwanaume mwenzio unaionaje? Naomba tusifanye kejeli wala utani.
According to researchers the following are the main benefits(and suposedly the only ones) of marriage:
What are the benefits married people enjoy?
* Live longer
* Have better physical and emotional health.
* Are happier
* Earn more
* Enjoy better sex lives
* Save more so they have fewer money worries.
Kama hivi vyote anavipata kwa uhakika sioni kwa nini uhangaike na worries kuhusu baba watoto wako wa kufikia.