Harambee: Saidia wahanga wa mafuriko Tanzania; zaidi ya watanzania 1960, wamechangia!
Mzee Mwanakijiji
8th January 2010, 09:34 PM
Agenda for Action:
SIKILIZA MAHOJIANO NA TANZANIA RED CROSS:
SIKILIZA PRESS CONFERENCE:
SIKILIZA Mahojiano na Clouds FM:
Rais wa mtandao wa wanataaluma Tanzania(TPN), santus Mtsimbe, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana, kuhusu TPN kwa kushirikiana na jamii Forum kukusanya Sh 10 bilioni za kuwasaidia waathirika wa mafuriko nchini. Picha na Michael Jamson.
Source:
http://www.mwananchi.co.tz/mwanaglob.asp
TPN, JamiiForums na Michuzi walipowasilisha michango ya awamu ya kwanza Tanzania Red Cross Januari 15, 2010.
Meya Kimbisa pichani akipokea misaada ya awali; Aliwashukuru wana-Mitandao na TPN kwa jitihada zao katika janga hili na kuomba wasiache kutoa ushirikiano pindi watakapohitajika! Misaada iliyokabidhiwa ni fedha taslimu TZS 1,068,000.00 na vifaa vyenye thamani ya Tshs 1,400,000/=
Kwa kushirikiana na tovuti za Jamiiforums na Mdau wa Jamii Bw. Issa Michuzi; pamoja na kushirikiana na Mtandao wa Wanaataluma wa Tanzania (TPN) tumeandaa mpango wa kuwashirikisha Watanzania mahali popote pale walipo kuchangia katika adha hii inayowakuta ndugu zetu katika mikoa mbalimbali hasa Morogoro, Dodoma, na sasa hivi Shinyanga na hata Mwanza na kuna uwezekano wa sehemu nyingine nchini kwa kadiri siku zinavyoendelea.
Tumeamua kutumia Chama cha Msalaba na Mwezi Mwekundu cha Tanzania kwani rekodi yao katika kufika na kutoa misaada wakati wa majanga hailinganishwi na chombo au taasisi nyingine yoyote. Zaidi ya yote tumepata uhakika wa kutosha wa misaada yetu kufika kwa walengwa baada ya kuzungumza na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mstahiki Meya (Dar) Adam Kimbisa (CCM).
Pata nakala ya mpango huo hapa:
http://www.box.net/shared/g99no7hjkg
Maelezo zaidi yanapatikana kwenye Programu ya Harambee!
Kuna tofauti kati ya kulalamika, kuhamasika na kutenda; Mwaka huu tunaenda kwenye kutenda. Hofu yangu ni kuwa yawezekana hatuko tofauti sana na jamii tunayotaka kuiongoza kuleta mabadiliko.
Nafahamu ni rahisi sana kwa wana JF kutupa lawama na kusikitika lakini ni vigumu mno kuamka na kutenda; lakini kuna wakati ambapo dhamira zituongoze kufanya vitu vizuri au tuombe misaada kwa Wamarekani utashangaa watakavyochangamka kutusaidia! Hili ni la kwetu na ningependa kuona ni jinsi gani sisi wenyewe tunaweza kufanya kitu.
Nimezungumza na Meya Kimbisa na nimepata baraka zake za kushirikiana na Red Cross TZ kwa ajili ya lengo hili. Tutawapa update baadaye leo tukishakamilisha modalities of what need to be done and by who and how. Silali leo.
=============================
JINSI YA KUCHANGIA:
Tumebuni njia mbalimbali za kuweza kuchangia vitu kama vyandarua, maboksi ya maji safi, nguo, madawa (ambayo hayajapita muda au kufunguliwa), mahitaji ya watoto na kina mama n.k.
A: MOJA KWA KWA MOJA KWA CHAMA CHA MSALABA MWEKUNDU
1. Peleka msaada wako moja kwa moja kwa Chama cha Msalaba Mwekundu kilicho karibu nawe. Kupata taarifa za Chama cha Msalaba Mwekundu wasiliana nao:
P.O. Box 1133
Dar es Salaam
Simu: (00255) (22) 215-0330/ 215-1839/215-0843 Email:
logistics@raha.com
B: KUTUMIA MTANDAO WA WANATAALUMA WA TANZANIA (TPN).
Hivyo TPN itakusanya michango yetu kwa njia mbalimbali hapa chini na kuiwasilisha kwa TRCS na kutoa taarifa za mara kwa mara za maendeleo ya kampeni hii.
2. Kuingiza Benki au kuhamishia fedha benki(bank deposit and transfers):
· Jina la Akaunti: Tanzania Professionals Network,
·
Jina la Benki: CRDB Bank ; Tawi: Lumumba
·
Jiji: Dar Es Salaam; Nchi: Tanzania
·
Swift Code: CORUTZ TZ
· US $ (Fedha za kigeni) A/C No: 02J1 007 608 900;
· TZS A/C No: 01J1 007 608 901
C: KUTUMIA MITANDAO YA SIMU
3. M-Pesa (Vodacom): 0768 777 888
4. Z-Pesa (Zantel): 0773 88 18 88
5. Zap (Zain) 0784 00 88 99
6. Michango ya kutumia makato ya kila siku ya Airtime za simu:
"Changia
Shs 150 kwa siku kwa waathirika wa mafuriko. Tuma SMS yenye neno
TPN kwenda
15522. Utakatwa
Shs 250 kujisajili. Kwa maelezo zaidi wasiliana na
0715 740 047.
7. Western Union - Tuma kwa jina la: Mr. Emmanuel Mmari; TPN Finance and Administrative Manager; Dar Es Salaam; Tanzania. Tuma nakala ya MTCN kwa
president@tpn.co.tz,
info@jamiiforums.com na
mwanakijiji@jamiiforums.com ili kuweka rekodi sahihi.
8: Michango ya vitu mbalimbali: Ofisi za TPN - Barabara ya Nyerere; Jengo la TOHS; Ghorofa ya kwanza, karibu na TBC (RTD) Radio. Piga simu 0715 740 047 kwa kupata msaada wa kuja kuchukua vitu kama huna usafiri.
M. M. Mwanakijiji