Dada yangu omwana, kufikia kwake na kupokea simu free si kigezo cha kukufanya wewe uwe na uhakika kwamba jamaa hajaoa.kuna jamaa nilikuwa nafanya naye kazi, jamaa alikuwa mjasiriamali mzuri tu ana mke na mtoto mmoja. lkn jamaa ana nyumba mbili fully furnished. moja anaishi na mke wake mitaa ya kinondoni, halafu ana ki apartment kapangisha mbezi beach, huko sasa anahamia pindi mchumba wake km mwenyewe anavyomuita akija toka uganda. anamuaga mkewe anakwenda kibiashara uganda anapanda basi anashuka kibaha anarudi mbezi beach, anakodisha gari full tinted na line anabadilisha so anakuwa hana mawasiliano na wife wake, kwa mtindo huo akija huyo mchumba wake anakuwa free na simu kupokea, kuandika sms, mchumba toka uganda anajua kapata kumbe kapatikana. zoezi likiisha ile geto inabaki ya mauaji mafupi mafupi. nadhani sasa omwana utakuwa umepata full picha, unapotezewa muda tu, kakufanya nyumba ndogo huyo.