Mapenziii au wizi????

First Born

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2011
Posts
5,312
Reaction score
1,475
habari wakuu,

Siku mbili tatu hizi kuna binti nimekuwa nikichati nae kupitia e.mail, yeye yupo senegal.
Katika mazungumzo/kuchati huku kuna hali isiyo ya kawaida anataka kuja nayo kwangu, huenda imekutokea wewe au kwa vyovyote lakini mimi yamenifikia! Naomba nikushirikishe tujadili hili ili tukigundua kuwa ni mwizi wana jf tuwe macho.

huyu binti alini PM kupitia humu, kabla sijamjibu nikashangaa tayari kashapigwa ban. Lakini kwa kuwa alikuwa ameniachia email nikamjibu.
Mwanzoni alidai eti alikuwa anatafuta rafiki lakini baadae akaanzisha mada nyingine kuwa eti yeye huko alipo yupo kama mkimbizi na wapo makambini kiasi cha kutokuwa hata na uhuru.


Anadai yeye ni mtoto pekee wa Dr mmoja aliekuwa tajiri ambae alifariki dunia. Kwa muda huu anadai anahitaji sana kuwa huru kwani huko anahisi kama yupo kifungoni na anahitaji sana kuwa huru.

Anasema ametokea kuniamini sana hivyo nimsaidie kwa namna yeyote ili aje Tz ikiwezekana awe mpenzi wng, she said that she has never been married and she is single.

Msaada alioniomba zaidi ni wa kumsaidia kumtolea pesa zake akaunti aliyokuwa amewekewa na her late father $7.5 millions kwa jina lake nimhamishie kwenye akaunti yangu ili nimtumie tayari kwa yeye kuja kuishi tz

Machale yananicheza sana, anadai kabla ya kufanya chochote alimwomba Mungu na akaonyeshwa eti mimi ndo msaada wake. Kanitumia picha kibao kwenye E.mail yangu kunivutia na uzuri wake. Na kiukweli picha nilizopokea ni kali kinoma.

Kanitumia maelezo yote kuhusu namna nitakavyoweza kuhamisha hizo pesa kwenye akaunt yangu, kanipa na akaunti namba ya babake pamoja na e.mail ya bank manager.



Maswali yanayonipata::


1. Huyu ni mwanamke kweli?

2. Huyu anaongea ukweli?

3. Kanipatia namba ya simu ya mtu ambae ye anadai ni mchungaji wake kwa hiyo nimpigie ili aniunganishe nae kwani yeye hana uwezo wa kunipigia, sasa inakuaje anaweza kuwasiliana kupitia email ashindwe kunipigia?

4. Nimemwomba ampe maelekezo hayo huyo pasta wake ili amsaidie kutolea hizo pesa, lakini anadai eti jamaa hataweza kisa anawasaidia wengi, sasa unaonaje hiyo?


Naombeni mawazo yenu, huyu ni mpenzi au mwizi??


ASANTENI,
Mie Mzaliwa wa Kwanza
 
yan wewe! Utapeli wa wazi kabisa huu unashindwa kuugundua? ? Hahahahaha! Wacha tamaa kijana! Kimbia utaingizwa choo cha kike sasa hv!
 
If it looks like a duck, swims like a duck, and quacks like a duck, then it probably is a duck. It sounds like a scam to me and she sounds like a scam artist herself.

So I'd counsel you not to be that credulous and believe such nonsense. I am even amazed at you for entertaining such correspondence. I normally don't even give the time of day to those kinds of e-mails.

But the choice is yours.
 
Hawa wa Nijeria wamejaa kwenye kila mtandao utawakuta kuanzia...g5click,teentz,twitter,JF....yaani kila sehemu....yaaani ni utapeli wa kijinga kabisa...dunia ya leo hii nani akupe hela..akuamini kiasi hicho...achana nao mkuu
 
thanx NN, nakupata boss.
 
yan wewe! Utapeli wa wazi kabisa huu unashindwa kuugundua? ? Hahahahaha! Wacha tamaa kijana! Kimbia utaingizwa choo cha kike sasa hv!
hahahahahahahahahahahahaaaa!!! Mie mwanaume mum nisije nikakojoa kwa kuchuchumaa! I gate you Lady.
 
una umri gani? maana wizi wa aina hii umeanza kitambo, nashangaa wewe bado haujaujua, ndio maana nataka nijue umri wako ili nisiendelee kukushangaa.
 
Hawa wa Nijeria wamejaa kwenye kila mtandao utawakuta kuanzia...g5click,teentz,twitter,JF....yaani kila sehemu....yaaani ni utapeli wa kijinga kabisa...dunia ya leo hii nani akupe hela..akuamini kiasi hicho...achana nao mkuu
machare kundesa babaangu, kiinglish chenyewe ni cha kinigeria kabisa. Afu anadai yeye msenegal, Ngastuka pumbatupu!
 
Do even have an idea of US$ 7.5millions? Unafanya mchezo wewe. Yaani mtu hakujui kabisa akuruhusu uhamishe pesa zote hizo kwenda kwenye akaunti yake?


Hapo utashangaa, in the process huyo mchungaji feki na bank manager feki atakwambia unatakiwa kutuma USD 200 kama fees or whatever, na ndio utakuwa umeliwa. Wanafanya hivyo kwa kuwa ni rahisi sana mtu kushawishika kutuma USD 200, sasa akiwapata watu 100 tayari ana USD 20,000!!
 
Nakupata mkuu.
 
kha! hata sijaisoma, nimeishia hiyo line ya kwanza kwenye 'senegal'. utapeli wa kizamani kweli huu!
 
Hivi wewe huna akili hebu angalia sura kama hizo zinapatikana kwenye kambi ya wakimbizi hebu google hii kitu Romantic scammer ndo utaelewa kuwa umesimama kwenye mlango wa choo cha kike ukisubilia ilikhali choo cha kiume mlango uu wazi
 
Dunia yote ilishatahadhalishwa siku nyingi juu ya aina hii ya wizii unaofanywa na baadhi ya wananchi wa nchi za Africa magharibi hasa Nigeria.
 
Huu ni Utapeli tu
Hakuna ukweli wowote ktk hili

Nina more than twenty mails asking the same, Bahati mbaya kuna mail kutoka kwa watu tofauti

ila wametumia picha moja

ACHANA NAO KABISA
 
Mi nashindwa kuelewa hapa,uhamishie hela zake kwenye account yako?Mmh!Is there any utapeli?
 
mbona haya ni mambo ya zamani sana jamani, hivi kuna binadamu hasiyejua wizi/utapeli huu?
 
Kwanza ingekuwa mimi ningefanya ifuatavyo:
1.Yeye amesema yupo senegal,ningeangalia Email Header zake na kujua source ya e-mail imetoka wapi? kama ni senegal ningemwambia kwanza anitumie yeye hela nifungue account,kama ni naigeria nisingmjibu ningempotezea tu!
2.Hizi 419 zipo nyingi na mda mrefu sana nashangaa bado ujazijua,mie nakumbuka tangia 2004 walinitumia lakini nilkikuwa nazipoteze coz nawajua ni wezi
 
Hiyo single wanaitumia sana hao watu,ni matapeli balaa ole wako umpe acc yako ndio utakapo jua anakupenda na kukuamini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…