POTOSHI Mapepo ya CHADEMA yarejea upya, Makete wamkataa Heche

POTOSHI Mapepo ya CHADEMA yarejea upya, Makete wamkataa Heche

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1


Screenshot 2026-06-08 101543.png
 
Tunachokijua
Kumekuwapo na video inayosambazwa mtandaoni ikiwaonesha wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, wakionekana kulalamikia kukiukwa kwa utaratibu ambapo mmoja wao anasikika akisema "Tunataka kuvunja katiba ya chama chetu kwa kutumia madhaifu ya CCM kuwaleta ndani ya chama hiki" Video hiyo imeambatanishwa na kichwa cha habari "MAPEPO YA CHADEMA YAREJEA UPYA, MAKETE WAMKATAA HECHE"

Je, ni upi uhalisia wa video hiyo?

Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia Reverse Image Search umebaini video iliyochapishwa YouTube na Global TV mwezi Mei 27, 2024 ambapo ilieleza kuhusu Uchaguzi wa marudio wa CHADEMA mkoa wa Njombe ulipotajwa kuingia dosari baada ya madai kuwa msimamizi wa uchaguzi alikiuka kanuni na katiba yao.

Msimamizi wa Uchaguzi huo aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Bara, Benson Kigaila aliondoka ukumbini baada ya vurugu iliyoibuka.

Awali katika uchaguzi huo uliokuwa ukiendelea katika ukumbi wa Milimani Motel mjini Njombe baadhi ya wajumbe kutoka wilaya za mkoa wa Njombe waliomba muongozo kuhusu uhalali wa wajumbe wa wilaya ya Makete ambao uchaguzi wao ulikatiwa rufaa makao makuu ya chama hicho na kisha kuundwa kikosi kazi (Task Force).

“Uchaguzi ulifanyika Makete kwa sababu haukuwa wa kikanuni na kikatiba, tukamuomba msimamizi wa uchaguzi atufafanulie ili tuweze kuelewa kwa sababu chama hiki ni chama kikubwa ambacho watu wanakitegemea kije kiwasaidie sasa kama kiongozi mkubwa anakaidi mawazo na maoni ya viongozi wake haiko sawa sawa,” walisikika wakisema wanachama

Awali akizungumza na wajumbe wa mkutano huo, Benson Kigaila alisema kama kuna kifungu cha katiba kimekiukwa watumie kulalamika kwenye kamati kuu.

Ikumbukwe kuwa Uchaguzi wa Chama hicho Mkoa wa Njombe uliofanyika Aprili 9 2024 ngazi ya mkoa ulifutwa kutokana na baadhi ya viongozi na wanachma kutoridhishwa na mwenendo wa uchaguzi huo.​

Back
Top Bottom