Uchaguzi 2020 Mapigo matatu kwa Bernard Membe katika harakati zake za kuitafuta Ikulu

... ndio hiyo simple majority aliyekuzidi hata kwa kura moja ndiye mshindi; yaani wewe una 17% na yeye ana 17.0001% yeye ni mshindi. Mkapa ndiye aliyefuta ile ya at least 50%.
Sijui walikuwa wanaogopa kuangushwa? Hawajiamini!
 
Bernard Membe amekuwa akipitia nyakati mbalimbali za machungu makubwa kwake katika harakati zake za muda mrefu za kuitafuta Ikulu ya Chamwino. Mapigo hayo yamezidi kufifisha ndoto yake hiyo ya mchana ambayo amekuwa akiiota kila uchao.

Pigo la Kwanza: Hili pigo alilipata mwaka 2015. Ni dhahiri kuwa mwaka ule alikuwa ameshaanza hata kufanya rehearsal ya kuapishwa, na alikuwa ameshaanza hata kutembea kimapozi kama Rais kwani alikuwa na uhakika kwa asilimia nyingi kuwa angeweza kuwa Rais wa Tanzania. Pigo kwake ilikuwa ni Kamati Kuu ya CCM kumkata jina, na hivyo kumuondoa kwenye orodha ya majina ya Wanachama Watatu ambao majina yao yalipelekwa kwenye Mkutano Mkuu ili kupigiwa kura na hivyo kumpata Mgombea kupitia chama hicho.

Pigo la Pili: Hili pigo alilipata baada ya kuvuliwa uanachama wa CCM. Baada ya kukosa nafasi hiyo, Membe bado aliendelea kuwa na imani kuwa mwaka 2020 atagombea nafasi hiyo. Matokeo yake ni kuwa alikamia sana hata akawa anavunja misingi waliyojiwekea kama chama, na hata mara nyingine akaonekana kuwa ni mtovu wa nidhamu. Hali hiyo ilipelekea chama kumvua uanachama wake, na hivyo likawa ni pigo lake la pili.

Pigo la tatu: Upinzani nao wote wamemkataa mchana kweupe. CHADEMA wamekataa kuungana naye, na hivyo kila chama kimeendelea na mchakato wa uchaguzi kivyake. Membe amebaki na ACT yake ambayo alihamia baada ya CCM kumtema. ACT-Wazalendo walimuahidi kumpa nafasi ya kugombea Urais kupitia chama hicho. Membe kipindi fulani alisema atakuwa tayari kugombea iwapo upinzani wangeamua kuungana na kumsimamisha yeye kama Mgombea wao. Ni dhahiri kuwa alijipa “Face Value” kubwa sana wakati wapinzani aliotaka waungane wanamuona kuwa ana “Actual Value” ndogo sana. Membe alitamani sana Chadema wakubali kumuunga mkono yeye; hivyo kitendo cha Chadema kumtema na kumteua Lissu kuwa Mgombea wao na Salum Mwalimu kuwa mgombea mwenza limekuwa ni pigo jingine kwa ndugu yetu Membe.

Yajayo yanafurahisha, Uko Tayari?

Non Sense.
 
mimi membe sijawahi kumuhamini hata siku moja, namuona kama mCCM damu damu aliyelelewa na CCM tangu enzi za chipukizi aliyeletwa uku upinzani kama ilivyokuwa kwa lowasa, sumaye, akina guninita na ata mzee kingunge kuja kutughiribu tu ili baadae atuhache kama alivyotufanyia Lowasa.

Pia tukumbuke kuna mda Bashiru Ally aliwai kusema kuwa wanaweza kumsamehe ili arudi kundini ikiwa na maana kuwa bado ni mtu wao na uku upinzani ni mpango wao maCCM kuwa akiumaliza tu mpango wake atarejea uko.

Kumbukeni kuwa Membe mwenyewe was quoted as saying " Ukiwa kachero ni kachero mpaka kaburini" . Ni kachero wa ccm mpaka kufa!!!
 
Ni Membe yupi unayemzungumzia wakupata 38 % ? Akipata 8 % nishitue.

Labda kuna Membe mwingine atafufuka kutoka wafu. Huyo tuliyenaye hata hiyo 8% ni kubwa sana kuifikiria tu
 
Bernard Membe amekuwa akipitia nyakati mbalimbali za machungu makubwa kwake katika harakati zake za muda mrefu za kuitafuta Ikulu ya Chamwino. Mapigo hayo yamezidi kufifisha ndoto yake hiyo ya mchana ambayo amekuwa akiiota kila uchao.

Pigo la Kwanza: Hili pigo alilipata mwaka 2015. Ni dhahiri kuwa mwaka ule alikuwa ameshaanza hata kufanya rehearsal ya kuapishwa, na alikuwa ameshaanza hata kutembea kimapozi kama Rais kwani alikuwa na uhakika kwa asilimia nyingi kuwa angeweza kuwa Rais wa Tanzania. Pigo kwake ilikuwa ni Kamati Kuu ya CCM kumkata jina, na hivyo kumuondoa kwenye orodha ya majina ya Wanachama Watatu ambao majina yao yalipelekwa kwenye Mkutano Mkuu ili kupigiwa kura na hivyo kumpata Mgombea kupitia chama hicho.

Pigo la Pili: Hili pigo alilipata baada ya kuvuliwa uanachama wa CCM. Baada ya kukosa nafasi hiyo, Membe bado aliendelea kuwa na imani kuwa mwaka 2020 atagombea nafasi hiyo. Matokeo yake ni kuwa alikamia sana hata akawa anavunja misingi waliyojiwekea kama chama, na hata mara nyingine akaonekana kuwa ni mtovu wa nidhamu. Hali hiyo ilipelekea chama kumvua uanachama wake, na hivyo likawa ni pigo lake la pili.

Pigo la tatu: Upinzani nao wote wamemkataa mchana kweupe. CHADEMA wamekataa kuungana naye, na hivyo kila chama kimeendelea na mchakato wa uchaguzi kivyake. Membe amebaki na ACT yake ambayo alihamia baada ya CCM kumtema. ACT-Wazalendo walimuahidi kumpa nafasi ya kugombea Urais kupitia chama hicho. Membe kipindi fulani alisema atakuwa tayari kugombea iwapo upinzani wangeamua kuungana na kumsimamisha yeye kama Mgombea wao. Ni dhahiri kuwa alijipa “Face Value” kubwa sana wakati wapinzani aliotaka waungane wanamuona kuwa ana “Actual Value” ndogo sana. Membe alitamani sana Chadema wakubali kumuunga mkono yeye; hivyo kitendo cha Chadema kumtema na kumteua Lissu kuwa Mgombea wao na Salum Mwalimu kuwa mgombea mwenza limekuwa ni pigo jingine kwa ndugu yetu Membe.

Yajayo yanafurahisha, Uko Tayari?
umenichekesha kwenye pigo la kwanza hakika yajayo yanafurahisha
 
Mkuu, lakini endapo matokeo ya uchaguzi hayatatoa mshindi wa zaidi ya 50%, yaani tuseme Membe akipata 38% Lissu 40% na Magufuli 22% itapasa uchaguzi uingie "round" ya pili, na kwa vyovyote vile itampasa Membe apambane na Lissu, na ni lazima wana CCM watamuunga mkono Membe, kwa kuwa zimwi likujualo ....
Magu anapita kwa kishindo

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Basi kwa kupitia dhana hiyo Tundu Lissu atakuwa anasubiri kuapishwa kama Rais mteule wa JMT.

Watu mko vizuri sana kujipa matumaini ambayo mioyo yenu inakataa. Full Internal Contradiction
 
Mkuu, lakini endapo matokeo ya uchaguzi hayatatoa mshindi wa zaidi ya 50%, yaani tuseme Membe akipata 38% Lissu 40% na Magufuli 22% itapasa uchaguzi uingie "round" ya pili, na kwa vyovyote vile itampasa Membe apambane na Lissu, na ni lazima wana CCM watamuunga mkono Membe, kwa kuwa zimwi likujualo ....
Kwa katiba ipi mkuu?
 
Back
Top Bottom