Mapinduzi makubwa duniani yameletwa na matumizi ya zana za madini ya chuma, ni heri uache vyote ili uchimbe chuma kama unayo

Hii itakuww pigo kubwa sana kwa China.
 
Hivi unasemea hivi vyuma tunavyo uza 1kg = 300tsh/= tuchimbe madini yake ambayo ni malighafi ?
Mtoa mada atakuwa hajasoma kitu kinachoitwa "DEMAND AND SUPPLY" how price is affected by Dd & Ss😆
 
Eeenh, Sawa mkuu 'Mokaze'.

Wewe ni 'mhunzi'?

Nimependa ulivyoeleza jinsi ya kupata hivyo vyuma vya aina mbalimbali,... hebu endelea hadi kule kwa 'graphine basi; kwa vile naona una mwelekeo wa kuyafahamu haya mambo!

Nimesoma hii mada hadi nilipofikia mchango wako nikaona kuna urahisishaji wa mambo mengi yahusuyo chuma.
Ndiyo, pamoja na kuendelea kuwepo na umuhimu wa madini haya katika matumizi mengi, tusisahau kwamba teknologia imekwishakuwa kubwa na kupanuka zaidi. Hatuwezi kukiona chuma katika mwonekano uleule uliokuwepo miaka mia mbili iliyopita.

Ndio, nadhani Tanzania ingefaidika zaidi kama ingeweka mikakati ya kuchimba na kuendeleza utumiaji wa chuma chake katika kutengeneza bidhaa mbalimbali zitokanazo na mali ghafi hiyo hasa katika wakati huu. Tungeunganisha madini yetu mbalimbali kama 'nickel' na 'graphite', madini ambayo sasa yanachimbwa na kusafirishwa nje na kutengeneza aina mbalimbali za vyuma vyenye thamani kubwa na kutengeneza bidhaa mbalimbali kama mafriji, majiko na vitu vingine chungu nzima.

Pamoja na yote hayo, tukumbuke pia tunapojadili bidhaa ya chuma kama anayoiongelea mleta mada, tujiulize bei ya chuma duniani sasa hivi ikoje.? Ni nani watengenezaji wakubwa wa bidhaa hii na wameshikilia soko kwa kiasi gani. Tutaweza kushindana ndani ya soko hilo analotamba nalo mChina?
 
Mtoa mada atakuwa hajasoma kitu kinachoitwa "DEMAND AND SUPPLY" how price is affected by Dd & Ss😆
Haya sasa!

Si hivyo tu. Inabidi tuangalie pia tunataka kuitumia chuma yetu kwa bidhaa zipi. Je teknologia ya kuvitengeneza hivi vitu tunayo?

Hii 'dhana' yetu mbovu ya "hatuwezi" tutaiweka pembeni na kudhamiria kufanya kweli?

Soko la bidhaa za chuma lipo sana. Hivi vi-nchi vya Afrika vyote, hata kama vinakwenda taratibu, lakini vinaendelea. Vitahitaji bidhaa hizi katika maendeleo yao. Kwa nini chuma kitoke China kiuzwe rahisi kuliko hiki chetu kitakachotengenezwa hapa hapa Afrika? Kama AfCFTA itafanya kazi, kwa nini sisi tusiwe ndio nchi ya kuwapatia chuma hawa wengine wote katika umoja wetu?

"Kupanga ni kuchagua"; kama tukipanga na kudhamiria kwa dhati kufanya hilo ndilo liwe mchango wetu mkuu katika umoja huo, kwa nini isiwezekani? (kama tutaweza kupata uongozi wenye uthubutu), na sisi sote tutakuwa na 'mindset' hiyo hiyo ya uthubutu.
 
Hawa jamaa unaowaona wanashinda 'vijiweni' kila kona ya Tanzania,..., hawa ni 'vipuli' tele tunavyotakiwa kuvitumia, lakini kwa ushamba wetu, tunaviacha vinaozea hapo hapo.
Akitokea mtu (kiongozi), aseme anataka kuvitumia ipasavyo 'vipuli' hivi..., kwa nini visiweze kutumia kutimiza hayo uliyoandika hapa. Vyuo vya ufundi vipo, na vingi vingine vinaweza kujengwa kwa muda mfupi tu! Ndani ya miaka mitano, tunaweza kuwa na hali tofauti kabisa na ilivyo sasa. Ni swala la 'UTHUBUTU' tu na kuwa na dhamira halisi ya kutaka kutekeleza jambo. Hizi sifa kwa bahati mbaya viongozi wetu na sisi wenyewe hatujafanikiwa kuzitumia ipasavyo.
 
Mbarikiwe sana

Uzi wangu bora wa siku
 
Tunazo faculties za uhandishi vyuo vikuu, tunavyo vyuo vya kati vya ufundi, tuna SIDO, VETA, TIRDO, COSTECH, Nyumbu na wahunzi Tanzania. Sisi tulipaswa kuunda 80% ya viwanda vyetu vinavyozalisha bidhaa zetu na za kuexport. Brother hata vijiko na masufuria tunayaagiza kutoka nje. Nani katuroga?

Nickel haiwezi kutufikisha popote sisi kuliko chuma.
 
Quenched steel yenyewe vipi.
Ila nashukuru umefanunua Poa sana. Ile kemia f4 ilinitoaga nishai mana haikuwaga na kanuni ni full maelezo. Niliichukiaga sana. Sijui ni inorganic chemistry.extraction of metals and its oxides. Yaani kemia Nilikuwa naiona mchawi natamani ningekuwa na uwezo Wa kukomaa na fizikia and maths only.

 
Ni kweli tuna mabilion ya tani za chuma zipo ardhini...hizi ndiyo zingetumika kujengea reli yetu ya kisasa ili kupinguza gharama; kama tungeamua kuanza kuchimba madini haya ya chuma kwanza hiyo reli ingetumia chuma hiki hiki cha Mchuchuma na Liganga!! Tena chenye ubora mzuri

Sasa kwa kuwa bunge letu limebakia kibigoyo basi tena!! Hizi hoja hakuna wa kuziibua...kwa sasa ni utekelezaji wa miradi mizigo kwa wananchi ndiyo inayopewa kipaombele... maisha yanazidi kuwa magumu...ajira kwa vijana wetu ndiyo kabisaa!!
 
Kesho tunazindua shamba la miti chato hiyo habari ya chuma haituhusu karibuni sana chato
 
Kama tunataka maendeleo ya kweli ambayo yatawaudhi wazungu hatuna budi kutumia our uncommon sense, maana common sense ya hatuwezi, hatuna mtaji, hatuna technolojia ndiyo iliyotufikisha hapa tulipo. Lazima tuseme tunaweza na tuanze sasa. Viongozi wetu ni rahisi sana kuelekea kwenye dhahabu na almasi kwakuwa ni rahisi kupewa tofali la madini hayo kama zawadi binafsi. Kwenye chuma mambo hayo hakuna hivyo hayawavutii viongozi kuelekea huko. Lakini ni heri pesa yote ya dhahabu, almasi, germstones na nickel tukaitumia kwenye kwenye kusomesha watoto wetu kokote duniani kuhusu chuma na matumizi ya chuma, technolojia ya kutengeneza bidhaa za chuma na uchimbaji wa chuma. Baba wa taifa alishaianza hiyo kazi pale UFI ubungo, Mang'ula na arusha, SIDO nk lakini hatukumuelewa hata kidogo. Leo hii hata jembe la chapa jogoo linaagizwa kutoka china.
 
Kiongozi yuko tayari kuleta mzungu afundishe timu ya mpira kuliko kuleta mtaalamu wa kufundisha namna ya kutengeneza bidhaa za chuma kama matrecta. Badala ya kuuza bidhaa za dhahabu kama pete, mikufu, bangili, mikanda ya saa, makombe na mikanda ya mashindano mbalimbali sisi tunafurahia kuuza matofali ya dhahabu na malipo ya milabaha.
 
Iko siku watu watalipa kodi ya kuvaa chupi. Wanakamua ng'ombe asiyelishwa wapate maziwa ya nunualia vyuma toka china.
 
Tafuta sasa na documentary za railroads Australia uone how remote wanapotoa hizo iron ore, line ya reli inayofuata chuma ina kilometa ngapi na ukubwa wa train zenyewe ili kupata advantages za economy of scales: wakati sisi kujenga kilometre 500 za reli tu hela mtaani aionekani kila mtu analia.

Ujafika kwenye investment za heavy metal na zenyewe zinahitaji umeme wa uhakika, supporting infrastructure kama reli jumlisha na gharama za kiwanda chenyewe. Ukishafanikisha hayo inabidi uwe nafuu ili uweze ku import maana uzalishaji wenyewe unaweza jikuta unahitaji tonne elfu kadhaa kwa mwaka ili ufikie break even point si ajabu ni kiwango ambacho Tanzania pekee akiwezi tumia kwa hali ya leo.

Mteja wako mkubwa kwa sasa ni serikali ya Tanzania ambae ndio huyu huyu kujenga SGR deni la nchi limeongezeka maradufu.

In other words kujenga kiwanda cha chuma unamwambia serikali akakope kiasi karibu na ujenzi wa phase mbili za SGR, halafu akitoka hapo atafute na hela ya kununua hiyo chuma ili ajenge SGR (wakati kuisha haraka kwa SGR kuna benefit zingine kubwa za kiuchumi).

Hakuna nchi itaikopesha Tanzania kujenga icho kiwanda cha chuma kwa uchumi wake wa sasa na kwa upande wa soko la dunia Tanzania aiwezi zalisha chuma ya ku populate ata soko la Kenya na Uganda tu kwa ushindani wa bei kutoka kwa wazalishaji wakubwa.

We Tanzanians need to be realistic kuliko kutoa demands tu.
 
Quenched steel yenyewe vipi.



Quenching ni mchakato wa kufanya steels ziwe ngumu na imara (hard and tough), hii inahusisha kuchoma steels hasa iron based steels, katika curie temperature na kisha kupozwa kwa haraka kwenye coolant, coolant inaweza kuwa maji, brine (salt water), oil, nk.


Sio Quenching tu bali kuna njia nyingi za ku treat steel ili kupata sifa zinazohitajika, mfano kuna Annealing--- ni kuchoma steel ngumu katika joto la Curie na kisha kuachwa ipoe polepole yenyewe ili iwe laini kwa ajili ya machining nk.

Kuna Tempering-- hii ni kuchoma steel iliyokuwa Quenched ili kupunguza internal stresses zilizojijenga ndani ya Chuma ili kisivunjike kama glass wakati wa matumizi.

Kuna Normalising--- huu ni mchakato wa kurejea tabia ya asili ya chuma baada ya kuchomwa na kupondwa wakati wa forging (forging ni upondsji wa steel kupata shape inayotakiwa). Katika Normalising chuma huchoma katika joto husika baada ya forging.

Njia zote hizo na zingine nyingi zinaitwa steel heat treatments. Elimu hii ipo deeper katika "metallurgy".

Sijui Watanzania na Waafrika kwa jumla tumekwama wapi, Mababu zetu wa zamani walikuwa wakitengeneza majembe, visu nk, duni katika zama zao, walichukua Iron ore na kuichoma pamoja na mkaa wa miti migumu kama mpingo nk, na hapo walipata chuma ghafi (pig iron) na baadaye chuma hicho walifukuta na kukifua (forging) kupata vifaa walivyohitaji, kama katika zama za giza za 1800 wazee wetu waliweza vipi zama zetu hizi za Mwanga na maendeleo ya Elimu sisi vitukuu tunashindwa kufukuta hata jembe kutokana na iron ore??, leo wahunzi wetu wanafukuta mashoka, majembe nk, kutokana na Steels kutoka ulaya, mfano utakuta muhunzi anachukua Spring ya gari na kuifukuta kupata panga nk, malighafi zote hizo ni kutoka nje, kifupi tumelemazwa na wazungu kwa kila kitu hadi kifikra.
 
Hayo ni matumizi ya common sense, kuwa huwezi huwezi huwezi huna huna huna. Hata Rais ilimbidi atumie his uncommon sense kuhamia Dodoma kulikomshinda Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete.
 



Hivi ndugu unajua kiwanda cha chuma ni nini??--- na kitu gani kinafanyika humo kupata chuma??

Wazungu wanatuaminisha kwamba kujenga hicho kiwanda ni gharama kubwa na ni impossible lakini Wachina wanasomba tons of Iron ores kisha wanazalisha chuma kisha wanatuletea tena steels na bidhaa za chuma (machineries) kutoka katika hizo ores walizochukua/kupora huku kwetu.

Chuma ndiyo mapinduzi ya mechanizations na wazungu hawataki kamwe sisi waswahili tuzalishe chuma kwasababu tutapata maendeleo na tutaacha kuwategemea wao.
 
Ndo mana mtu akileta hoja nyepesi na dumavu za demand and supply, hatuna technologia, hatuna mitaji, nk. Babu zetu hawakuwaza kivivu namna hii.

Kupanga ni kuchagua lazima tuumie leo kwaajili ya kesho. Kinachoniuma hadi kesho ni kupoteza rasilimali zetu kuhamia Dodoma kwa sababu ambazo zingetatuliwa na uwekezaji kwenye mawasiliano, internet, whatsapp, simu, zoom, nk
 
Tena wachina wanakuwekea chuma kidogo sana kwenye bidhaa zao na kuchakachua na mafibers, plastics na maplastics. Yaani wanatufanya mazezeta. Unanunu gari la kichina lisilodumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…