Mapinduzi makubwa duniani yameletwa na matumizi ya zana za madini ya chuma, ni heri uache vyote ili uchimbe chuma kama unayo

Sijui wewe umekuja na mlengo gani, lakini swali langu ni halali kabisa juu ya bei ya chuma kama 'commodity' inayojitegemea kama ilivyo kahawa, sukari, n.k.

Kama wewe unataka kujua bei za vitu hivyo, sawa. Acha nami niwe huru kuuliza bei ya chuma.
 
Kupanga ni kuchagua, Unaonaje kama pesa ya kujenga majengo, barabara na miundombinu mingine, kuhamisha watumishi, majeshi, nk kuja Dodoma ingetumika kuimarisha mawasiliano ya tehama (telecomfering, e-government, data, usikivu wa Radio na TV ya Taifa, na simu) nchi nzima na chenchi itakayobaki ianze mdogomdogo uchimbaji wa chuma? Mataifa yenye chuma na teknolojia ya chuma ni tishio duniani tangu zama za kale.

Wakati dunia imekuwa kijiji sisi tunaifanya Tanzania iwe dunia kwa kuwaza kuwa watu wengi watakwenda Dodoma (katikati) kwenda kuhudumiwa. Hata kiusalama, siku hizi teknolojia imewezesha Korea Kaskazini itambe kuidungua Marekani ikiwa hukohuko N.Korea bila kulazimika kusogea hata sentimita moja kuelekea Marekani. Vita siku hizi hazipiganwi kwa majambia tena.
 
Chuma kinachanganywa na chuma na sio Nickel inachanganywa na chuma. Nickel inakiboresha chuma. Madini mama kwa viwanda mama duniani ni chuma
 
Ni palepale tu, mawazo yako ni yaleyale ya hatuwezi milele, wakati mwingine taifa makini huwa halifanyi kazi na kupanga mipango kwaajili ya ya kizazi cha leo na faida ya leo, bali linapanga kwaajili ya vizazi vijavyo pia. Unachowaza wewe unawaza kama SACCOS ya kupata faida na mkopo leoleo. Yaani tujenge SGR kwa chuma cha kununua kwa bei kubwa kutoka nje ili tukimbilie kupata faida ya SGR kesho asubuhi badala ya kuendelea kutumia njia zilizopo za usafirishaji ili kujenga uwezo wa kutumia chuma chetu wenyewe kujengea SGR kwa bei nafuu
 
Chuma kinachanganywa na chuma na sio Nickel inachanganywa na chuma. Nickel inakiboresha chuma. Madini mama kwa viwanda mama duniani ni chuma
Huenda sijakuelewa vizuri:

Una maana gani ya "chuma kinachanganywa na chuma"?
Kwa mfano, kutengeneza "stainless Steel" unachanganya chuma gani na chuma gani?

Halafu unasema "nickel inakiboresha chuma"; kwa vipi, kwa sababu katika mstari huohuo umeandika "sio nickel inachanganywa na chuma"; sasa kama haichanganywi na chuma "inakiboresha chuma" vipi?

Nadhani unaweza ukawa katika sekta hii, lakini bado ukawa huna uelewa wa kutosha wa sekta husika.

Kwa mfano mwingine; huu msemo wako wa "Madini mama kwa viwanda mama duniani", sielewi unalenga nini hapa na msemo huu?

Nchi kama yetu hii yenye madini mbalimbali, kama hicho chuma na nickel, sisi tukitaka hatuwezi kufanya madini hayo kuwa viwanda mama kwa kutengeneza mazao yanayotokana na madini hayo na tukafaidika na bidhaa hizo?

Unataka mpaka tuwe 'specialists' tu wa chuma ndio tujue tuna "kiwanda mama"?
 
Ni kuwa na nia tu. Ukiweza kuwa na chuma wewe ni habari nyingine kabisa.
 
Kizazi hiki kimekwama wapi? tumekuwa brain washed kwelikweli. Haba babu zangu walikuwa wanachimba chuma wenyewe na kutengeneza bidhaa kama bunduki za gobore, mitego ya simba na nguruwe, masufuria ya kupikia, majembe, sululu, mapanga, visu vya jikoni na ngaliba, mikuki na mishale ya kuwibdia wanyama na silaha za mapigano, nk. Wakoni walipokuja wakawapiga marufiku na kuwawaweka ndani wasichimbe na kutengeneza vitu hivyo hasa magobore.

Leo hii miaka 60 ya uhuru kuna kijana anasema hatuwezi kuchimba chuma hatuna hela wala tecn... Huu ni msiba sawa na misiba mingine tu. Unaweza usichimbe kama wanavyofanya huko Australia, lakini tunaweza kuchimba kidogo kwaajili ya mashine zetu za kufyatua matofali, chesis za mashine za dona, majembe, visu, nyembe, sindano za kushonea na mapanga ambayo sasa hivi tuna import kwa pesa za kigeni
 
Nikiri tu hapo nimekuchangaya, namaanisha "chuma kinachanywa na nickel"
 
Kaka wanafurahia mabasi ya YOUTONE ya bei rahisi yenye chuma kidogo sana kwakuwa chuma inasafirishwa kutoka Brazil, nk
 
Ni tatizo kubwa sana mkuu. Tuna mind set ya kushindwa. Tuko hovyo kuliko mababu zetu. Mwingine hapo anaangalia bei ya chuma kama chuma na kusahau bidhaa zitokanazo na chuma. Nimewahi kaa kule Ludewa kwenye chuma. Kule kulikuwa na wajapan na wamarekani wanapeleka msaada kila leo. Walikuwa hawakauki ila lengo lao kuu ni kunyemelea chuma. Lakini usishangae sana, kama mtu hajui kuwa nchi hii ina makaa ya mawe ya kutosha unafikiri atajua umuhimu wa chuma!
 
Put it this way economy, finance and investment sio fani yako.

Watu wanapowekeza wanaangalia cost na return zake, maamuzi ya kitaifa allocative efficiency and marginal utility ya uwekezaji.

Hiyo miradi unayoponda ni catalyst ya haraka kwenye kukuza uchumi; hakuna anaekataa chuma ni muhimu ila kwa kufanya uwekezaji huo kwa sasa ni kuchelewesha kasi ya ukuaji ya uchumi.

Kulielezea kwa mapana inataka kuandaa info kadhaa ili upate picha ya kitu gani naongea, unfortunately hii week inachangamoto ya kimajukumu yanayotaka muda wangu.

Like I told you hakuna anaekataa umuhimu wa chuma Ila kwa serikali kuwekeza huko kwa sasa economically sio investment sahihi, labda aje mwekezaji.
 
Unaona ulivyo kilaza.. Chums kinachochea Maendeleo.. Unafikri train, rail, meli n'a vipafaa vya ujenzi vinazalishwa na uchawi
 
Unaona ulivyo kilaza.. Chums kinachochea Maendeleo.. Unafikri train, rail, meli n'a vipafaa vya ujenzi vinazalishwa na uchawi
ndio hatuyataki sasa, tunataka madini yenye thamani, small weight more money.
 
Huezi kuni convince kuwa kununua ndege nyingi kwa mpigo kwa cash ni uwekezaji sahihi kuliko kuichimba na kuichakata chuma chetu japo kwa matumizi yetu na Afrika. Chuma kingetoa ajira kubwa (returns) kwa wachimbaji, wenye smelters, mafundi mchundo wanaotengeneza vikaango vya chapati, na hata kwa wanaofikiria kuunda zana za kilimo na vipuli vya mashine mbalimbali. Leo hii hata bolts, screw na nati tunaagiza. Vijana wanaiba vyuma vya madaraja na alama za barabarani kwenda kuuza kama chuma chakavu kwa watengeneza nondo, misumari na bati. Kuna uwekezaji ambao hauleti faida ya moja kwa moja kwa TRA lakini indirectly unawapa manufaa kwa wananchi, chuma ni moja ya uwekezaji unaotoa both direct and indirect returns.

Hakuna plan ya kuchimba chumba ndio maana hata vyuo na mitaala yetu vyuo haijajikita sana upande huo.
 


Eneo moja wapo litakalofaidika na hili ni ujenzi wa makazi ya watu.

- Hapa tupo nyuma sana, ukianzia mipango miji mpaka ubora wa nyumba zenyewe, hasa ukizingatia mfumo wa kila mmoja ajenge nyumba yake i.e daktari awe mjenzi, mwalimu awe mjenzi, etc ambao una madhara makubwa.

Tunahitaji sana mabati, nondo na cement zenye ubora kwa bei nafuu ili kupunguza gharama za ujenzi.

Nchi ipo ‘underconstruction” , na imezungukwa na na nchi za kariba zinazofanana...alafu tuna madini ya chuma! uhitaji kuwa na Phd kujua nini cha kufanya.
 
Marekani ilihamisha viwanda vyake kwenda Asia nakuiacha Detroit kibakiwa na kiwanda kimoja kikubwa cha Ford tu. Hii ni baada waliokuwa watumwa kuanza kuzidai haki zao za mishahara, afya bora, risk allowances, mazingira, na haki za binadamu. Migomo na vurugu kati ya wenye viwanda na wafanyakazi vilikuwa haviishi kila siku, hivyo matajiri wakafunga migodi ya chuma na makaa na kuhamishia viwanda Asia ambako gharama za uzalishaji ni ndogo, haki za binadamu na mzingira havijaliwi sana na bei ya bidhaa zinaweza kushindana na zile za china, japan na Korea sokoni. Lakini mapinduzi ya viwanda Detroit US yalichangiwa na chuma, makaa ya mawe na watumwa. Ile vita ya dunia Marekani ilikuwa mtengenezaji mkuu wa bidhaa ya chuma kama silaha, ndege, mabomu, meli kubwa na magari na kuwauzia wanaopigana Ulaya. Na hapo ndipo utajiri wa Marekani ulipoanzia.
 
California, USA

Feb 2019 — “In order to keep up with the world of 2050, you will need not merely to invent new ideas and products but above all to reinvent yourself over and over again” writes Dr. Yuval Noah Harari, professor of world history at the Hebrew University of Jerusalem in his latest book, 21 Lessons for the 21 st Century

21 Lessons for the 21st Century | Yuval Noah Harari | Talks at Google

Source : Talks at Google
 
I think even a country has to reinvent itself, for example Buy American is a step to reinventing the country , started by Donald Trump and now Joe Biden is pushing for more on Buy American.


"History is not the study of past. History is the study of change." - Yuval Noah Harari
 
Wamegundua (Marekani) hatua ya kupeleka viwanda nje ya Marekani ni suala lililofanywa kwa pupa bila kuangalia mbele sasa Amerika imeamua kuvirudisha viwanda nyumbani kama siyo kwa bidhaa kutengenezwa kwa 100% Amerika basi bidhaa hiyo ya kiwandani iwe 50 % ya thamani yake kubwa ktk tekenolojia, madini ghafi na ujuzi iwe imetengenezwa ndani ya Marekani na waMarekani wenyewe. Mfano hawataki Marekani itengeneze bodi ya lori ambayo ni thamani ndogo ktk kukamilisha lori wakati vitu vya thamani kubwa kama injini, mfumo wa hydraulic na mifumo ya eletroniki iwe ya kutoka nje ya Marekani.

Kauli mbiu za Make America Great Again ya Donald Trump na Buy American ya Joe Biden zote zinaongea kurudisha viwanda Marekani huko Detroit na kwingineko.
 
Kurudisha viwanda America ni Kazi ngumu sana kwao. Hii itawafanya wamerekani waanze pia kutengeneza bidhaa zenye ubora mdogo ili kushindana na Soko LA bidhaa za China, Korea, Japan, Singapore, Malaysia duniani zenye ubora hafifu.

Kurudisha viwanda nyumbani maana yake wabuni techñolojia mpya ya viwannda visivyochafua mazingira yao.

Leo hii ukienda kwenye malls za marekani hata wazungu wananunua bidhaa za China zaidi kwakuwa zina bei ndogo lakini zinapendeza ingawa hazidumu. Ukiangalia magari ya Ford, chevrolent na Jeep ya sasa sio kama ya zamani kwa uimara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…