Mapinduzi makubwa duniani yameletwa na matumizi ya zana za madini ya chuma, ni heri uache vyote ili uchimbe chuma kama unayo

Mapinduzi makubwa duniani yameletwa na matumizi ya zana za madini ya chuma, ni heri uache vyote ili uchimbe chuma kama unayo

Usiulizie bei ya chuma duniani bali ulizia bei za bidhaa za chuma duniani kama vile nondo, vyuma vya madaraja, mataruma ya reli, makontena, heavy machines kama skaveta, matrekta, combine harvesters, fork lifts, mitambo ya viwanda, bati, meli, malori, nk ni bei gani?
Sijui wewe umekuja na mlengo gani, lakini swali langu ni halali kabisa juu ya bei ya chuma kama 'commodity' inayojitegemea kama ilivyo kahawa, sukari, n.k.

Kama wewe unataka kujua bei za vitu hivyo, sawa. Acha nami niwe huru kuuliza bei ya chuma.
 
Kuamia Dodoma majengo yenyewe ya serikali mengi yana gharama za billioni moja mpaka tatu so far jengo lilichokua hela nyingi ni la uhamiaji pekee na lenyewe alizidi 10 billion.

That’s not the point kusema kitu kinawezekana au la sio swala la theory pia kujua chuma kinavyopatikana.

Unachotakiwa kutuambia ni investments costs zinazohitajika kuchimba chuma ie from primary production kiasi gani cha mchanga kinaitaji kuchotwa kwa siku mashine gani inatumika, transportation mpaka kwenye secondary production train (reli yenyewe ipo au inabidi ijengwe) au tutatumia tipers (ngapi), gharama za mafuta, mishahara yield inayopatikana kwenye secondary production ujue production level zako na kama it’s enough to meet the local demand.

Then uje kwenye gharama za secondary production inayotenganisha mchanga na chuma gharama za icho kiwanda, umeme na kutoka hapo kupeleka kwenye tertiary production inayoweza mould heavy iron for different usage gharama zake, kiwanda size cha size gani ambacho kitaziba pengo la importation.

Njoo walau na hizo data; otherwise kulaumu tu. Watu wengi Tanzania wanaviwanja, mchanga upo, cement ipo, nondo zipo, paa zipo, mafundi wapo; tatizo ni gharama za kukusanya vitu vyote ivyo upate nyumba kulingana na mapato ya wananchi wengi ndio maana wafanyakazi wengi wanaishia kukodi.

Hakuna asiejua faida za chuma kwenye uchumi issue can the government afford to invest in that project at this moment given its constraints and if so will it be economic viable given our current economic status. Hapo ndipo unapotakiwa kushawishi.
Kupanga ni kuchagua, Unaonaje kama pesa ya kujenga majengo, barabara na miundombinu mingine, kuhamisha watumishi, majeshi, nk kuja Dodoma ingetumika kuimarisha mawasiliano ya tehama (telecomfering, e-government, data, usikivu wa Radio na TV ya Taifa, na simu) nchi nzima na chenchi itakayobaki ianze mdogomdogo uchimbaji wa chuma? Mataifa yenye chuma na teknolojia ya chuma ni tishio duniani tangu zama za kale.

Wakati dunia imekuwa kijiji sisi tunaifanya Tanzania iwe dunia kwa kuwaza kuwa watu wengi watakwenda Dodoma (katikati) kwenda kuhudumiwa. Hata kiusalama, siku hizi teknolojia imewezesha Korea Kaskazini itambe kuidungua Marekani ikiwa hukohuko N.Korea bila kulazimika kusogea hata sentimita moja kuelekea Marekani. Vita siku hizi hazipiganwi kwa majambia tena.
 
Mbona nickel hiyo hiyo ikichanganywa na chuma vinatoa vitu vizuri zaidi, au hili hujalifuatilia vizuri?

Kwa sasa tunapoteza mali ghafi yetu nzuri hii kwa kuisafirisha nje kama mali ghafi bila ya kupanga kuitumia pamoja na chuma tulichonacho ili kuongeza thamani zaidi kwa vyote viwili; nickel na chuma.
Chuma kinachanganywa na chuma na sio Nickel inachanganywa na chuma. Nickel inakiboresha chuma. Madini mama kwa viwanda mama duniani ni chuma
 
Hakuna anae kataa umuhimu wa huo uwekezaji alikadhalika hili sio swala la chicken and egg conundrum, which appeared first.

Mwingine anadai kuna wawekezaji walijitokeza as far as I know wachina Mchuchuma walikuwa interested na makaa ya mawe for importation purposes ila sio kujenga kiwanda cha chuma na kama wangekuwa na nia izo sidhani kama wangezuiwa or else leta ushahidi hata wa article.

Having said that ndio maana nikasema nyie watu inabidi muwe realistic mtu anaona article inasema kiwanda cha chuma huko halipo quote vimetumia gharama za $1.3-1.5 billion + uwekezaji wa umeme kwenye icho kiwanda cha Nigeria na ndio kwanza vinauwezo wa kuzalisha tonne 20K kwa mwezi.

Ujenzi wa SGR yote mpaka kuisha ni $3billion dollars mpaka sasa hata nusu atujafika serikali hoi, huyo anaetuambia kila siku tunajenga kwa hela zetu siku hizi anawaambia wachina mtu-kopeshe tumalize mradi wazi wazi.

Halafu nyie mna suggest serikali ingetumia kwanza almost $1.5 billion kujenga reasonable size steeel plant, ikimaliza hapo itafute hela za kujenga SGR huku ikiwa na deni ambalo inabidi itafute vyanzo vingine vya mapato kuligharamia, wakati ikianza kujenga SGR mradi ukiisha unaanza kuwaingizia mapato na kuna direct effects za kuchochea uchumi mahala utakapo pita kuwaongezea mapato mengine ya kodi na kulimudu deni.

Unaanza kutambaa, kusimama na mwisho kutembea and not otherwise; kwa mapato ya sasa we have to prioritise.

Zama za kina Andrew Carnigie watu hela walikuwa wanatengeneza wenyewe wakishirikiana na private kama hakina Morgan Stanley ndio maana ikawa raisi hao watu kufanya hiyo miradi. Hata kesho US wakiingia vitani wana amuru tu central banks zao kuchapa notes, wanunua silaha na kuingia vitani sisi hatuna uwezo huo.

South Africa one of biggest producers wa iron ore kashindwa tengeneza icho kiwanda cha kuhudumia soko la Africa iwe sisi kwa hali yetu ya sasa.

Sisemi atukihitaji hiko kiwanda ila kwa uchumi wetu wa sasa hizo hela can yield better return in other investments to propel growth for now; huko mbele sawa.
Ni palepale tu, mawazo yako ni yaleyale ya hatuwezi milele, wakati mwingine taifa makini huwa halifanyi kazi na kupanga mipango kwaajili ya ya kizazi cha leo na faida ya leo, bali linapanga kwaajili ya vizazi vijavyo pia. Unachowaza wewe unawaza kama SACCOS ya kupata faida na mkopo leoleo. Yaani tujenge SGR kwa chuma cha kununua kwa bei kubwa kutoka nje ili tukimbilie kupata faida ya SGR kesho asubuhi badala ya kuendelea kutumia njia zilizopo za usafirishaji ili kujenga uwezo wa kutumia chuma chetu wenyewe kujengea SGR kwa bei nafuu
 
Chuma kinachanganywa na chuma na sio Nickel inachanganywa na chuma. Nickel inakiboresha chuma. Madini mama kwa viwanda mama duniani ni chuma
Huenda sijakuelewa vizuri:

Una maana gani ya "chuma kinachanganywa na chuma"?
Kwa mfano, kutengeneza "stainless Steel" unachanganya chuma gani na chuma gani?

Halafu unasema "nickel inakiboresha chuma"; kwa vipi, kwa sababu katika mstari huohuo umeandika "sio nickel inachanganywa na chuma"; sasa kama haichanganywi na chuma "inakiboresha chuma" vipi?

Nadhani unaweza ukawa katika sekta hii, lakini bado ukawa huna uelewa wa kutosha wa sekta husika.

Kwa mfano mwingine; huu msemo wako wa "Madini mama kwa viwanda mama duniani", sielewi unalenga nini hapa na msemo huu?

Nchi kama yetu hii yenye madini mbalimbali, kama hicho chuma na nickel, sisi tukitaka hatuwezi kufanya madini hayo kuwa viwanda mama kwa kutengeneza mazao yanayotokana na madini hayo na tukafaidika na bidhaa hizo?

Unataka mpaka tuwe 'specialists' tu wa chuma ndio tujue tuna "kiwanda mama"?
 
Lakini kumbuka ukifanya huo mradi ni game changer, yaan ukiacha kuwekeza kwenye madaraja na kuwekeza kwenye miradi mingi ambayo haizalishi na sio ya kimkakati kama ile ya Chatle.
Ukaamua kuwekeza kwenye kiwanda cha chuma nadhani baadq ya miaka 10 tungeanza kuwa watu wengine kabisa.


Ni kuwa na nia tu. Ukiweza kuwa na chuma wewe ni habari nyingine kabisa.
 
Sijaweka ushabiki wa kisiasa hapa. Miradi kama hii ambayo inaweza geuza kabisa uchumi wa nchi huwa inapata upinzani mwingi sana. Niliandika kwenye jukwaa la great thinkers jinsi US ilivyomzuia mjapan kumuuzia Korea Kaskazini kinu cha kufua chuma. Alijua umuhimu wa chuma kwa nchi.

Hapa kwetu mtu anaweza pinga kwa ajenda mbalimbali. Labda ni mkenya hataki Tanzania iwe na chuma, Labda ni msauzi anaogopa upinzani sokoni nk. Wazo la ubishani wa kisiasa halikuwepo kabisa.

Chuma hata usikiingize kwenye kucompare na uwekezaji mwingine kwenye ishu za opportunity cost. Chuma ni kama elimu, hospitali, barabara, madaraja na vitu vingine vya msingi kwa nchi. Hii siyo bidhaa tu ya kuuza na kununua, ni kitu cha msingi kama elimu na afya. Inatakiwa kufanya kila njia kuwa nayo.

Unafikiri kwanini wachina wako tayari kutoa Ore Njombe, kusafirisha mpaka Mtwara kupakia kwenye meli mpaka uchina? Unafikiri imeweza kuwa mzalishaji namba moja duniani kihivihivi?. Kama yeye ameweza kusafirisha chuma toka Brazil, SA na Australia na anaona kuna faida, sisi tunashindwa nini kuchimba na kusafisha hapo hapo?
Kizazi hiki kimekwama wapi? tumekuwa brain washed kwelikweli. Haba babu zangu walikuwa wanachimba chuma wenyewe na kutengeneza bidhaa kama bunduki za gobore, mitego ya simba na nguruwe, masufuria ya kupikia, majembe, sululu, mapanga, visu vya jikoni na ngaliba, mikuki na mishale ya kuwibdia wanyama na silaha za mapigano, nk. Wakoni walipokuja wakawapiga marufiku na kuwawaweka ndani wasichimbe na kutengeneza vitu hivyo hasa magobore.

Leo hii miaka 60 ya uhuru kuna kijana anasema hatuwezi kuchimba chuma hatuna hela wala tecn... Huu ni msiba sawa na misiba mingine tu. Unaweza usichimbe kama wanavyofanya huko Australia, lakini tunaweza kuchimba kidogo kwaajili ya mashine zetu za kufyatua matofali, chesis za mashine za dona, majembe, visu, nyembe, sindano za kushonea na mapanga ambayo sasa hivi tuna import kwa pesa za kigeni
 
Huenda sijakuelewa vizuri:

Una maana gani ya "chuma kinachanganywa na chuma"?
Kwa mfano, kutengeneza "stainless Steel" unachanganya chuma gani na chuma gani?

Halafu unasema "nickel inakiboresha chuma"; kwa vipi, kwa sababu katika mstari huohuo umeandika "sio nickel inachanganywa na chuma"; sasa kama haichanganywi na chuma "inakiboresha chuma" vipi?

Nadhani unaweza ukawa katika sekta hii, lakini bado ukawa huna uelewa wa kutosha wa sekta husika.

Kwa mfano mwingine; huu msemo wako wa "Madini mama kwa viwanda mama duniani", sielewi unalenga nini hapa na msemo huu?

Nchi kama yetu hii yenye madini mbalimbali, kama hicho chuma na nickel, sisi tukitaka hatuwezi kufanya madini hayo kuwa viwanda mama kwa kutengeneza mazao yanayotokana na madini hayo na tukafaidika na bidhaa hizo?

Unataka mpaka tuwe 'specialists' tu wa chuma ndio tujue tuna "kiwanda mama"?
Nikiri tu hapo nimekuchangaya, namaanisha "chuma kinachanywa na nickel"
 
Unaposema kuwa kuchimba chuma ni gharama na kunahitaji teknolojia kubwa unatakiwa kuanisha siyo kusema maneno matupu. Ndiyo nyie mnakubaliana na hali ya sisi kuuza ngozi Italy na kisha waitaliano kuja kutuuzia viatu, mikanda na Wallet. Mnasema kutengeneza viatu ni gharama, kunahitaji teknolojia kubwa, inahitaji ujuzi!.

Zamani mlikuwa na uzembe huu wa kusema kuchenjua dhahabu kuna gharama kubwa, mkawa mnasafirisha mchanga dhahabu. Kumbe ni ujinga tu, leo watu wana vielution vya kuchenjua dhahabu kila kona na wanapiga pesa nyingi tu tulizokuwa tunapoteza. Unafikiri kwanini wachina wanatoa madini ya chuma Brazil, wanaenda kwao kufua na kuja kutuuzia kwa faida?
Kaka wanafurahia mabasi ya YOUTONE ya bei rahisi yenye chuma kidogo sana kwakuwa chuma inasafirishwa kutoka Brazil, nk
 
Kizazi hiki kimekwama wapi? tumekuwa brain washed kwelikweli. Haba babu zangu walikuwa wanachimba chuma wenyewe na kutengeneza bidhaa kama bunduki za gobore, mitego ya simba na nguruwe, masufuria ya kupikia, majembe, sululu, mapanga, visu vya jikoni na ngaliba, mikuki na mishale ya kuwibdia wanyama na silaha za mapigano, nk. Wakoni walipokuja wakawapiga marufiku na kuwawaweka ndani wasichimbe na kutengeneza vitu hivyo hasa magobore.

Leo hii miaka 60 ya uhuru kuna kijana anasema hatuwezi kuchimba chuma hatuna hela wala tecn... Huu ni msiba sawa na misiba mingine tu. Unaweza usichimbe kama wanavyofanya huko Australia, lakini tunaweza kuchimba kidogo kwaajili ya mashine zetu za kufyatua matofali, chesis za mashine za dona, majembe, visu, nyembe, sindano za kushonea na mapanga ambayo sasa hivi tuna import kwa pesa za kigeni
Ni tatizo kubwa sana mkuu. Tuna mind set ya kushindwa. Tuko hovyo kuliko mababu zetu. Mwingine hapo anaangalia bei ya chuma kama chuma na kusahau bidhaa zitokanazo na chuma. Nimewahi kaa kule Ludewa kwenye chuma. Kule kulikuwa na wajapan na wamarekani wanapeleka msaada kila leo. Walikuwa hawakauki ila lengo lao kuu ni kunyemelea chuma. Lakini usishangae sana, kama mtu hajui kuwa nchi hii ina makaa ya mawe ya kutosha unafikiri atajua umuhimu wa chuma!
 
Kupanga ni kuchagua, Unaonaje kama pesa ya kujenga majengo, barabara na miundombinu mingine, kuhamisha watumishi, majeshi, nk kuja Dodoma ingetumika kuimarisha mawasiliano ya tehama (telecomfering, e-government, data, usikivu wa Radio na TV ya Taifa, na simu) nchi nzima na chenchi itakayobaki ianze mdogomdogo uchimbaji wa chuma? Mataifa yenye chuma na teknolojia ya chuma ni tishio duniani tangu zama za kale.

Wakati dunia imekuwa kijiji sisi tunaifanya Tanzania iwe dunia kwa kuwaza kuwa watu wengi watakwenda Dodoma (katikati) kwenda kuhudumiwa. Hata kiusalama, siku hizi teknolojia imewezesha Korea Kaskazini itambe kuidungua Marekani ikiwa hukohuko N.Korea bila kulazimika kusogea hata sentimita moja kuelekea Marekani. Vita siku hizi hazipiganwi kwa majambia tena.
Put it this way economy, finance and investment sio fani yako.

Watu wanapowekeza wanaangalia cost na return zake, maamuzi ya kitaifa allocative efficiency and marginal utility ya uwekezaji.

Hiyo miradi unayoponda ni catalyst ya haraka kwenye kukuza uchumi; hakuna anaekataa chuma ni muhimu ila kwa kufanya uwekezaji huo kwa sasa ni kuchelewesha kasi ya ukuaji ya uchumi.

Kulielezea kwa mapana inataka kuandaa info kadhaa ili upate picha ya kitu gani naongea, unfortunately hii week inachangamoto ya kimajukumu yanayotaka muda wangu.

Like I told you hakuna anaekataa umuhimu wa chuma Ila kwa serikali kuwekeza huko kwa sasa economically sio investment sahihi, labda aje mwekezaji.
 
Wewe ndio kilaza unayetaka hayo madini yasiyo na thamani duniani. Unabeba mikontena ya vyuma na makaa ya mawe alafu pesa unayolipwa ni ya kilo 3 za dhahabu au Tanzanite sii ujinga huo. Storage yenyewe ni shida. Wakati dhahabu ya mabilioni unaficha kwenye kabegi ka lucky Dube alafu unasepa zako dadeki.
Unaona ulivyo kilaza.. Chums kinachochea Maendeleo.. Unafikri train, rail, meli n'a vipafaa vya ujenzi vinazalishwa na uchawi
 
Unaona ulivyo kilaza.. Chums kinachochea Maendeleo.. Unafikri train, rail, meli n'a vipafaa vya ujenzi vinazalishwa na uchawi
ndio hatuyataki sasa, tunataka madini yenye thamani, small weight more money.
 
Put it this way economy, finance and investment sio fani yako.

Watu wanapowekeza wanaangalia cost na return zake, maamuzi ya kitaifa allocative efficiency and marginal utility ya uwekezaji.

Hiyo miradi unayoponda ni catalyst ya haraka kwenye kukuza uchumi; hakuna anaekataa chuma ni muhimu ila kwa kufanya uwekezaji huo kwa sasa ni kuchelewesha kasi ya ukuaji ya uchumi.

Kulielezea kwa mapana inataka kuandaa info kadhaa ili upate picha ya kitu gani naongea, unfortunately hii week inachangamoto ya kimajukumu yanayotaka muda wangu.

Like I told you hakuna anaekataa umuhimu wa chuma Ila kwa serikali kuwekeza huko kwa sasa economically sio investment sahihi, labda aje mwekezaji.
Huezi kuni convince kuwa kununua ndege nyingi kwa mpigo kwa cash ni uwekezaji sahihi kuliko kuichimba na kuichakata chuma chetu japo kwa matumizi yetu na Afrika. Chuma kingetoa ajira kubwa (returns) kwa wachimbaji, wenye smelters, mafundi mchundo wanaotengeneza vikaango vya chapati, na hata kwa wanaofikiria kuunda zana za kilimo na vipuli vya mashine mbalimbali. Leo hii hata bolts, screw na nati tunaagiza. Vijana wanaiba vyuma vya madaraja na alama za barabarani kwenda kuuza kama chuma chakavu kwa watengeneza nondo, misumari na bati. Kuna uwekezaji ambao hauleti faida ya moja kwa moja kwa TRA lakini indirectly unawapa manufaa kwa wananchi, chuma ni moja ya uwekezaji unaotoa both direct and indirect returns.

Hakuna plan ya kuchimba chumba ndio maana hata vyuo na mitaala yetu vyuo haijajikita sana upande huo.
 
Chuma ndio madini mama duniani, mapinduzi makubwa duniani yameletwa na matumizi ya zana za madini ya chuma, ni heri uache vyote ili uchimbe chuma kama unayo. Tena huna haja ya kutafuta mwekezaji kwenye madini ya chuma chimba mwenyewe.

Taifa lengo malengo litachimba chuma kwanza hata kabla ya dhahabu na nickel. Yaani kwa umuhimu itaanza chuma na kufuatiwa na makaa ya wawe, shaba, bati na dhahabu.

Chuma ndiyo itatumika kutengenezea zana kuchimbia madini mengine na njia za kusafirisha madini mengine.


Eneo moja wapo litakalofaidika na hili ni ujenzi wa makazi ya watu.

- Hapa tupo nyuma sana, ukianzia mipango miji mpaka ubora wa nyumba zenyewe, hasa ukizingatia mfumo wa kila mmoja ajenge nyumba yake i.e daktari awe mjenzi, mwalimu awe mjenzi, etc ambao una madhara makubwa.

Tunahitaji sana mabati, nondo na cement zenye ubora kwa bei nafuu ili kupunguza gharama za ujenzi.

Nchi ipo ‘underconstruction” , na imezungukwa na na nchi za kariba zinazofanana...alafu tuna madini ya chuma! uhitaji kuwa na Phd kujua nini cha kufanya.
 
Hakuna anaesema tuanze kama China alivyo leo. Tunaanza chini. Unaangalia mahitaji ya nchi kwa mwaka na kuanza na kiwango hicho. Unaendelea kupanua kulingana na soko. Unaanza na vitu basic. Hivyo vyuma sijui vya kwenye oil rigs ni mambo ya baadaye. Tunaanza na chuma cha kufaa reli, nondo, nut, bolt, baiskeli, shoka, jembe, nk. Vitu basic. Marekani hawazalishi sababu ya gharama kubwa za mishahara na mambo ya mazingira. SA wana chuma cha kuwafaa wao na kuexport pia. Kila nchi ina hali na changamoto zake. Siyo sababu Marekani hawachimbi chao basi na kwetu haitawezekana.

Ni ngumu nchi kuendelea bila chuma, kama tu ilivyo ngumu kuendelea bila elimu au afya. China angekuwa na mentality kama yako asingefika alipofika leo.
Marekani ilihamisha viwanda vyake kwenda Asia nakuiacha Detroit kibakiwa na kiwanda kimoja kikubwa cha Ford tu. Hii ni baada waliokuwa watumwa kuanza kuzidai haki zao za mishahara, afya bora, risk allowances, mazingira, na haki za binadamu. Migomo na vurugu kati ya wenye viwanda na wafanyakazi vilikuwa haviishi kila siku, hivyo matajiri wakafunga migodi ya chuma na makaa na kuhamishia viwanda Asia ambako gharama za uzalishaji ni ndogo, haki za binadamu na mzingira havijaliwi sana na bei ya bidhaa zinaweza kushindana na zile za china, japan na Korea sokoni. Lakini mapinduzi ya viwanda Detroit US yalichangiwa na chuma, makaa ya mawe na watumwa. Ile vita ya dunia Marekani ilikuwa mtengenezaji mkuu wa bidhaa ya chuma kama silaha, ndege, mabomu, meli kubwa na magari na kuwauzia wanaopigana Ulaya. Na hapo ndipo utajiri wa Marekani ulipoanzia.
 
California, USA

Feb 2019 — “In order to keep up with the world of 2050, you will need not merely to invent new ideas and products but above all to reinvent yourself over and over again” writes Dr. Yuval Noah Harari, professor of world history at the Hebrew University of Jerusalem in his latest book, 21 Lessons for the 21 st Century

21 Lessons for the 21st Century | Yuval Noah Harari | Talks at Google


Source : Talks at Google
 
I think even a country has to reinvent itself, for example Buy American is a step to reinventing the country , started by Donald Trump and now Joe Biden is pushing for more on Buy American.

25 January 2021

Joe Biden atangaza mpango kabambe wa kufufua viwanda mama, kusaini waraka wa dharura kuinusuru Marekani


Rais wa 46 wa USA Joe Biden ameapa kuhakikisha kuwa viwanda vya vyuma, aliminium, glasi, viwanda vya tekenolojia ya kisasa kama biotekinoloji n.k vinabaki Amerika huku malighafi / mashine/ utaalamu pia uwe wa kutoka ndani ya Marekani na serikali yake (Joe Biden) kuwa mkali zaidi ya Donald Trump kisera kuhusu "Marekani Kwanza" kwa kuhakikisha kila kitu kinazalishwa ndani ya Amerika na kuwa atasaini waraka wa dharura (executive order/decree) mapema kutimiza ndoto hiyo ya "Amerika Kwanza".

Rais Joe Biden anasisitiza sera ya "Marekani Kwanza" ni hakikisho la kuwa Marekani inabaki kuwa na viwanda mama, viwanda vidogo, vyuo vikuu vitakavyo fanya tafiti zitumike ktk sekta za viwanda / kilimo/ Afya vya Marekani, uchumi mkubwa, ajira nyingi za ndani na usalama ktk kandarasi za kijeshi na vifaa tiba madawa, chanjo afya za waMarekani.

Serikali yake imeunda Kurugenzi Maalum itakayokuwa chini ya Ofisi ya Rais kuhakikisha kandarasi zote zinakwenda kwa waMarekani. Pia itakuwa lazima Kurugenzi hiyo kutangaza kwa umma fursa hizo za kandarasi na uzalishaji ktk vyombo vya habari ili kuhakikisha Kurugenzi hiyo haiwapiti waMarekani kwa bahati mbaya.

Maana serikali haifahamu kila kitu hivyo "Uwazi" kupitia taarifa kwa umma anaweza kutokeza Mmarekani akasema anaweza kuifanya kazi hiyo kabla ya makampuni ya kigeni kupewa fursa hiyo pia kutakuwepo mfuko maalum kuwasaidia waMarekani wenye makampuni yenye ujuzi lakini wenye mtaji mdogo kuweza kuchukua kazi za kandarasi kubwa ili waMarekani wafaidike kwanza.

Biden gives remarks on strengthening American manufacturing
Source : PBS NewsHour

January 25, 2021

Biden signs ‘Buy American’ order​

WASHINGTON (AP) — President Joe Biden signed an executive order Monday to boost government buying from U.S. manufacturers, as talks with Congress over a $1.9 trillion stimulus package that he considers essential to the nation's recovery showed few signs of progress.

Watch Biden's remarks in the player above.

The executive order is among a flurry of moves by Biden during his first full week to publicly show he's taking swift action to heal an ailing economy. Biden reiterated Monday that he believes the country is in a precarious spot and and that relief is urgently needed, even as he dismissed the possibility of embracing a scaled-down bill to secure passage faster. Among the features of the stimulus plan are a national vaccination program, aid to reopen schools, direct payments of $1,400 to individuals and financial relief for state and local governments.

"Time is of the essence," Biden said. "I am reluctant to cherry-pick and take out one or two items here."

Biden, meanwhile, was growing more bullish on vaccine distribution in the U.S., after he and his aides face criticism for their caution in setting vaccination targets for the virus-weary nation. Biden told reporters that he believes 150 million shots in arms may be achievable in his first 100 days in office — up from 100 million doses — and that he expects widespread availability of the vaccines for Americans by spring, with the U.S. "well on our way to herd immunity" by summer.

Biden's comments come after his team held a call Sunday to outline the stimulus plan with at least a dozen senators, while the president has also privately talked with lawmakers.

"There's an urgency to moving it forward, and he certainly believes there has to be progress in the next couple of weeks," White House press secretary Jen Psaki said Monday. She warned that action needed to be taken before the U.S. reaches an "unemployment cliff" in March, when long-term unemployment benefits expire for millions of Americans.

But Republicans on Capitol Hill were not joining in the push for immediate action.

One key Republican, Sen. Susan Collins of Maine, said after Sunday's call that "it seems premature to be considering a package of this size and scope." Collins described the additional funding for vaccinations as useful while cautioning that any economic aid should be more targeted.

Senate Minority Leader Mitch McConnell, R-Ky., said Monday that "any further action should be smart and targeted, not just an imprecise deluge of borrowed money that would direct huge sums toward those who don't need it."

Biden sought to downplay the rhetoric from GOP lawmakers, saying, "I have been doing legislative negotiations for a large part of my life. I know how the system works."

"This is just the process beginning," he added. "No one wants to give up on their position until there's no other alternative."

Monday's order will likely take 45 days or longer to make its way through the federal bureaucracy, during which time wrangling with Congress could produce a new aid package. That would be a follow-up to the roughly $4 trillion previously approved to tackle the economic and medical fallout from the coronavirus.

The order was aimed at increasing factory jobs, which have slumped by 540,000 since the pandemic began last year.

"America can't sit on the sidelines in the race for the future," Biden said before signing the order in the Eisenhower Executive Office Building. "We're ready, despite all we're facing."

Biden's order would modify the rules for the Buy American program, making it harder for contractors to qualify for a waiver and sell foreign-made goods to federal agencies. It also changes rules so that more of a manufactured good's components must originate from U.S. factories. America-made goods would also be protected by an increase in the government's threshold and price preferences, the difference in price over which the government can buy a foreign product.

It's an order that channels Biden's own blue-collar persona and his promise to use the government's market power to support its industrial base, an initiative that former President Donald Trump also attempted with executive actions and import taxes.

"Thanks to past presidents granting a trade-pact waiver to Buy American, today billions in U.S. tax dollars leak offshore every year because the goods and companies from 60 other countries are treated like they are American for government procurement purposes," said Lori Wallach, director of Public Citizen's Global Trade Watch and a critic of past trade agreements.

While Trump also issued a series of executive actions and tariffs with the goal of boosting manufacturing, he didn't attempt to rewrite the guidance for what constitutes a U.S.-made component or tighten the process for granting exemptions to buy foreign goods, a key difference from Biden's agenda, Biden's administration said.

The order also has elements that apply to the separate Buy America program that applies to highways and bridges. It aims to open up government procurement contracts to new companies by scouting potential contractors. The order would create a public website for companies that received waivers to sell foreign goods to the government, so that U.S. manufacturers can have more information and be in a more competitive position.

Past presidents have promised to revitalize manufacturing as a source of job growth and achieved mixed results. The government helped save the automotive sector after the 2008 financial crisis, but the number of factory jobs has been steadily shrinking over the course of four decades.

The number of U.S. manufacturing jobs peaked in 1979 at 19.5 million and now totals 12.3 million, according to the Labor Department
Source : WATCH: Biden signs 'Buy American' order, pushes for urgent COVID-19 relief


"History is not the study of past. History is the study of change." - Yuval Noah Harari
 
Marekani ilihamisha viwanda vyake kwenda Asia nakuiacha Detroit kibakiwa na kiwanda kimoja kikubwa cha Ford tu. Hii ni baada waliokuwa watumwa kuanza kuzidai haki zao za mishahara, afya bora, risk allowances, mazingira, na haki za binadamu. Migomo na vurugu kati ya wenye viwanda na wafanyakazi vilikuwa haviishi kila siku, hivyo matajiri wakafunga migodi ya chuma na makaa na kuhamishia viwanda Asia ambako gharama za uzalishaji ni ndogo, haki za binadamu na mzingira havijaliwi sana na bei ya bidhaa zinaweza kushinda na zile za china, japan na Korea sokoni. Lakini mapinduzi ya viwanda Detroit US yalichangiwa na chuma, makaa ya mawe na watumwa. Ile vita ya dunia Marekani ilikuwa mtengenezaji mkuu wa bidhaa ya chuma kama silaha, ndege, mabomu, meli kubwa na magari na kuwauzia wanaopigana Ulaya. Na hapo ndipo utajiri wa Marekani ulipoanzia.
Wamegundua (Marekani) hatua ya kupeleka viwanda nje ya Marekani ni suala lililofanywa kwa pupa bila kuangalia mbele sasa Amerika imeamua kuvirudisha viwanda nyumbani kama siyo kwa bidhaa kutengenezwa kwa 100% Amerika basi bidhaa hiyo ya kiwandani iwe 50 % ya thamani yake kubwa ktk tekenolojia, madini ghafi na ujuzi iwe imetengenezwa ndani ya Marekani na waMarekani wenyewe. Mfano hawataki Marekani itengeneze bodi ya lori ambayo ni thamani ndogo ktk kukamilisha lori wakati vitu vya thamani kubwa kama injini, mfumo wa hydraulic na mifumo ya eletroniki iwe ya kutoka nje ya Marekani.

Kauli mbiu za Make America Great Again ya Donald Trump na Buy American ya Joe Biden zote zinaongea kurudisha viwanda Marekani huko Detroit na kwingineko.
 
Wamegundua (Marekani) hatua ya kupeleka viwanda nje ya Marekani ni suala lililofanywa kwa pupa bila kuangalia mbele sasa Amerika imeamua kuvirudisha viwanda nyumbani kama siyo kwa bidhaa kutengenezwa kwa 100% Amerika basi bidhaa hiyo ya kiwandani iwe 50 % ya thamani yake kubwa ktk tekenolojia, madini ghafi na ujuzi iwe imetengenezwa ndani ya Marekani na waMarekani wenyewe. Mfano hawataki Marekani itengeneze bodi ya lori ambayo ni thamani ndogo ktk kukamilisha lori wakati vitu vya thamani kubwa kama injini, mfumo wa hydraulic na mifumo ya eletroniki iwe ya kutoka nje ya Marekani.

Kauli mbiu za Make America Great Again ya Donald Trump na Buy American ya Joe Biden zote zinaongea kurudisha viwanda Marekani huko Detroit na kwingineko.
Kurudisha viwanda America ni Kazi ngumu sana kwao. Hii itawafanya wamerekani waanze pia kutengeneza bidhaa zenye ubora mdogo ili kushindana na Soko LA bidhaa za China, Korea, Japan, Singapore, Malaysia duniani zenye ubora hafifu.

Kurudisha viwanda nyumbani maana yake wabuni techñolojia mpya ya viwannda visivyochafua mazingira yao.

Leo hii ukienda kwenye malls za marekani hata wazungu wananunua bidhaa za China zaidi kwakuwa zina bei ndogo lakini zinapendeza ingawa hazidumu. Ukiangalia magari ya Ford, chevrolent na Jeep ya sasa sio kama ya zamani kwa uimara.
 
Back
Top Bottom