Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Upinzani mkali uliotokea ndani ya maseneti ya Nigeria na miongoni mwa wananchi imetajwa ni sababu kuu zilizopelekea muda uliotolewa kama ukomo wa kurudishwa Rais Bazoum wa Niger madarakani kupita bila kutokea chochote.
Raisi Bola Tinubu ambaye ni mwenyekiti wa sasa wa ECOWAS amelaumiwa kwa kutoa tamko la vitisho mapema kwa watawala wa kijeshi wa Niger hata baada ya kupata idhini kutoka kwa mabaraza hayo na kabla ya kushauriana kikamilifu na viongozi wengine wa ECOWAS.
Lawama nyengine dhidi yake ni kwa kule kutofikiria athari za ndani iwapo uingiliaji wa kijeshi huo utafanyika.
Amelaumiwa pia kutaka kuchukua hatua kali za kuyaridhisha mataifa ya nje kabla kufikiria hasara zitakazopatikana kwa ukanda mzima Afrika Magharibi.
Kitendo cha kuikatia Niger na kuiingiza nchi hiyo gizani kilifanyika kinyume na makubaliano yaliyofanyika katika ujenzi wa bwawa la umeme kwenye mto Niger.
Upande wa wananchi wameonekana kutokubaliana kabisa na uamuzi wa kuingilia kijeshi Niger wakiiona nchi hiyo kama ni ndugu wa karibu sana huku idadi kubwa ya watu wa Nigeria wakiwa na asili ya Niger na kinyume chake.
Niger kabla ya mgawanyo wa mipaka wa wakoloni hapo mwaka 1884 ilikuwa ni mwendelezo wa utawala mmoja na Nigeria.
Hii si mara ya mwanzo kwa kiongozi huyo kuchukua maamuzi ya haraka haraka na ya kipekee.Mara alipoingia madarakani alitoa tangazo la kusitisha ruzuku ya mafuta kwa wananchi jambo lillilopelekea machafuko makubwa nchini kote.