Mapinduzi ya Niger yanaweza kumkumba Tinubu wa Nigeria

Hii ni mara ya 5 kutokea mapinduzi ya kijeshi Niger
Mbali na kuioindua serikali hata wajeda wao kwa wao imeishatokea

Hawa west Africa wana mitihani kujaribu kuweka maisha mazuri kwa wananchi wao ila bado hawajapata njia sahihi

Wao wanaona vita tu na mapinduzi ndio sahihi
Wamepinduana x 5 huoni wana matatizo hao

Zee la Nigeria ni mfanyabiashara mkubwa anaangalia maslahi tu
 
Neno Uzalendo, Kibaraka na Propaganda linatumika vibaya sana currently.
Unaweza msakama kiongozi yoyote kwa hila zako binafsi kwa kutumia moja ya Majina hayo ili kupata uungwaji.
Mapinduzi ya Niger ni full ukabila
Na Tinubu Kukataliwa na maseneta ni ukabila huo huo. Hausa wanaona kupeleka jeshi Niger ni kwenda kuua ndugu wa kabila lao.
 
Mimi naamini baada ya mapinduzi Niger , kuna nchi nyingine inafuata. Time will tell.
 
Mtoa mada ya udini uwezo wake wa kufikiri na kudadavua mambo ni mdogo sana. Mpuuze. Anatakiwa awe msomaji.
 
Hii sentensi ya mwisho imenichekesha sana.
Kaka hii Africa inakwamishwa sana na wanasiasa wetu hawa.

Kama ukombozi wa Bara hili ulifanywa na vijana hadi wengine wakazeeka ndio wanakuja kupewa mamlaka waliyopambania.

Basi hii inaonesha ni namna gani kijana anavyoweza kubadili hali mbaya na kuwa nzuri akiamua.

Sasa hivi kuna wimbi la wazee wetu kuona vijana ni watu wasiofaa kupewa madaraka makubwa.Hii sio haki.

Ni muda wa vijana kupewa nafasi ya kupambania maisha ya bara hili maisha ya Taifa hili.Hawa wanasiasa ambao umri umeenda sana hawana cha kupoteza wanaona hata wakifa leo kwao ni sawa tu.

Hawa vijana wenzetu hata wakifanya ujinga kuna wakati watafikiria na umri wao na namna watakavyopata shida wakiwa vijana.

Hivi unadhani mtu mwenye miaka 60 au zaidi hata mkimpa adhabu ya kunyongwa jamii itasikitika sana kama vile kijana wa chini ya miaka 40 akipewa hyo adhabu.
 
Hakuna mchambuzi yeyote Duniani aliewahi kufikiria kuwa vita ya Ukraine na Russia itaipasua vipande vipande jumuiya ya kiuchumi ya Afrika Magharibi
Inategemea na upeo wako na platforms zako mkuu.
Usi seal hilo jambo kwa namna hiyo kwa sababu tu wewe hukuona
 
ndo tunautaka maana bila hivyo africa iliyo bora tuisikia kwenye vitabu. Viongozi wengi hawana maamuzi sababu ya blanda iliyofanyika huko nyuma.
Wewe unataraji wimbi la mapinduzi lina uwezo wowote wa kumuweka huru Mwafrika?
Tulishasema humu kuwa Waafrika wanalalamika sana wakidhani wanaonewa. Hii hata kwa wazungu miongoni mwao wanafanyiana hivyo.

Angalia vizuri sababu za BREXIT ndiyo utajua. Jinsi Mfaransa alivyokua akiongea shits kwa Uingereza alivyoamua ku EXIT unadhani Uingereza angemuacha hivihivi? Maana haya ya uholela wa kuruhusu Wahamiaji ulifanywa zaidi na kupigiwa chapuo na Ufaransa akijua dream destination ya Wahamiaji wengi ni Uingereza ndiyo maana Uingereza alianza kuigomea Shengen Visa.
Pia walippamua kuanzisha sarafu ya Euro, France ndiye alikua front na German, german faster akaiua Deutsche mark, na France akaitosa French franc, hawakuupenda utawala British pound wakataka wasawazishe nguvu kwa kutengeneza currency moja.
Uingereza akaona ni ufala maana mambo mengi kuanzia production, employment, history and pride yanaenda kuiathari yenyewe moja kwaja Moja. Ndipo akaja na BREXIT.
Hivyo hata wao wazungu wanawindana sana, ni swala la muda tu kuja kuona hata hayo Mapinduzi ya West Afrika hata Russia anatembelea nyota tu.
Kwa sasa tutulie tu na kuendelea kufuatilia.
 
nimekupata mkuu mimi nauthika mno na the way hizi nchi zetu za kiafrica zinavyoendeshwa.
 
Huyu babu hana uzoefu wa kijeshi.Hajui athari za vita vya wenyewe kwa wenyewe au kwa uzee wake amesahau tu.
Tinubu.ha ha ha huyu ni joe Biden wa Afrika ,anafanana kimatendo na umri.
Ingawa natania lkn inaelekea hukohuko.😀😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…