TANZANIA YA VIWANDA
Kumekua na sera nzuri sana katika nchi ya Tanzania ambayo ina mtazamo chanya unaoweza kubadili taswira na ramani yote ya kiuchimi ulio dhalili na kua nchi yenye mafanikio kiuchumi. Sera hiyo ni ile iliyoletwa na rais wa awamu ya tano Dr john Magufuli ambayo inaeleza na kusisitiza mageuzi ya uchumi wa Tanzania kuwa Tanzania ya viwanda.
Tanzania ya viwanda maana yake ni kutengeneza na kuimarisha uchumi wa Tanzania kutegemea viwanda kwa kiasi kikubwa. Kutokana na kile kilichothibitika na kusemwa kwamba nchi zote zilizoendelea zinatemea viwanda kwa kiasi kikubwa kwan viwanda vimekua ni tegemezi katika dunia ya leo.
Tanzania imekua miongoni mwa mataifa makubwa barani Afrika ambayo inazalisha malighafi zitumikazo kutengeneza bidhaa nyingi zenye thamani. Malighafi hizo huzalishwa nchini Tanzania na kuuzwa kunako mataifa ya mbali ya kigeni yanayosadikika kuwa yameendelea au yamepiga hatua kubwa kiuchumi.
Mataifa yaliyoendelea hununua malighafi kutoka mataifa duni ya Kiafrika kisha kutengeneza bidhaa na baadaye kutuuzia tena kwa bei kubwa.
Kutokana na huu mzunguko husababisha mataifa mengi ya Afrika kupoteza fedha nyingi za kigeni na kuwanufaisha watu wa mataifa ya ulaya na magharibi ambao wao hununua malighafi nchini kisha kutengeneza bidhaa na hatimaye kutuuzia tena bidhaa.
Tatizo lilipo…
Mapinduzi ya viwanda huambatana na kukua kwa sayansi na teknologia, hivyo basi hatuwezi kufanya mapinduzi ya viwanda nchini Tanzania hali ya kua bado tupo nyuma sana au hatukimbizani na ukuaji wa dunia ya leo wa sayansi na teknologia.
Uendeshaji wa viwanda hauhitaji pesa ya mtaji pekee bali pia unahitaji watu ambao wamebobea kikamilifu kwenye tasnia hiyo. Pia unahitaji watu ambao wanataaluma kubwa sana na kitu au bidhaa ambayo kiwanda anataka kuzalisha.
Nini kifanyike...
Serikali iandae mkakati yakinifu wa kuhakikisha au kutoa dira iliyonyooka ya kuifikia ndoto adhim na yenye malengo thabiti ya kugeuza uchumi wa Tanzania na kua ya viwanda.
Kutokana na uchache wa wataalam husika serikali itoe fursa kwa wanafunzi wanahitimu kidato cha sita, wachukuliwe baadhi ya wachache kati ya hao wanafunzi na kuwasomesha vyuo vikuu nje ya nchi. Vyuo hivyo viwe ni vile ambavyo vinatoa elimu sahihi kwa vitendo kiasi ambacho mwanafunzi atakapohitimu chuoni hapo awe na ujuzi au ataalamu wa kile alichosomea.
Serikali isimamie na kuhakikisha inawasomesha wanafunzi hao kwa pesa za serikali na mara baada ya masomo yao ya chuo kikuu, serikali itafute kazi ya kujitolea kwa wanafunzi hao kwa muda usiopungua miaka miwili au miezi 18 ndani ya nchi ambayo vijana hao wamesoma, au katika nchi nyingine yeyote ambayo imeendelea kiuchumi wa viwanda ili vijana hao wawe na uwezo mkubwa na weledi wa kuzalisha bidhaa husika.
Serikali ianzishe sera inayowapunguzia ushuru na gharama kubwa za wawekezaji wa viwanda. Hili litasaidia wawekezaji wengi kuanzisha viwanda nchini na kupelekea watanzania kupata fursa za kuajiriwa katika viwanda hivyo kisha baadae hata wantanzania wenyewe watapoanzishisha viwanda vyao wenyewe, wataalamu na wazoefu watakua wanapatikana nchini.
Serikali ianzishe sera ya kukaribisha wawekezaji wa viwanda kwa mkataba wa muda fulani na kuajiri asilimia hitajiki ya wafanayakazi kutoka ndani ya Tanzania. Serikali ihakikishe inaingia kunako mkataba na wawekezaji ambao utasaidia watanzania wenye taaluma katika tasnia fulani kuweza kuajiriwa. Kisha serikali na wawekezaji wakifikisha muda wa kumaliza mkataba wa uwekezaji viwanda hivyo vibaki chini ya serikali, ndipo yitakapokua tayari vinamilikiwa na serikali ya Tanzania kwa manufaa ya watanzania.
Serikali ianzishe sera ya kua na viwanda vya Umma.
Sera hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kwani vijana watakao toka nje kimasomo watakua wanaajiriwa kwenye viwanda hivyo na kupelekea kuimarika kwa viwanda nchini.
Kutokana na serikali kuanzisha viwanda vya Umma, malighafi zote zilizokua zikinunuliwa na kusafirishwa nchi za nje zitakua zinasalia nchini na kuzichakata kisha kuzalisha bidhaa ya mwisho hatimae kuuza bidhaa hizo nje ya nchi na kujiongezea pato la taifa

Upvote
0