Mapinduzi ya Zanzibar: Ukweli ni Upi?

Mapinduzi ya Zanzibar: Ukweli ni Upi?

Wana bodi, japo tuko kwenye harakati za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge, kuna swali linanitatiza kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar, ambapo majibu yake sahihi, pia yanaweza kuwa ni kiashiria tosha cha mshindi wa urais wa Zanzibar, iwapo uchaguzi utakuwa huru na wa haki.

Swali hili lahusu ukweli haswa kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964, baada ya kuibuka kwa kitabu kingine kiitwacho 'Kwaheri Ukoloni Zanzibar, Kwaheri Uhuru Zanzibar' kilichoandikwa na Mwanazouni wa Zanzibar, Dr. Harith Ghassany, kama kilivyofanyiwa mapitio na mwandishi Mohamed Said, kwenye gazeti la Al-Nuur la leo.

Ghasanny anasema kumbe mapinduzi ya Zanzibar yalitekelezwa na askari mamluki wa Kimakonde (Wakata Mkonge) ambao waliongozwa na Mzee Mohamed Omar Mkwawa (Tindo) chini ya Amiri Jeshi wa jeshi la mamluki hao Victor Mkello (RIP). (kumbe am,iri jeshi hakuwa Okello peke yake, pia Mkello yumo?.).

Mamluki hao walitumia zana zao za kukatia mkonge, zile sime za makali kuwili, walizisunda kwenye nguo zao za ndani na kusafirishwa kwa mitumbiwi usiku usiku kupitia Kipumbwi. Wale mashuhuda wa mapinduzi yale matukufu, wanayakubali haya?.

Pia mwandishi anamalizia kwa kusema hata mauaji ya Karume, haykutekelezwa na wapinga mapinduzi, bali ni miongoni mwa hao hao wanamapinduzi, baada ya kupishana kauli fulani fulani za uendeshaji wa Zanzibar baada ya Mapinduzi.

Nimesoma kitabu cha John Okello kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar, yeye anasema yake, vitabu kadhaa vya waandishi wazungu wanasema yao, historia tukuka ya mapinduzi hayo nayo inasema kivyake, hivi hakuna any straight line yoyote kuhusu Mapinduzi hayo, yalipangwa na nani, yalitekelezwaje, nini haswa kilichotokea, nani alifanya nini wapi? na wahanga ni kina nani haswa?.

Majibu ya maswali haya yatasaidia kujua mustakabali wa matokea ya uchaguzi wa Zanzibar kudhirihisha kuwa Wazanzibari ni wamoja, hakuna kundi la walishiriki Mapinduzi ndio wenye uhalali zaidi kuitawala Zanzibar kuliko wasioshiriki, after all kumbe Mapinduzi yenyewe, yametekelezwa na askari mamluki wa Kimakonde, toka mashamba ya mkonge Tanga!.
Maswali kuhusu Mapinduzi Matukukufu ya Zanzibar, bado ni mengi kuliko majibu!.

Nawatakia Maadhimisho mema ya sherehe ya kumbukumbu ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar!.

Pasco
 
Hili bandiko lina miaka 8 humu, na maswali haya bado yapo na bado hayana majibu ya kutosheleza.

Hata hivyo natuma salamu za pongezi ya miaka 54 ya Mapinduzi, matukufu ya Zanzibar kwa Wanzibari wote, Wazanzibara na Wapemba, japo hawakushiriki Mapinduzi.

Mapinduzi Daima.

P
 
Ukimsoma vizuri mwandishi nguli wa makala kwenye gazeti la raia mwema ndg Joseph Mihangwa utaujua ukweli kuhusu mapinduzi.
 
Ukimsoma vizuri mwandishi nguli wa makala kwenye gazeti la raia mwema ndg Joseph Mihangwa utaujua ukweli kuhusu mapinduzi.
Nakumbuka kumsoma gezatini, kama mada uliletwa humu naomba link.

P.
 
Dr. Ghassany.
Katika kitabu chake yeye alifanya kazi ya kuchukuwa maelezo ya wahusika na kuyaweka kama kumbukumbu. Sijaona pahali anatowa maelezo yake binafsi katika mirengo yeyote lbda watu wamemuelewa tofauti. Yeye mwenyewe amesisitiza kufanywe utafiti wa kina ili watanzania wawe na uwelewa mpana kuhusu mapinduzi.

Sema kwasababu huyu Dr. Ghassany kajitambulisha kuwa ni mzanzibari na rangi yake ile ya kipemba pemba hivi ndio hizi chuki za kibongo unazozionesha hapa.
 
Ni watu wa Okello na planner mkubwa alikuwa Mwalimu Nyerere. Kuna clip ya (motion picture) iliyochukuliwa na helikopta (au ndege ndogo) iliyotoka katika manowari ya Australia (au Uingereza?) iliyokuwa jirani na Zanzibar siku hiyo ambayo ilichukuwa picha kutoka angani ikionyesha jinsi Waarabu (wakiwemo wanawake na watoto) walivyokuwa wanakimbizwa na watu wenye bunduki kuelekea ufukweni ambako huko walikuta makaburi (mass graves) yaliyochimbwa tayari na kumiminiwa risasi na kuangukia humo. Kulikuwa hakuna mapanga -- nadhani zilikuwa ni bunduki aina ya Marker Four. Hivi yale makaburi hayakupatikana?

Mwenye clip hii atuwekee hapa -- kwa upande mmoja inasikitisha sana maana ilikuwa kama vile (nimeiona picha moja) ya wale askari wa kiNazi wa Hitler walivyokuwa wakiwaua Wayahudi baada ya wao kulazimishwa kuchimba makaburi (mass graves) na kisha kuvuliwa nguo zote huku wanawake wakiwabeba vichanga vyao! Lakini hii ndiyo historia ya dunia, lakini huko kwenye karne za nyuma zaidi ukatili ulikuwa mkubwa zaidi.
Nasikitika sana kwa kuharibika kompyuta yangu hii video unayoizungumzia hapa nilikuwa nayo. Inasikitisha sana watu wengi walipoteza maisha kwenye fukwe za bahari.
 
Kikundi cha John Okello, Kundi la Wakommunist chini ya Babu na Vijana wa ASP walioasi msimamo wa ASP kutaka kuingia madarakani ndio waliofanya MAPINDUZI ila kikundi cha kwanza kuanza kufyatua risasi ndipo penye utata hapo
 
Nyerere ndie aliefanya mapinduzi Zanzibar. Na ndio ukaanza utawala wa Tanganyika ndani Zanzibar Mpaka hii leo.
 
Nawatakia kumbukumbu njema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyovikomboa visiwa hivi.
P
 
Today’s official slogan in Zanzibar is “Mapinduzi daima!” (Revolution forever!). Revolution, Yes! But Zanzibar, Tanzania and the rest of Africa needs a Mapinduzi ya Mawazo (Mental Revolution), to learn from the past, to appreciate the present and to plan and work for a better future!
 
Hahaha kaka ili usiitwe tena kuhojiwa na Bunge, kubali yote unayoyasikia. Chama cha mapinduzi nao wanasemaga ndio walileta ukombozi. Ukiwasikiliza ccm wanakueleza eti Karume aliongoza mapinduzi takatifu. Waliisha sema na kutunga sheria kwamba wao tu ndio husema ukweli, wengine wote hamruhusiwi kuhoji wala kupinga wasemalo wao.
Nakumbuka marehemu Mtikila katika harakati zake kudai usajili wa DP aliwahi kuambiwa kwamba alisema uongo kwasababu aliyoyasema hayakuwa kwenye kiapo. Mtikila akamuuliza Marehemu jaji Lihundi yani uongo nikiusema chini ya kiapo unabadirika kua ukweli?! Na akiwa hapo hapo mahakamani akaomba aende kwenye kizimba aape, na aliomba muda wote aongee akiwa kizimbani ili Lihundi amuamini, hahaha jamaa alikuwa matata. Anyway wao tu ndio wakweli kaka.
 
Historia haijulikani kwasababu kumekuwa na version tofauti kuhusu nini kilijiri nani alihusika na kwa vipi. Mimi binafsi nimesoma theory kama 3 ambazo zote zinachanganya tu. Wajumbe wa baraza la mapinduzi, ambao wanajua jinsi ''tombola'' lilivyopangwa, baadhi wapo hai kabisa, hawa wasipobanwa kueleza ukweli historia itafutika. Sina uhakika lakini nadhani wafuatao wanaweza kuwemo katika baraza la mapinduzi au wanajua nani alikuwemo: Mzee Hassan N Moyo, Abdalah Natepe, Aboud Jumbe, Ali Hassan M,
Natepe alishafariki mwaka Jana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu, habari Kuna sehemu nimepitia nikaona kuwa John okelo ndiye rais wa kwanza wa zanzibar, wakati tunajua kuwa ni Karume, mwenye kujua hili atusaidie,wakuu
 
Back
Top Bottom