Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
- Thread starter
-
- #21
Maswali kuhusu Mapinduzi Matukukufu ya Zanzibar, bado ni mengi kuliko majibu!.Wana bodi, japo tuko kwenye harakati za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge, kuna swali linanitatiza kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar, ambapo majibu yake sahihi, pia yanaweza kuwa ni kiashiria tosha cha mshindi wa urais wa Zanzibar, iwapo uchaguzi utakuwa huru na wa haki.
Swali hili lahusu ukweli haswa kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964, baada ya kuibuka kwa kitabu kingine kiitwacho 'Kwaheri Ukoloni Zanzibar, Kwaheri Uhuru Zanzibar' kilichoandikwa na Mwanazouni wa Zanzibar, Dr. Harith Ghassany, kama kilivyofanyiwa mapitio na mwandishi Mohamed Said, kwenye gazeti la Al-Nuur la leo.
Ghasanny anasema kumbe mapinduzi ya Zanzibar yalitekelezwa na askari mamluki wa Kimakonde (Wakata Mkonge) ambao waliongozwa na Mzee Mohamed Omar Mkwawa (Tindo) chini ya Amiri Jeshi wa jeshi la mamluki hao Victor Mkello (RIP). (kumbe am,iri jeshi hakuwa Okello peke yake, pia Mkello yumo?.).
Mamluki hao walitumia zana zao za kukatia mkonge, zile sime za makali kuwili, walizisunda kwenye nguo zao za ndani na kusafirishwa kwa mitumbiwi usiku usiku kupitia Kipumbwi. Wale mashuhuda wa mapinduzi yale matukufu, wanayakubali haya?.
Pia mwandishi anamalizia kwa kusema hata mauaji ya Karume, haykutekelezwa na wapinga mapinduzi, bali ni miongoni mwa hao hao wanamapinduzi, baada ya kupishana kauli fulani fulani za uendeshaji wa Zanzibar baada ya Mapinduzi.
Nimesoma kitabu cha John Okello kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar, yeye anasema yake, vitabu kadhaa vya waandishi wazungu wanasema yao, historia tukuka ya mapinduzi hayo nayo inasema kivyake, hivi hakuna any straight line yoyote kuhusu Mapinduzi hayo, yalipangwa na nani, yalitekelezwaje, nini haswa kilichotokea, nani alifanya nini wapi? na wahanga ni kina nani haswa?.
Majibu ya maswali haya yatasaidia kujua mustakabali wa matokea ya uchaguzi wa Zanzibar kudhirihisha kuwa Wazanzibari ni wamoja, hakuna kundi la walishiriki Mapinduzi ndio wenye uhalali zaidi kuitawala Zanzibar kuliko wasioshiriki, after all kumbe Mapinduzi yenyewe, yametekelezwa na askari mamluki wa Kimakonde, toka mashamba ya mkonge Tanga!.
Nawatakia Maadhimisho mema ya sherehe ya kumbukumbu ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar!.
Pasco