Ahlan,Mkuu Ndahani
Baada ya maamkizi hayo kwa hisani ya Nguruvi3
Tanganyika ilikwenda wapi baada ya 1964?
Mkuu Tanganyika ilifanyiwa usanii tu.
Je unatambua jina la asili la Muungano? Kama umelisahau, Jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar...Jina hili lilifanyiwa uchakachuaji, mizengwe, mazingaombwe, kiini macho au tuseme usanii likaopolewa Jamhuri ya Muungano wa Tan+Zan+ ia.
Huo ulikuwa uchakachuaji nambari moja, uchakachuaji nambari mbili ni ile sehemu inayoitwa Tanganyika,(iliyofupishwa kuwa Tan kuitwa Bara au Tanzania bara.
Wapi umepata kusikia kuwa mwanachama wa Muungano anapotea?
Muungano wa Tanzania una wanachama wangapi?
UK ambayo inatumia mfumo wa unitary gvt ina wanachama wake, England, Scotland, Wales na annexed-Nothern Ireland.
Usirudi na usanii kusema Tanzania ina wananachama wawili, Bara na Zanzibar.
Umempongeza Barubaru juu ya umuhimu wa elimu. Tumia elimu yako sasa kutafuta jibu hapo. Sio lazima kurudi hapa kujibu.
Ukivunjika Muungano kesho huyu mwanachama aliyeungana na Zanzibar hatotumia jina lake la asili(Tanganyika)?
Katika Muungano yapo mambo yanayoitwa mambo ya Muungano, halafu kuna mambo ambayo kila mwanachama wa Muungano ana mambo yake kivyake. Hutopata tabu kusema kuna mambo ya Zanzibar. Je mambo ya Tanganyika utasema ni mambo ya nani? Bara? Tanzania bara? au ya yule mwanachama aliyeungana na Zanzibar na kukubaliana kuwa kuna mambo hayatokuwa ni mambo ya Muungano?
Hivi Zanzibar iliungana na nani? Basi hayo mambo hapa yatakuwa ya huyu uliyemtaja.
Mtu hahitaji darubini kuona kuwa msuguano kama ulikuwa haupo Tanganyika basi sasa unajengeka.
Unauliza; "ntaanzia wapi mkuu?"
Barubaru ametahadharisha tusifiche maradhi.
Kuna haya yanayojiri Tanganyika.
1.Ndugu zake Mkandara wanataka mahakama ya kadhi, ambayo ilikuwepo mwanzoni, irejeshwe tena.
2.Kuna shule za kiislamu zinalalamikia matokeo ya mitihani.
3.Kuna BAKWATA wanataka kipengele cha dini ya raia kiingizwe kwenye sensa au itahamasisha waunga mkono wao kususia/ kugomea sensa.
4.Kuna MOU ya serikali na kanisa amabyo inalalamikiwa na wasio na MOU na serikali.
5.Kauli aliyoitaja Barubaru kuhusu Mzee Edwin Mtei na wingi wa wajumbe wa dini moja.
6.Malalamiko ya teuzi anazofanya Kikwete. kwa hili fungua mada zinazotaarifu teuzi za rais hapa JF.
7. Malalamiko kuwa kuna idadi ndogo ya wabunge wa imani moja bungeni.
8. Malalamiko kuwa Serikali inaendeshwa kwa mfumo-kristo.
9. Kauli kuwa CUF ni ya wavaa kanzu chafu na vibaragashia na kauli kuwa CHADEMA ni cha wakristo au watu wa kanda za juu,kaskazini.
10. Kauli zinazotoka za kuwa UAMSHO wanachoma moto makanisa ya "machogo" ambazo pia zinachukua sura ya "waislamu vs wakristo"
11. Kauli za dharau kuhusu/dhidi ya wanamadrasa kwa upande mmoja na "wanaona nchi hii kuwa ni mali yao" kwa upande mwingine.
Hata kama haya yote si kweli, yawe ni matamshi yanayoelea hewani tu, lakini ni vyema kuwa na tahadhari, kwani maumivu ya kichwa huanza pole pole.
Kukana kuwa hakuna msuguano unaojengeka ni kujifanya mbuni. Kuzika kichwa mchangani, udongoni huku mwili wote uko nje!
Pale penye kasoro ni vyema kufanyiwa kazi kurekebisha kasoro hizo kwa manufaa ya jamii.