tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
Kesi ya kupinga kuenguliwa kwa mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ACT Wazalendo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu (2025), iliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini wa chama hicho na Luhaga Mpina dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imeendelea kwa njia ya mtandao leo, Jumatano Septemba 03.2025 chini ya Majaji watatu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu Dodoma
Soma pia: Monalisa Ndala: Mpina hastahili na hana sifa kugombea urais ACT Wazalendo
Miongoni mwa yaliyojitokeza Mahakamani hapo leo ni pamoja na upande wa serikali kuamua kuondoa mapingamizi waliyokuwa wameweka awali kuhusiana na kesi hiyo, hatua ambayo imeongeza urahisishaji wa kusikiliza kesi ya msingi, ambapo sasa Mawakili wa pande zote mbili watakutana Mahakamani Jumatatu ya juma lijalo kufanya mjumuisho wa hoja zilizowasilishwa kwa maandishi Mahakamani hapo
===
Kesi ya kupinga uamuzi wa Tume ya Huru ya Taifa Uchaguzi (INEC) imesikilizwa leo katika Mahakama Kuu, Masijala Kuu ya Dodoma kwa njia ya mtandao, ambapo baada ya Serikali kuwasilisha hoja zake, imesogezwa tena hadi Septemba 8, 2025.
Kesi hiyo inahusu malalamiko yaliyowasilishwa na mgombea urais wa Chama cha ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina, akipinga uamuzi wa Tume kuzuia urejeshaji wa fomu za uteuzi.
Awali Agosti 28, mawakili wa Serikali waliomba siku 14 za kujibu malalamiko hayo, hata hivyo mahakama hiyo iliwakatalia na kuwataka wajibu ndani ya siku tano.
Akizungumza kwa simu leo Septemba 3, Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano wa ACT Wazalendo, Shangwe Ayo aliyekuwa mahakamani hapo, amesema mawakili wa Serikali walikuja na mapingamizi ambayo hata hivyo hayakuwekwa wazi.
Amesema wakili anayeiwakilisha ACT Wazalendo, John Seka alipinga kufichwa kwa mapingamizi hayo.
“Ndipo mahakama iliahirishwa hadi saa 8 mchana. Iliporudi mawakili wa Serikali waliomba kuondoa mapingamizi yao.
“Baada ya mapingamizi ya Serikali kuondolewa, mahakama iliamuri kesi ya msingi ianze kusikilizwa. Lakini mawakili wa Serikali waliomba tena siku 14 za walalamikaji kuleta maombi yao na siku nyingine 14 za wao kuyajibu.
“Hata hivyo, wakili Seka alipinga hoja hiyo akisema kesi hiyo imefunguliwa kwa hati ya dharura na kwa kuwa ni ya uchaguzi ratiba inaendelea.
“Alisema mpaka sasa zimepita siku saba za kampeni na mgombea hajafanya kampeni na hajui kuhusu usiri wa karatasi za kupigia kura, hivyo anahitaji kupata haki yake mapema,” alisema.
Amesema baada ya hapo, majaji walikubaliana na upande wa walalamikaji wakisema kesi hiyo inahusisha haki za wananchi.
“Majaji, wakaja na maoni kwamba wanatambua haki za mgombea na kesi hiyo ina haki za wananchi.
“Hivyo majaji waliagiza upande wa walalamikaji walete malalamiko yao ndani ya siku mbili, yaani Septemba 5 na wajibu maombi wajibu hadi septemba 7, halafu Septemba 8 mahakama itasikiliza pande mbili ana kwa ana na kisha watataja siku ya kutoa uamuzi,” alisema.