Matojo Cosatta
JF-Expert Member
- Jul 28, 2017
- 234
- 390
MAPINGAMIZI YA UCHAGUZI NA HAKI YA KUWAKILISHWA NA MWANASHERIA
Ni raia yangu kuwa wagombea Urais, ubunge na Udiwani wapewe haki ya kuwakilishwa na wanasheria hususani mawakili katika mchakato mzima wa Uchaguzi na hususani katika kuweka, kusikiliza na kufanyia uamuzi mapingamizi na kukata na kusikiliza rufaa za mapingamizi ili kutenda haki kwa wagombea ambao sio wanasheria wakati wanapokabiliana na wagombea ambao ni wanasheria. Kuna mwamko mkubwa sana wa wanasheria kugombea nafasi za kisiasa mwaka huu na mwamko huu utaongezeka mara dufu katika uchaguzi mkuu ujao na uchaguzi kuu zitakazofuata baada ya hapo. Hivyo, ni muhimu wagombea Urais, ubunge na Udiwani wapewe haki ya kuwakilishwa na wanasheria hususani mawakili katika mchakato mzima wa Uchaguzi.
Piga picha mgombea ambaye sio Mwanasheria akutane na mgombea ambaye ni mwanasheria mbobezi wa sheria za uchaguzi kwenye shauri la kusikiliza mapingamizi mbele ya Tume ya Uchaguzi, Msimamizi wa Uchaguzi au Msimamizi Msaadizi wa Uchaguzi. Hapa mgombea ambaye sio Mwanasheria akitana na mgombea ambaye ni mwanasheria mbobezi wa sheria za uchaguzi kwenye shauri la kusikiliza mapingamizi huyu mgombea ambaye sio mwanasheria atakuwa mdogo sana kama pilitoni.
Pia, mgombea ambaye ni mwanasheria mbobezi wa sheria za uchaguzi kwenye shauri la kusikiliza mapingamizi atamdhibiti Msimamizi wa uchaguzi au Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ambaye sio mwanasheria kihoja, kiakili na kihisia kwa kuwa Msimamizi wa uchaguzi au Msimamizi wa Uchaguzi atapoteza kujihamini (confidence) na atajiona mnyonge (inferior) mbele ya mwanasheria mbobezi wa sheria za uchaguzi na mwanasheria huyo anaweza kumpotosha kwa makusudi Msimamizi wa uchaguzi au Msimamizi wa Uchaguzi kutoka na uelewa wake mdogo wa sheria za uchaguzi. So the lawyer stands in the best position to dominate the will of Returning Officer or Assistant Returning Officer during hearing of election objections.
Kwa mfano, piga picha Prof. Lipumba au Dr. Magufuli akutane na Tundu Lissu kwenye kusikiliza shauri la mapingamizi mbele ya Tume ya Uchaguzi wakati Prof. Lipumba ni mchumi mbobezi na Dr. Magufuli ni mkemia mbobezi kwa upande mmoja na Tundu Lissu ni mwanasheria mbobezi wa sheria za uchaguzi kwa upande mwingine, hii ni sawa na mechi kati ya Yanga SC dhidi ya Barcelona FC na sio haki kuwapambanisha watu hawa katika mapambano ya pingamizi za uchaguzi ambazo kwa asili ni swala la kisheria kwa sababu mwanasheria atakuwa na faida isiyokuwa ya haki (unfair advantage) ya kitaaluma dhidi ya mkemia na mchumi. Hivyo basi, haki ni kwamba Dr. Magufuli awakilishwe na Prof. Kabudi na Prof. Lipumba awakilishwe Fatma Karume kwa upande mmoja wakapambane na mwanasheria mwenzao Tundu Lissu kwenye vita ya mapingamizi ya kiuchaguzi.
Mfano hai ni jimbo la Lupembe ambapo mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM Wakili na Wanasheria Enosy Edwin Swalle amemsambalatisha kwa mapingamizi mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya Chadema, Ndugu Edson Ezekiel D'zombe katika ngazi zote kwa maana ya ngazi ya Jimbo kwa Msimamizi wa uchaguzi na katika ngazi ya taifa katika rufaa mbele ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Ni ushauri wangu kwa Tume ya Uchaguzi kubadilisha Kanuni za Uchaguzi au Bunge kuifanyia marekebisho Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sura ya 343 na Sherai ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292 ili wagombea Urais, ubunge na Udiwani wapewe haki ya kuwakilishwa na wanasheria hususani mawakili katika mchakato mzima wa Uchaguzi na hususani katika kuweka, kusikiliza na kufanyia uamuzi mapingamizi na kukata na kusikiliza rufaa za mapingamizi ili kutenda haki kwa wagombea ambao sio wanasheria wakati wanapokabiliana na wagombea ambao ni wanasheria.
Imeaandikwa na Matojo M. Cosatta.