Mapishi mbalimbali ya Karanga za kukaanga

KakaJambazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2009
Posts
18,804
Reaction score
12,227
Naomba wataalam wa kutengeneza zile karanga flani ivi zinakua sijui na mayai ambazo naziona kwenye masuper market au sherehe ambalo wanaita bites anipe recipe yake tafadhali.

CC gfsonwin ladyfurahia charminglady Madame B etc

=================================================



 
Last edited by a moderator:
Karanga ninazozijua mm ambazo zinawekwa kwenye masupa maketi mengi
zinatengenezwa hivi:

vitu:
- karanga mbichi kilo 10
- chumvi kiasi
- Mayai 20pcs

Utayarishaji:
Chukua karanga zako zichambue na ondoa uchafu kisha ziweke kwenye kikaango, weka chumvi kiasi
kisha chukua mayai yako yagonge pembeni kisha weka katika hizo karanga hakikisha zote zinapata mayai

chukua kikaangio kisha anza kukangaa hizo karanga hakikisha zinakuwa za uzurungi kiasi epuka zisiungue kwani
zitaondoa radha yote ya utamu wa karanga, ukimaliza epua na weka kwenye sahani tayari kwa kula
waweza kula na juice, soda, chai ya maziwa na hata maji ukipenda
MPAKA HAPO UMESHANIELEWA KIDOGO ANZA MAANDILIZI YA KUTENGENEZA KARANGA ZAKO
Naomba wataalam wa kutengeneza zile karanga flani ivi zinakua sijui na mayai ambazo naziona kwenye masuper market au sherehe ambalo wanaita bites anipe recipe yake tafadhali.

CC gfsonwin ladyfurahia charminglady Madame B etc
 


Asante ladyfurahia

Nshaiprint kwa ajili ya wkend.
 
Last edited by a moderator:
Mahitaji
-karanga kilo moja
-mayai 2-3 inategemea na ukubwa
-chumvi kijiko kimoja
-sukari kiasi unachohitaji
-unga wa ngano robo kilo(kidogo tu)

Kuandaa
-chukua karanga weka katika sinia, chambua kuondoa karanga mbovu,zilikatika na taka taka.
-baada ya kuchambua weka katika bakuli au chombo cha kukandia, piga mayai katika chombo pembeni na uweke chumvi. Tia mayai katika karanga na kisha zichanganye kuhakikisha zote zimekolea mayai.
-chukua kiasi cha sukari unachokadiria kitakufaa Tia katika ule mchanganyiko wa karanga,mayai na chumvi kisha changanya ili sukari inate katika karanga zote.
-
-
-
-
 
Mahitaji:
-Karanga kilo moja.
-Mayai 2-3 inategemea na ukubwa.
-Chumvi kijiko kimoja.
-Sukari kiasi unachohitaji.
-Unga wa ngano robo kilo(kidogo tu).
-Mafuta ya kupikia.

Kuandaa:
-Chukua karanga weka katika sinia, chambua kuondoa karanga mbovu,zilikatika na taka taka.
-Baada ya kuchambua weka katika bakuli au chombo cha kukandia, piga mayai katika chombo pembeni na uweke -Chumvi. Tia mayai katika karanga na kisha zichanganye kuhakikisha zote zimekolea mayai.
-Chukua kiasi cha sukari unachokadiria kitakufaa Tia katika ule mchanganyiko wa karanga,mayai na chumvi kisha -Changanya ili sukari inate katika karanga zote.
-Chukua unga Tia Katika mchanganyiko wako, changanya vizuri kuhakikisha karanga zote zimekuwa nyeupe kwaku funikwa na unga.
-Weka mafuta kiasi kwenye kikaango, yakichemka anza kukaanga karanga zako hakikisha unazitoa kabla hazijawa Brown sana usijeunguza karanga zako

 

Attachments

  • IMAG0298.jpg
    329.7 KB · Views: 2,142
  • IMAG0300.jpg
    242.5 KB · Views: 1,843
Thank you,nlikua natafuta hii kitu
 

samahani....mafuta yanakua ya kuloweka au una kaanga kama kwa mafuta kidogoo kama unakaanga dagaa wa mwanza?
 
Asante sana kwa kunifundisha leo nime zipka, 2mezilaaaaaaaaa, yani ni tam kwelkwel.
 
samahani....mafuta yanakua ya kuloweka au una kaanga kama kwa mafuta kidogoo kama unakaanga dagaa wa mwanza?
mafuta kiasi tu karanga ukiziweka zinaiva bila shida unaendelea kuzigeuza tu. Hujitaji mafuta mengi kama ya maandazi ila hakikisha zote zimo ndani ya mafuta
 
Pia unaweza kuziandaa kwa njia hii..
- Chukua karanga ziloweke kidogo kwenye maji yenye chumvi kiasi
-zikaushe kwenye kikaango
-vunja yai kisha uchanganye na sukari koroga mpaka mchanganyiko upate rangi nyeupe
-tia karanga zako kwenye mchanganyiko wa yai na sukari
-nyunyizia unga wa ngano kwene mchanganyiko wako kisha ukaange kwa deepfry

-zikiwa brown ipua tayari kwa kula na juisi pia soda!@KakaJambazi
 
ladyfurahia...ndio zinaitwaje. Karanga huwa nazila kama butter tu. Sina ujuzi nao zaidi.....
 
Last edited by a moderator:
Hizi vitu ni tamu sana mpaka raha
sasa pembeni uwe na maji ya Kilimanjaro
bariidii .
 

Nakushukuru sisy kwa kumjibu mtoa mada!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…