Mapishi ya Chapati: Jikoni kwa Evelyn Salt & Mentor

Mapishi ya Chapati: Jikoni kwa Evelyn Salt & Mentor

Mentor

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2008
Posts
20,328
Reaction score
23,909
Salaam!

Tangu kuzaliwa kwangu nimeshapika vyakula vingi. Hata hivyo (nadhani kwa kutokana na kuzaliwa wa kiume) sikuwahi kupika chapati. Niliaminishwa mapishi ya chapati yana utaalamu ambao ni binti wa kike, tena waliofundwa vyema, wenye kuuweza.

Na ninakiri, ukimpata binti anayejua kupika chapati laini zenye layers zinazoonekana, basi huyo muoe hahah.

Anyway, leo nilimuomba mke wangu Evelyn Salt anifundishe mapishi ya chapati. Na huu ni mrejesho wa mapishi yenyewe. Nathibitisha kuwa hajagusa chochote, nimepika kila kitu kutoka mwanzo hadi mwisho, ila maelekezo yote niliyapata kwake. Muda wote alikuwa pembeni akinywa wine...

IMG_20170106_192643.jpg

1. Kama kawaida yetu tunaandaa mahitaji yote na kuyaweka mezani kabla ya kuanza mapishi. Hii inakuhakikishia kuwa una kila unachokihitaji kabla hujaanza. Isijetokea ukahitaji mafuta kumbe huna na ulishaanza kupika/kuandaa.

Mahitaji: Unga wa ngano (au kwa nchi za wenzetu wanatumia all-purpose flour), mafuta ya kupikia, chumvi, sukari, maji, bakuli, frying pan (kiswahili?), kikombe na kijiko cha kupimia, brush ya kupakia mafuta, mikono misafi, kibao/meza safi ya kukandia na kile kimbao cha kukandia (sifahamu jinale sanifu).

IMG-20170106-WA0110.jpg

JINSI YA KUANDAA:

2 (a). Anza kwa kutia vijiko vinne vya mafuta ya kupikia kwenye sufuria na kuyapasha moto

2 (b). Kisha pasha maji yako kuwa ya vuguvugu

3. Pima vikombe viwili vya unga kwenye bakuli.

4. Ongeza kijiko kimoja cha chai cha chumvi

5. Ongeza 'pinch' (yaani chukua kwa vidole viwili) ya sukari

6. koroga pamoja mchanganyiko wako kuhakikisha chumvi na sukari vimechanyangika vyema na unga wako.

IMG_20170106_114439.jpg

7. Ongeza mafuta yako (vijiko vinne vya mafuta ya kupikia ulivyokwisha kuvichemsha 2 (a)) Kisha uendelee kuuchanganya mchanganyiko wako. Sasa unaweza kutumia mikono kuchanganya mchanganyiko wako. Fanya hivyo kwa dakika mbili hadi tatu. Jitahidi kuhakikisha sehemu kubwa ya unga imeshika mafuta. (mchanganyiko wako utakuwa na vibonge bonge, usihofu)

IMG_20170106_115727.jpg

8. Ongeza robo tatu ya kikombe cha maji yale ya vuguvugu (hatua 2 (b)) na kisha uanze kuukanda unga wako. Dakika moja ya mwanzo unaweza kukata tamaa maana unga wako utashikana sana na mikono na chombo chako, usihofu.

9. Ongeza unga kidogo kidogo huku ukiendelea kuukanda unga wako. (kipimo cha kidogo kidogo ni kuchukua unga kwa vidole vyako vyote vitano - vidole, sio mkono). Kwa njia hii hutajikuta umepitiliza kuweka unga mwingi. Endelea kufanya hivi kwa dakika si chini ya tano. Baada ya hapa, unga wako utakuwa umeachana na sufuria na mkono wako.

10. Toa unga wako kutoka kwenye bakuli na uuweke juu ya meza yako safi au tumia kibao cha kukandia (hakikisha usafi wa eneo utakalofanyia kazi). Nyunyiza unga juu ya eneo hilo kisha endelea kuukanda unga wako. Endelea kukanda huku ukinyunyiza unga kila wakati. Fanya hivi kwa dakika zisizopungua 15. Kuwa mwaminifu kwako mwenyewe wakati wa kukanda usifanye tu ili kumaliza dakika 15, ila hakikisha unaukanda vyema.

11. unda mpira/tufe wa mchanganyiko wako na kisha utie ndani ya bakuli lako uliloanzia nalo kuchanganyia.

12. Kwa kutumia brashi yako, paka sehemu ya juu ya tufe lako mafuta kiasi, kisha funika bakuli lako kwa kitu chochote ambacho hakitaruhusu kupitisha hewa. Acha kwa dakika zisizopungua 30.

IMG_20170106_135222.jpg

IMG_20170106_123351.jpg

13. Baada ya dakika thelathini, toa tufe lako na uligawe katika vitufe vidogo vinne (kutokana na vipimo tulivyotumia).

14. tengeneza mduara kama unataka kupika chapati tayari. kisha upake mafuta kwa kutumia brashi yako. Mafuta kiasi tu.

IMG_20170106_135913.jpg

15. Kisha zungurusha kama unatengeneza kijiti (pipe). Baada ya hapo zungurusha tena 'pipe' yako katika mduara kisha kile kisehemu cha mwisho kichomeke chini ya mduara wako kama inavyoonekana kwenye picha ya chini.

IMG_20170106_141312.jpg

16. Funika tena na uviache kwa dakika zisizozidi 15.

17. Baada ya hapo tengeneza vitufe vyako kama chapati tayari kwa kupika. (muda wote unapotengeneza chapati zako hakikisha unanyunyizia unga kwenye meza/ubao wako).

18. Tengeneza chapati zako (hakikisha ile iliyokuwa ya kwanza kutengenezwa kwenye namba 15 ndiyo inaanza kutengenezwa/kupikwa) tayari kwa kupika. Jitahidi kutengeneza kuwa mduara.

IMG_20170106_143851.jpg

19. Tia frying pan yako kwenye jiko na hakikisha moto wako sio mkubwa (uwe wa wastani, sawa na namba tano kwenye jiko la umeme). Hakikisha pan yako ni kavu na haina mafuta wala majimaji.

IMG_20170106_144846.jpg

20. Acha kwa dakika moja kisha geuza chapati yako, ichome kwa dakika moja kisha kwa kutumia brashi yako paka mafuta kwenye sehemu ya juu. Geuza chapat yako na upake tena mafuta sehemu iliyopo juu. Subiri kwa dakika moja kisha geuza tena kwa dakika moja na utoe chapati yako tayari kwa kuliwa.

IMG_20170106_171042.jpg

21. Hakikisha unasafisha jiko lako baada ya kupika.

IMG_20170106_191149.jpg

Wasalaam wapendwa,
Mentor & Evelyn Salt.
 
Kuna uzi niliwahi kusoma hapa ulisema maji ya kukandia yawe ya baridi kiasi ndio chapati zinakuwa laini... hongera kwa mapishi

Nimegundua mapishi ya chapati ni mengi. Ila hii niliyoweka ni niliyoifanyia kazi mwenyewe, kwa mikono yangu, inatoa chapati nne na ukitaka ziwe nyembamba basi zitatoka sita.

Ni laini, na inakunjika vyema ingawa si laini kama chapati za kumimina.
 
Hongera zenu kwa kupika chapati mie baada ya kuona sizipendi hata kujifunza kupika nikaona uvivu
 
Hongera sana ,zina muonekano mzuri naamini ni tamu pia ..napenda sana chapati
 
Hongera zenu kwa kupika chapati mie baada ya kuona sizipendi hata kujifunza kupika nikaona uvivu

Jifunze um-surprise my-husband-wako.

Hongera
Ila katika kitu kilichinishinda kupika basi n chapati za kukanda aisee

Mhh! Walisema kipimo cha mke bora basi ni mapishi yake ya chapati, sasa kama hujui kupika kabisa...sijuiiii!!!
 
Kuna uzi niliwahi kusoma hapa ulisema maji ya kukandia yawe ya baridi kiasi ndio chapati zinakuwa laini... hongera kwa mapishi
Maji haijalishi yakiwa ya baridi (room temp) au ya vuguvugu, chapati ni ukandaji, pia chapati kuwa na layers ni lazima ikunjwe na wakati wakukunja unatumia mafuta ya samli. Chapati haitiwi sukari wala hiliki (kama nilivyoona kwenye uzi mmoja humu) hayo tena maandazi lol. Wengine huweka hadi mayai kama chapati za maji. Asikudanganye mtu, chapati wapishi ni ss watu pwani bwana wengine wanadandia tu.
 
Duh punguza majivuni spinderella my dear,

Sote tunajifunza. Kuhusu origin ya chapati hata hao wa pwani walikopa kutoka kwa wahindi wakaiboresha.

Si vibaya mtu akiongeza a pinch of suga ama iliki vyote ni ili kuboresha chapati yako. Akiweka yai ama maziwa na ikatoka chapati bado sijaona lililoharibika. Hakuna definition moja ya chapati.

Japokua hujaniita mimi huwa natumia maji ya baridi kabisa chapati zinatoka laini kabisa

Basi nadhani ni sahihi kuhitimisha kuwa ubaridi/jotoridi la maji haliathiri chochote kwenye chapati yako ila ukandaji wako.

Nashukuru kwa hili.
 
Maji haijalishi yakiwa ya baridi (room temp) au ya vuguvugu, chapati ni ukandaji, pia chapati kuwa na layers ni lazima ikunjwe na wakati wakukunja unatumia mafuta ya samli. Chapati haitiwi sukari wala hiliki (kama nilivyoona kwenye uzi mmoja humu) hayo tena maandazi lol. Wengine huweka hadi mayai kama chapati za maji. Asikudanganye mtu, chapati wapishi ni ss watu pwani bwana wengine wanadandia tu.

Duh punguza majivuni spinderella my dear,

Sote tunajifunza. Kuhusu origin ya chapati hata hao wa pwani walikopa kutoka kwa wahindi wakaiboresha.

Si vibaya mtu akiongeza a pinch of sugar ama iliki vyote ni ili kuboresha chapati yako. Akiweka yai ama maziwa na ikatoka chapati bado sijaona lililoharibika. Hakuna definition moja ya chapati.

Back
Top Bottom